Serikali Kujenga Kituo cha Michezo Manyara

Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye amesema serikali itajenga kituo cha michezo katika Mkoa wa Manyara ili kuacha kutumia kituo cha hifadhi ya mbuga ya Tarangire Mkoani humo.

Waziri Nape ameyasema hayo leo Bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA Martha Umbula aliyetaka kujua kuhusiana na ni lini serikali itajenga kituo cha mkoa cha michezo kitakachoweza kuwakusanya wanamichezo wengi kwa wakati mmoja kuliko ilivyo sasa.

''Serikali itajenga kituo hicho baada ya kupata eneo la kutosha kwani kujengwa kwa kituo hicho kutarahisisha upatikanaji wa ajira pamoja na biashara''Amesema Waziri Nape.

Aidha kufuatia swali hilo Mbunge wa Mbulu Lazaro Massey (CCM) amesema kwamba kuna uwezekano wa kupata ardhi bure kama serikali itaridhia kujengwa kwa kituo hicho katika wilaya ya Mbulu.

Waziri Nape akijibu swali hilo amesema kwamba kama ardhi ipo serikali itajenga kituo hicho wilayani humo ili kuweza pia kumuenzi kazi nzuri ya riadha aliyofanya Filbert Bay katikakuipatia heshima Tanzania.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad