Shilole Humfikii Vanessa Mdee Kwa Uzuri - Mashabiki Wagoma

Ikiwa zimepita siku kadhaa toka msanii Shilole afunguke kwenye kipindi cha 5Selekt kinachorushwa kwenye ting'a namba moja kwa vijana EATV kuwa hakuna msanii wa bongo fleva mzuri zaidi yake, mashabiki wameamua kutoa ya mioyoni.

Mashabiki wamemchana Shilole na kusema kuwa yeye si mwanamke mzuri katika wasanii wanaofanya bongo fleva huku wakisema kuwa uzuri wake hausofei kabisa kwa msanii Vanessa Mdee.

Baadhi ya mashabiki walikuwa wakimpa madongo kuwa mwanamke mzuri hawezi kujianika kama yeye, huku wengine wakisema kuwa mwanamke mzuri hawezi kuwa yeye kutokana na tabia yake ya kutojiheshimu na wengine wakisema kuwa yeye hana lolote na wa kawaida kabisa.

"Kuna manzi wakuitwa Vanessa cheki yule manzi alivyo mcute wewe nani wachakuji puraaaaaaaaaaa" Africanboihacker

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Vanessa Mdee hana uzuri wowote, mweusi ti

    ReplyDelete
  2. Vanessa mdee mwembamba kama ana ngoma vile

    ReplyDelete
  3. Shilole ndiyo mrembo na amefika Ulaya mara nyingi sana, lini Vanessa mdee amefika Ulaya? sababu Vanesa Mdee hajakaribishwa kuja Ulaya

    ReplyDelete
  4. ni kweli Vanessa Mdee mwembamba kama ana ngoma, Shilole mrembo pia amenona nona halafu ni mcheshi sana akilewa ndiyo maana nampenda Shilole

    ReplyDelete
  5. yaani wewe ni bogasi kabisa, Vanessa alikuwa anaishi hapa marekani kwa miaka mingi tu na usisahau baba yake alikuwa anafanya kazi ubalozi wa Tanzania, pia ni mwanamke ambaye anajiheshimu sana na anajitambua.

    ReplyDelete
  6. Marekani na Ulaya ni vitu viwili tofauti, mimi nilisemea kama kwa mwanamuziki wa kike wa bongo fleva ambaye amewahi kukaribishwa Ulaya kimuziki, na mtu ukikaribishwa huku Ulaya inabidi uwe na mvuto ambao watu wengi wanakukubali na ni Shilole peke yake ndiye mwenye sifa hizo na ndiyo maana amekaribishwa nchi nyingi za hapa Ulaya

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad