Sifanyi Muziki Kwa Ajili ya Tuzo-Nay wa Mitego

Msanii wa muziki wa bongo fleva Nay wa Mitego ambaye alisumbua sana na wimbo wake 'Shika adabu yako' ambao ulifungiwa na Baraza la Sanaa (BASATA)

na sasa ameachia wimbo wake mpya 'Saka hela' amefunguka na kusema kuwa yeye hafanyi muziki ili kupata au kushinda tuzo..

Nay wa Mitego aliyasema haya alipokuwa akihojiwa kwenye kipindi cha eNEWS na kuwataka mashabiki wa muziki wake watambue kuwa yeye hafanyi muziki ili kupata tuzo au kushinda tuzo bali yeye anafanya muziki kutoa burudani, kurekebisha sehemu anapoona si sawa pamoja na kumuingizia kipato ndiyo maana siku zote huwa anajiita mwanamuziki mfanyabiashara.
"Mimi siku zote sifanyi muziki ili nipate tuzo au nishinde tuzo hata mashabiki zangu naomba mtambue kuwa mimi sifanyi muziki kwa ajili ya tuzo" alisema Nay wa Mitego.

Katika hatua nyingine Nay wa Mitego anadai kuwa anapotoa ngoma zake za kuchana watu au kurekebisha baadhi ya mambo kwa watu au jamii huwa zinapokelewa vizuri zaidi na kuleta changamoto kwenye muziki ikiwa pamoja na kuchangamsha muziki wa bongo.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kweli kajisemea jay dee kichaa huwa haponi kwa hiyo unarukaruka tu kama chura wa snura huna malengo,. unawasindikiza domo na kiba katika game,. kama biashara si uuze nyanya kuliko kutoa minyimbo isiyo na meseji yoyote mpaka unashindwa kulipa madeni madogomadogo ya kina gigi.! kweli ushamba mzigo!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad