Suala la Yanga na Ndanda Kuchezea Uwanja wa Taifa, Simba yasema ni Rushwa


Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Jerry Muro amesema, Ndanda FC itakapoutumia Uwanja wa Taifa itamaanisha kwamba Ndanda FC watakuwa nyumbani na hata mapato katika mgao asilimia kubwa ataipata Ndanda hivyo haoni sababu ya wengine kuanza kuongea kwa kuona ni makosa katika mchezo huo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Klabu ya Simba Zacharia Hans Pope amesema, mchezo huo ni sio halali kwani inaonekana ni rushwa ya waziwazi kwa timu hizo, kwani haiwezekani umfadhili mpinzani wako ambaye unashindana na ukategemea matokeo ya halali.
Yanga ambayo ndio bingwa wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara msimu wa 2015/16 wakiwa wamesalia mechi mbili mkononi itakutana na Ndanda F Jumamosi Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo mara baada ya kukamilika kwa mchezo huo, Yanga watakabidhiwa Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Tags

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Viongozi wa simba acheni kutafuta sababu na visingizio kila kukicha.Julio kawapeni vidonge vyenu,au na yeye kapewa rushwa?Kwa akili ya harakaharaka unadhani TFF wangebariki hayo bila kujua sheria?basi sawa tufanye yanga wamepoteza point 3 kwa kufanya hivyo(kuwalubuni ndanda)ndio tutapanda kufikia nafasi ya 2?adhabu za kufungia wachezaji si nyie ndio mlitangaza?na bado mchezaji anaomba msamaha hamuelewi.Mna
    kurupuka kwenye kutoa maamuzi,sasa yanga wanatumia huo mwanya kutengeneza kwao.mnakumbuka kwa tambwe?halafu bila haya sasa hivi mnamtamani tena,tatizo viongozi wetu mnaongea sana na ushabiki wa jikoni,au mnakumbuka wakati Niyonzima ana mgogoro na yanga?bado alikuwa mwajiriwa wa yanga lakini baadhi yenu mliingilia ule mgogoro tena wengine kwa kutamka kabisa,ni bahati nzuri Niyonzima aliomba msamaha na anafanya kazi vizuri.Wapisheni wengine waongoze vinginevyo kila mwaka simba itakuwa hivyohivyo,sijui mjirekabishe labda,lakini sidhani.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wanatukera sanasana,walituahidi mwaka huu SIMBA ushindi ni lazima,sasa sijui walitumia kigezo gani na sasa wanatoa sababu zisizo na msingi.Wanapoteza muda mwingi kutaka kuharibu kwa YANGA kuliko kutengeneza SIMBA.Kiongozi na akili yako unatumia muda kushawishi mashabiki kuwashangilia waarabu ili iweje,au itakusaidia nini?Kwa uongozi huu unatufanya wengine tukae kando,uongozi gani kila mtu kawa msemaji wa club.

      Delete
    2. Mdau umenena vyema kwamba simba wanatumia nguvu nyingi kuwaharibia yanga wakati kwao kunamung'unyika,mfano hili la ndanda kwa nini simba wamekuwa wasemaji wakuu kuliko ndanda wenyewe?daah!wako radhi kupoteza pesa kuharibu kwa yanga, walijitahidi kununua jezi za waarabu ili tu kuwaumiza yanga,malipo yake ndio hayo.Wakati wanayanga wanawapongeza azam kwa kuwafunga tunisia wakasema yanga wanajikomba kwa azam,

      Delete
  2. VIONGOZI WA SIMBA ACHIENI NGAZI,MMESHINDWA.

    ReplyDelete
  3. Kama ni rushwa hata simba kuna rushwa,na Kama tunataka mafanikio kwenye soka letu basi tusimamie ukweli.Tujiulize kwamba
    uongozi wa Simba walitumia kigezo gani kumuajiri Mayanja,maana mimi naona ilikuwa ni zima moto,kocha kafukuzwa huku kwa kutofanya vyema wewe unamuona anafaa kwa nini?alitaka pesa kidogo au?wanasema bure aghali.Hivi mchezaji wa kimataifa kama Nimuboma unamsajili kwa pesa ndogo vile hujiulizi?Simba kumejaa mkanyagano,tujipange!

    ReplyDelete
  4. wamatopeni mapovu yanawatoka!

    ReplyDelete
  5. Simba wamesahau walivyomchezesha Ajib wakati ana kadi tatu za njano msimu uliopita kwa kusaidiwa na hiyo TFF kwamba eti mchezaji amechagua mechi za kutocheza?Leo wanaona wenzao wamenonga wakati wao walisha nonga kitambo tuu,kwanza mchezo wenyewe ni wa kukamilisha ratiba hauna umuhimu wowote kwa timu zote mbili.Yaani kwako kunateketea unashobokea ya jirani zako.
    Nyie akina Hans Pope njooni msherehekee ubingwa hapo Uwanja wa Taifa jumamosi,hata msipokuja wanenu watawasimulia!

    ReplyDelete
  6. YANGA WALIJIPANGA,MWENYEKITI WAO SIO MAGUMASHI,ANGALIA UBINGWA MARA 2 MFULULIZO SIO MCHEZO.

    ReplyDelete
  7. Kudadadeki!mlipika majungu kwa rage tukaamini mna nia ya kurekebisha kumbe lengo ni chuki tu,na kwa uongozi huu mwakani ni mwendo wa kushuka daraja na laana yenu,mtamkumbuka hadi wambura.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad