SUKARI Tani 133 za Sukari iliyoingizwa Kimagendo Yagawiwa Bure

Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imegawa Sukari yote ya Magendo Mifuko 5,319 yenye thamani ya Zaidi ya Shilingi Milioni 373.5 kwa Taasisi mbali mbali Mkoani Lindi baada ya kuthibitishwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA kuwa ni Salama kwa matumizi.

Sukari hiyo ilikamatwa mwezi Februari mwaka huu katika bandari ya Lindi ndani ya meli ya MV Hassanat ikiingizwa kinyume cha Sheria ikitokea nchini Brazil kupitia Zanzibar.

Sukari hiyo ilipaswa kulipiwa Kodi zaidi ya shilingi Milioni 246.

Sukari hiyo imegawiwa kwa taasisi 31 mkoani humo baada ya TFDA kuthibitisha kuwa sukari iko salama kwa matumizi ya binadamu.

Akizungumza wakati wa ugawaji wa sukari hiyo Mkurugenzi wa huduma na Elimu kwa mlipakodi TRA Richard Kayombo amesema baada ya kukamatwa kwa bidhaa hizo TRA kwa kushirikiana na taasisi nyingine za serikali ikiwemo ofisi ya mkuu wa mkoa wa Lindi, iliamriwa sukari hiyo kuigawa kwa watu wenye uhitaji katika mkoa huo zikiwemo taasisi za elimu, Afya, kambi za wazee na Jeshi la magereza.

Chanzo: TBC
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Yaleeee mambo ya wahujumu uchumi yanajirudia na jambo la kushangaza uchumi unao hujumiwa upo pale pale.

    ReplyDelete
  2. hiyo ni dhuluma kwa mfanyabiashara wala hatuwasifii waonevu tu na mnaenda kuua uchumi wa nchi na mabavu yenu maisha yamekuwa magumu

    ReplyDelete
  3. Tena. Iwe kwa ufariliaji Na uadilifu...manake isije ukileta ulaji. Na. Ubadhirifu WA kirahisi... Hapa Ni kazi Tu Na ukweli katika matendo...

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad