Tahadhari Kuhusu Makachero FEKI Wa TAKUKURU Wanaojifanya Kufuatilia Sakata la Sukari

Tangu kuanza kwa zoezi la kufuatilia wafanyabiashara wanaoficha sukari kwa agizo la Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mh. Dr John Pombe Magufuli, kumekuwa na wimbi la watu wanaojiita “makachero wa TAKUKURU  kutoka Makao Makuu” nao wakifuatilia sakata la sukari mkoani Kilimanjaro.

Matapeli  hao ambao kwa sasa wapo  wilayani  SIHA, wamekuwa wakiwasumbua   wafanya biashara kwa kudai kuwa  wametumwa kuwashughulikia huku wakiomba kupewa  fedha ili wawasafishe.

Kiasi cha fedha ambacho kimekuwa kikiombwa ni kati ya Shilingi 150,000/= hadi 500,000/= kama “gharama ya kuwasafisha kwa Mheshimiwa Rais”

Naomba  wafanya baiashara  Mkoani Kilimanjaro waelewe kwamba, TAKUKURU inao mfumo wa utendaji kazi ambao unajali misingi ya utawala bora na kamwe haihusiki na utapeli wa aina hii.

TAKUKURU katika utendaji wake wa kazi, haiwatozi wafanya biashara fedha kama adhabu kwa kuhifadhi sukari kinyume na taratibu. TAKUKURU  inafuatilia, kuhoji na kumtaka mfanyabiashara kuonesha namna  anavyomiliki sukari hiyo kwa kutoa vielelezo husika. Mwisho wa zoezi hili, atakayetoa tamko ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Ifahamike kuwa hakuna afisa wa TAKUKURU mpaka sasa aliyetumwa kutoka Makao Makuu kuja mkoani Kilimanjaro kufuatilia zoezi la sukari. Zoezi hili mkoani hapa linaendeshwa na vyombo vya ulinzi na usalama kama timu moja na wala halifanywi na TAKUKURU pekee .

Ifahamike pia kuwa hakuna zoezi linaloihusisha TAKUKURU litakaloendeshwa mkoani bila ofisi ya mkoa kuwa na taarifa.

Kwa misingi hiyo yeyote anayeendesha zoezi hilo nje ya utaratibu nilioufafanua ni tapeli, taarifa zake zitolewe mapema ili akamatwe na kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

Maofisa wote kutoka ofisi ya TAKUKURU mkoa wanavyo vitambulisho na kama watatiliwa shaka basi ofisi yangu ijulishwe kupitia simu namba   0784 998 804 au 0786 089 805 muda wowote.                                                              
                             
IMETOLEWA NA                                                                  
ALEX J KUHANDA
MKUU WA TAKUKURU  MKOA WA KILIMANJARO
11/5/2106.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hili suala ni so sensitive lakini Ndugu Mwandishi wa Habari huliweki hadharani. Je ni kwa miaka mingapi sisi ambao ni Watanzania tumekuwa Tukilishwa Sumu????????? Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda ametoka kuyakamata Makontena 1115 yenye Sukari inayosemekana imeagizwa kutoka Nchi za Nje. Kwa mujibu wa taarifa za waliyoikamata ni kuwa hii Sukari iliagizwa kutoka Nchini Brazil na kupelekwa Nchini Dubai kwa ajili ya kupakiwa kwenye mifuko amabayo hatujui kama ni kweli huo ndio utaratibu ama la. Je ukiagiza Sukari kutoka Nchini Brazil ni kwa nini ipitie Dubai????? Tena kwa ajili ya kupakiwa kwenye mifuko mingine?????? Kwani Nchi ya Brazil huwa hawahusiki na upakiaji wa Sukari kwenye mifuko inayotakiwa na kuisafirisha moja kwa moja kwenye Nchi husika????? Nadhani hapa Ndugu zangu Watanzania inabidi tujiulize hili swali la kuwa tumekuwa tukilishwa Sumu tangu lini???????? Halafu kitu kingine cha ajabu na kulingana na taarifa za wakamataji wa hayo Makontena yaliyosheheni hiyo Sukari ni kuwa baadhi ya mifuko ni ya Kiwanda cha Sukari cha Kilombero. Sasa hii ina maana gani, ni kuwa hawa ambao ni Wafanya biashara wa Sukari wamekuwa wakinunua ama kutumia ile mifuko iliyotumika ya Sukari kutoka Kiwanda cha Sukari ya Kilombero na kuitumia kupakia hiyo Sukari kutoka huko Brazil ili kuficha uhalali wa kama ni kweli hiyo Sukari ni nzuri kwa matumizi ya binadamu. Sasa tunarudi kulekule na kubakia midomo wazi tukijiuliza ya kuwa tumekuwa tukilishwa hii Sumu kwa muda gani?????? Na je hizi athari za kuitumia hii Sukari iliyokwisha muda wa matumizi yake ni nani atazigharamia??????? Jamani Watanzania wenzangu tufunguke macho na kujiuliza hili swali huku tukitafuta ukweli wa jibu lake. Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda ni kuwa hii Sukari iliyokamatwa pale Bandarini haijulikani ni ya nani. Je huu mchezo wa kutudanganya kila siku utaisha lini?????? Haiwezekaniki Bandari ikawa inapokea mizigo ambayo haijulikani muagizaji ni nani. Huu ni uongo na utapeli wa hali ya juu sana. Ama ni katika kutufanya sisi Watanzania ni magoigoi hatujui lolote ama hatuwezi kufikiri na kuhoji baadhi ya vitu ambavyo ni so sensitive katika maisha yetu. Kwa utaratibu wa Import and Exportation ama Clearing and Forwarding haiwezekani wahusika wa bidhaa ama mali hizo wasijulikane, hicho ni kitu ambacho hakiwezekani. Kwa sababu nyaraka zote muhimu za kusafirisha hiyo mizigo ni lazima zitakuwa na vielelezo muhimu vya wasafirishaji na wapokeaji mizigo. Sasa hilo suala la kutuambia eti ya kuwa waagizaji wa hayo Makontena 1115 yenye Sukari kuwa hawajulikani huo ni uongo na utapeli mkubwa amabao hauwezi kuvumiliwa na Watanzania kwa ujumla na hasa wale wanaoitakia Nchi yao Neema.............Kwa kweli Huu Mchezo Hautaki Hasira lakini kwa Mantiki hii Inatia Hasira tena sana tuuu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad