Tisa Mbaroni kwa Kuuza Sukari Kinyume cha Bei Elekezi

Polisi mkoani Arusha inawashikilia watu tisa kwa kosa la kuuza sukari tofauti na bei elekezi ya Sh1,800.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amesema leo kuwa watu hao wamekamatwa kwa nyakati tofauti na watashtakiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi.

Mkumbo alisema mmoja wa watu hao amekutwa akiuza kwa Sh5,000 kwa kilo moja.

Alisema wengine walikamatwa wakiuza sukari Sh6,200; Sh3,000; Sh2,500  na Sh4,500 kwa kilo.

Kamanda Mkumbo amesema kamatakamata ya watu wa aina hiyo ni endelevu na aliwashauri wafanyabiashara wote mkoani Arusha kuuza sukari kwa bei elekezi iliyopangwa na Serikali.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hongereni sana ,mkuu wa police wa Mkoa wa Arusha wa askari police wa Mkoa wa Arusha kwa kazi wanayofanya ya kukamata wafanyabiashara wanao kiuka angizo la Mheshimiwa Rais wetu Magufuri la bei ya sukari,Naombeni wakuu wote wa police wa Mikoa na Wilaya zingine waige mfano wa Mkoa wa Arusha.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad