TRA imetoa wapi mamlaka ya kugawa Sukari bure?

Nimesikia taarifa ya habari kuwa,Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imegawa Sukari yote ya Magendo Mifuko 5,319 yenye thamani ya Zaidi ya Shilingi Milioni 373.5 kwa Taasisi mbali mbali Mkoani Lindi

Sakata la hii sukari lilianza Febuary mwaka huu,unaweza ukajiuliza
Tangu Februari hadi leo nini kilikuwa kinasubiriwa?

Je lini TRA imeanza kugawa BURE vitu vinavyodaiwa kodi?kwa hiyo kesho wakikamata gari ambazo hazijalipiwa ushuru watazigawa bure?

Je, wakikamata mafuta yatagaiwa bure?Haya yanayotokea ni madhara ya nchi kutokuwa na DIRA.

Tunakumbuka miezi miwili nyuma wimbo wa viongozi wote wa serikali kuanzia Dc,RCs,na wakuu wa idara zote za umma ulikuwa ni watumishi HEWA!

Suala la watumishi Hewa halijaisha limekuja suala la sukari sasa hadi TRA ambao sheria inawataka wakusanye kodi,ni mamlaka ya kukusanya kodi,wala sio kutoa vitu ambavyo havijalipiwa ushuru!

Kimsingi hii ni ishara na kielelezo cha Ombwe la uongozi,pamoja na ukosefu wa DIRA

Bila MAONO Taifa huangamia
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Udaku Hilo swali Ni zuri..Jibu Ni Rahisi kabisa wewe si unalijua!! Ni like like Na ikibidi tunaweza kuanzisha emergency sabotage tribunals on presidential capacity.. Nyamaza Hilo Ni soma kwa wwngine..Bidha hii Ni consumable Na has life time..tumezingatia vyote. Ukusanyaji Na ulipaji kodi Ni jukumu la kila muhusika Na hizo harakati..ACACIA PIA BADO TUKONAO NA MALIPO YATAONGEZEKA...WW LEAVE NO STONE 💎 UNTURNED..ITS A MATTER OF TIME AND ITS SOON..HII NI WAMU YETU NA AMINI TUNAWAJIBIKA..KAA PEMBENI UANGALIE.. NA MANENO YA UPOTOSHAJI HATUYATAKI..DIRA KUKOSENA UNA MAABA TUKO AUTOPILOT? TUNAENDA KIHOLELA??

    ReplyDelete
  2. hana jipya huyo anyamaze aache wanaume wafanye kazi ya kuwaletea maendeleo wananchi

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad