Tuhuma Nzito Bungeni..Baadhi ya Wabunge Wadaiwa Kuvuta Bangi na Kutumia Madawa ya Kulevya

Tukio la Zamani Bungeni
Mbunge wa Viti Maalum, Mariam Msabaha (Chadema) ametoa tuhuma nzito kuwa ndani ya Bunge kuna wabunge vijana wanaovuta bangi na kutumia dawa za kulevya.

Mbunge huyo amemuomba Rais John Magufuli kuagiza wabunge wa aina hiyo ambao hata hivyo hakuwataja wapelekwe Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ili kufundishwa nidhamu.

Msabaha ametoa kauli hiyo Bungeni mjini Dodoma wakati akichangia hotuba ya bajeti ya wizara ya Ulinzi na JKT iliyowasilishwa na Waziri mwenye dhamana na Wizara hiyo, Dk Hussein Mwinyi.

“Wabunge nao waende JKT kwa sababu hili Bunge wameingia vijana wengine ambao ni mateja wa unga na wengine wanavuta bangi. Wengine wanawavua mama zao nguo,” amesema Msabaha.

“Wengine mama zao wameshakufa wanakuja humu wanawatukana mpaka wazazi wao. Kwa hiyo niombe Rais Magufuli vijana wote wabunge ambao hawana nidhamu waende JKT,” alisisitiza.

Mbunge huyo amesema wabunge wa aina hiyo hawana viwango vya kuzungumza ndani ya chombo hicho cha kutunga sheria hivyo ni vyema waende JKT ili wakirudi wawe wamejua namna ya kuchangia.

Ingawa hakumtaja Mbunge yeyote, lakini mchango  ulioibua mtafaruku bungeni ni wa Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga aliyedai wabunge wa viti maalumu Chadema huitwa Baby ili kupewa nafasi hiyo.

Tafsiri ya kauli hiyo ni kuwa wabunge wa viti maalum Chadema lazima wafanye mapenzi au kuwa na mahusiano na viongozi wa juu wenye mamlaka ndani ya chama hicho ndipo wateuliwe kuwa wabunge.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Duh!Kwa mipigo hiyo safari yaani bado ndefu sana kufikia pale ambapo watanzania wengi wanaota usiku na mchana waifikie hiyo hatua maana bangi+madawa ya kulevya bungeni ni=na sifuri(kalaga bao walisema wazaramo)

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tunahitaji mahudhurio ya Mwili Na Akili..kazi tunayo Na kuelisha Ni wajibu..wengi Wao hajielewi Na poshho wanayo inawapa time katika Holidei...Wapi ? Dodoma nyama choma..Azzan/ Ndugai / Kassim...huu ndio ukweli halisi tuushughulikie Na tunyooshe asiye weza arudi jimboni kwake kujieleza kuwa Dhamana mliyipa ilikuwa juu ya uwezo wangu Samahani kwa kuwaangusheni..HAPO TUTAWAELEWA..SI AIBU NI UKWELLI..NA MSEMA KWELI NI MPENZI WA MUNGU..NA TUTAMWELEWA KUWA MZALENDO ALIE ACHIA KAMBA NA MTAKA MAENDELLEO YA NCHI AWAACHIE WENYE KUWEZA NA SIYO TAMAA TU..ENDELEA BABA HAPA KAZI TUU

      Delete
  2. Inatishaaaa..... Watunga Sheria ni wavunja sheria...Pungwe kaingia Bungeni..Matokeo ni sawa na hakuwapo wala hatakuwepo.....ZER000000. JPJM anakazi kubwa kwa Waheshimiwa asipo idhinisha / kuwapa !20Mil toka 90Mil.. itabidi waanze Madudu ambayo hatuyataki... Bunge lina Heshima yake.. Asiyejiheshimu hatopewa heshima kama Muheshimiwa... Waheshimiwa kuweni na Nidhamu na Uzalendo muliokoe hili Taifa.. Mlete MAENDELEO... SIASA KWENYE KAMPENI

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad