DHANA ya utumbuaji majipu sasa imemgeukia Rais John Magufuli kutokana na kuongoza wizara iliyotawala na ubadhirifu wa fedha za umma, anaandika Regina Mkonde .
Katika Serikali ya Awamu ya Nne chini ya Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, Dk. Magufili alikuwa Waziri wa Ujenzi – wizara ambayo inatajwa kujaa ubadhirifu wa pesa za umma na kwamba, rais huyo ameshindwa kuchukua hatua.
Kutokana na hali hiyo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imemtaka Rais Magufuli kutumbua majipu yake wake wakati akiwa kwenye wizara hiyo.
James Mbatia, Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano amesema, katika wizara hiyo kuna ubadhilifu wa fedha za umma.
Pia kumekuwepo na utendaji mbovu wa watumishi na kwamba, serikali haina mpango wa kuwachukulia hatua za kisheria wahusika kutokana na kutoonesha jitihada.
“Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inajiuliza kama serikali ya awamu ya tano inafanya kazi yake kwa haki, uadilifu, uwazi na usawa kwa wote na hasa kwa kile kinachojulikana kama utumbuaji majipu, swali hapa ni nani amfunge paka kengele? au mkuki mtamu kwa nguruwe mchungu kwa binadamu?” amehoji Mbatia.
Wakati akitoa hotuba ya maoni ya kambi ya upinzani leo Bungeni mjini Dodoma kuhusu mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017 Mbatia amefafanua baadhi ya dosari zilizofanywa na wizara hiyo.
Moja kati ya dosari hizo ni kitendo cha Wakala wa Barabara nchini TANROADS cha kuitia hasara zaidi ya Sh. 5 bilioni serikali.
“TANROADS imebainika kuwa na utendaji mbovu kama ambavyo mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) alivyobaini juu ya usimamizi mbovu katika mikataba ya ujenzi wa barabaa na madaraja ambapo ilikuwa chini ya iliyokuwa wizara ya ujenzi katika serikali ya awamu ya nne,” amesema.
Mbatia ameongeza kuwa “TANROADS wakati wa kipindi hicho, iliitia hasara serikali ya jumla ya Shilingi 5,616,652,051 kutoka kwenye riba (interest) inayoongezeka kila siku kutokana na TANROADS kuchelewa kuwalipa wakandarasi 11.”
Amesema kuwa, hasara hiyo iligundulika kati ya kipindi cha mwaka 2012 na mwaka 2015 kwa mujibu wa Ripoti ya CAG ya Hesabu za Serikali Kuu wakati wa ukaguzi wa taarifa za fedha kwa mwaka ulioishia tarehe 30 Juni 2015 iliyotolewa mwezi Machi 2016 (Ukurasa wa 134 na 135).
Dosari nyingine ni ile ya serikali kuruhusu matumizi ya matairi yanayofahamika kwa jina la Super single tires ambayo yanaharibu barabara.
“Utafiti unaonesha matairi haya (super single tyres) yanaharibu barabara. Matairi haya yameanza kutumika takribani miaka mitano iliyopita na mzigo uliokuwa unabebwa na matairi 24 sasa unabebwa na matairi 12,” amesema.
Mbatia amesema, uruhusiwaji wa matumizi ya matairi hayo haukuwa wa busara kutokana na kwamba matokeo yake ni uharibifu mkubwa wa barabara.
“Uamuzi wa kuruhusu matairi haya haukuwa na busara maana barabara zetu hazijabuniwa kuhimili shinikizo la uzito (excessive pressure) linalotokana na matairi hayo,” amesema.
Ameitaka serikali kuzuia mara moja matumizi ya matairi hayo ili kuzinusuru barabara lakini pia kuokoa fedha za walipa kodi zinazotumika kurekebisha mara kwa mara barabara hizo na kunyima fursa maeneo mengine kupata barabara za kiwango cha lami.
Akizungumzia uuzwaji wa nyumba za serikali Mbatia amesema, serikali iliuza nyumba zake kwa bei ya hasara hivyo kuigharimu nchi.
“Katika muktadha huo kambi Rasmi ya Upinzani inalikumbusha Bunge kwamba, kati ya mwaka 2002 mpaka 2004 Serikali iliuza nyumba zipatazo 7,921 na mpaka mwaka 2008 Serikali ilikuwa imejenga nyumba 650 tu,” amesema.
Amesema kuwa, katika biashara ya kuuza nyumba zilizokuwa mali ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), serikali ilipata Sh. 252,603,000/-
ambazo haziendani na thamani halisi ya nyumba hizo.
“Hivi sasa serikali inahitaji kusaka nyumba zaidi ya mara dufu ya kiasi hicho kujenga nyumba za fidia.
Kwa mujibu wa taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge juu ya uuzaji wa nyumba za serikali kinyume cha taratibu, serikali itatumia Sh. 677,606,000/- kujenga nyumba mpya ili zirejeshwe kwa Tamisemi, Rejea taarifa ya Serikali Bungeni tarehe 25 April 2008,” amesema.
Mbatia amesema, waliouziwa nyumba hizo, kuna taarifa kuwa kati yao wapo walioziuza na kujipatia faida kubwa kinyume na mikataba ya mauzo hayo,na kwamba KRUB inapendekeza wanyang’anywe nyumba hizo kwa kukiuka mikataba na malengo ya mauzo.
“Kumbukumbu za taarifa rasmi za Bunge zinaonesha kwamba, serikali ilitoa taarifa ndani ya Bunge hili kuwa, kuna kamati iliundwa kuchunguza mchakato wa mauzo ya nyumba ya serikali.
“Kamati hiyo ilitegemewa kumaliza kazi mwezi Februari, 2007, lakini hadi Bunge la Tisa na Bunge la Kumi linamaliza uhai wake hakuna taarifa iliyotolewa na serikali. Kambi Rasmi ya Upinzani Buneni inaitaka serikali ya awamu ya tano irejeshe nyumba hizo,” amesema.
Mbatia amesema, kuna maadhimio kadhaa yaliyoadhimiwa na bunge ikiwemo kuitaka serikali kurejesha nyumba zilizouzwa kinyume cha taratibu na kwa watu ambao hawakuwa watumishi wa umma.
“Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeiitaka Serikali kutekeleza azimio hilo la Bunge, na kwa njia hiyo ile kauli mbiu ya hapa kazi tu, iweze kutafsiriwa kwa vitendo,” amesema na kongeza;
“Tunajua uuzwaji huo ulisimamiwa na Wizara aliyokuwa akiiongoza yeye na kuna uwezekano mkubwa kwamba alisimamia maamuzi ambayo hakuwa na uwezo wa kuyakiuka.”
Amesema, sasa ni muda sahihi Rais Magufuli kurekebisha kasoro alizozisimamia na katika mchakato huo ili kurejesha imani katika jamii.
“Tukumbuke kuwa Rais Kikwete alielekeza nyumba hizo zirudishwe serikalini lakini alikosa uthubutu wa kusimamia kauli yake,” amesema.
Aaaaa nyinyi bana munatafut tuu njia yoyote ya kumchafua rais na kumkata nguvu ila hamutawez kwan tayar kashind uchaguz ujao wa 2020. Sasa bakien kuzungumz tu wakat yey anakwendelea kujiongezea umaarufu inchi na duniani kote. Wapinzan hawan lolote yaani wamezimwa vibay mno wenyew hawajitambui yaani wame panik kwan zil kelel na tuhuma mbalimbali hakun hawajui watamuanzia wapi kwan kila sehem amewazim. Sasa upinzan utakuw na kaulimbio gani 2020? hakun kwan rais kawagus wengi. Et atumbue kweny wizara yake ya zamani!! ahahahaha nachek sio wazir ten hiv ni rais na njomaan anafany mambo ambayo ulimweng unasifia na weng wanaiga. Muulizeni mambo ya sasa sio wakat alikua wazir achen ujinga na mada isio na tija.
ReplyDeleteJPM TUMBUAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA
ReplyDeleteLISU NA LEMA MTABAKI KUPANIKI SIKU ZOTE
MIMI KAMA MIMI SIIPENDI CCM LKN NAMPENDA JPM NA NINAIMANI ATATUFIKISHA KWENYE MAENDELEO YA KWELI ...NA HAO WANAO SEMEA CHINI CHINI WALIKUWA WANANUFAIKA NA UFISADI KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE..SASA WANATAMANI KUMWAMBIA MZEE JPM BASI WACHIA NAFASI UFISADI TUENDELEE KUIFISADI NCHI WANASHINDWA-NA NDIO MAANA WANATAPA TAPA KILA KUKICHA..WASHINDWE NA WALEGEE-AAAAAAAAAAAMIIIIIIIIIIIIIIIIIIIINA...MAGUFULI OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE
ReplyDeleteWapinzani na Wenye maono mazuri walisema Rudisha katiba. Kutokana na Katiba kungekuwa na ufuatiliaji wenye usawa na unaolindwa kisheria. Ndugu Kikwete hakuweza tumbua sababu kuna migogoro inamhusu yeye direct. Hangeweza kujitumbua. JMP ameanza kazi vizuri, Alichosahau ni kweka sheria wazi, sawa, yenye maadili. Hiyo itaweza kufanikisha tumbua sababu watu wote wenye makosa sheria ingecheza sawa, Tatizo la kuchomoka na kutumbua kiholela. Wengine wanatumbuliwa bila kupewa chansi ya kujitetea. Wengine wanaundiwa tume an\mbazo hazina ubavu wowote. Wengine hawataguswa kabisa na wameifilisi nchi. Hawa wanakwepa lakini wakionekan kumsapoti ili wasitumbuliwe. Mshauri safi wa JMP inabidi alitazame kwa ukaribu jambo hili kusudi wahusika vigogo waweze ktumbuliwa pia.Ni hapa Magufuli atashindwa kuyatumbua majipu makuu. Lakini kasema atatumbia yote.
ReplyDeleteTumsubiri tuone.