Utumbuaji Majipu Siyo Ukatili- Rais Dkt. Magufuli Afunguka Kanisani

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amesema hatua anazochukua kwa ajili ya kuwasimamisha watumishi wa umma kazi zisitafsiriwe kama ni ukatili kwakuwa watumishi hao wamekuwa wakifanya mambo kinyume na maadili ya utumishi wa umma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 08 Mei, 2016 ameungana na waumini wa Parokia ya Toleo la Bwana iliyopo katika Jimbo Katoliki la Arusha kusali ibada ya Jumapili, ambapo katika salamu zake amewaomba watanzania kuendelea kuiombea nchi yao ili kazi anayoifanya ya kukabiliana na matatizo yanayowakabili watanzania wanyonge ifanyike kwa mafanikio.
Dkt. Magufuli amesema hayo alipokaribishwa na Mwenyekiti wa Parokia hiyo Bw. Philemon Mushi kuwasalimu waumini wa kanisa hilo, mara baada ya kumalizika kwa ibada ya Jumapili ya kupaa kwa Bwana.

"Niko pamoja na nyinyi ndugu zangu watanzania na wana Arusha wote, napenda kuwaahidi tena sitawaangusha, nitasimama mbele kuwatetea masikini, siku zote nitakuwa upande wenu, siku zote nitatembea na nyinyi, nasema kwa dhati kabisa na nataka muamini hilo kwamba sitawaangusha" amesema Rais Magufuli huku akishangiliwa na waumini walioshiriki ibada hiyo.
Rais Magufuli amewahakikishia watanzania wote kuwa atahakikisha ahadi zote alizoziahidi anazitekeleza na amewaomba watanzania wote kuungana na kushikamana ili kufanikisha juhudi za kuijenga Tanzania bora.

"Ninajua kuongoza ni kazi kubwa, ninajua kuongoza Taifa lililo masikini kama Tanzania inahitaji mkono wa Mungu, kwa hiyo niwaombe sana ndugu zangu Wakristo na watanzania kwa ujumla, muendelee kuliombea Taifa hili, kuniombea mimi, na pia kujiombea sisi wote ili amani tuliyonayo katika nchi yetu iendelee kudumu katika maisha yote.

"lakini siku zote katika matendo yetu kila tunapofanya tumtangulize Mungu kwa sababu Mungu ndio kila kitu, lakini tutambue kwamba siku moja tutakufa, kwa hiyo ni vyema katika matendo yetu tutakapokuwa hapa duniani tujitahidi sana kufanya matendo mazuri kwa ajili ya watu na hasa watu wanyonge, ambao kwa kweli watanzania waliowanyonge wanapata shida sana" Amebainisha Rais Magufuli.

Pia Dkt. Magufuli amewasihi watanzania wote kuachana na ushabiki wa vyama vya siasa na badala yake waungane katika ujenzi wa Taifa na kukabiliana na kero zinazowaumiza

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. JPJM..Ni Sawa yote na nasema kuwa Waumimi Wa DINI ZOTE WANAKUOMBE NA KUIOMBEA NCHI YETU AMANI UTULIVU NA MAENDELEO..WAZEMBE NA WATOVU WA NIDHAMU NA MAADILI...HATUWATAKI KTK NYASHIFA NA MADARAKA IKIEA WATASHINDWA KUWAJIBIKA IPASAVYO.. ENDELEA BABA..WAUMINI WA DINI ZOTE TUOMBE AFYA NA UMURI TAWILE EA MCHAPA KAZI WETU JPJM..

    ReplyDelete
  2. Mungu atakulinda kwa mabawa yake mwenyewe. Mungu azidikukuongoza kila siku katika maisha yako ya kusaidia wanyonge. Mungu mbariki rasi Magufuli, Mungu ibariki Tanzania na Afrika. Kutoka USA.

    ReplyDelete
  3. Mheshimiwa Rais,Amiri jeshi mkuu wa Tanzania Ndugu J Magufuli,1 Nakupongeza kwa kupata URAIS 2 Nakupongeza kwa kazi kubwa unayoifanya ya utumbuaji wa MAJIPU madogo na MAJIPU sugu,3 Katika kipindi ulichofanya kazi ,kazi yako imeonekana kwa Taifa na ulimwengu wote wanakusifu kwa kazi nzuri ,4 Umeifanya TANZANIA imekuwa mfano wa kuingwa na Nchi jirani 5 Mheshimiwa Ris sio watu wote wanakupenda,maadui ulionao ni wengi MUNGU nakuomba umzidishie ulinza Rais wetu,nakufunika kwa damu ya YESU ,damu ya yesu iketangirie kila uendapo,

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad