Vijana Wanaovaa Suruali Chini ya Kiuno Kuchapwa Viboko 70


Wakazi wa Kata ya Karansi, Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro wametoa uamuzi kuwa wanawake watakaovaa sketi fupi na vijana watakaovalia suruali chini ya kiuno, wataadhibiwa kwa kuchapwa viboko 60 hadi 70.

 

Uamuzi huo umefikiwa na wakazi zaidi ya 200 wakisema uvaaji huo ni kinyume na mila na desturi za Kiafrika.
 

Vazi lingine lisilotakiwa kwa wanawake ni kuvaa suruali pamoja na vijana kunyoa ndevu mitindo isiyofaa.
 

Mkutano huo ulioandaliwa na wazee wa kimila jamii ya Meru (Wachili) na Wamasai (Malaigwani), uliwavutia wananchi wengi ambao walihudhuria.
 

Sambamba na uamuzi huo utakaokuwa unafanyika hadharani, pia adhabu hiyo itawahusu wezi wa mali na wanaopenda kucheza pool table wakati wa kazi.
 

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Wilbrod Mutafungwa alipinga uamuzi huo akisema kwa maazimio hayo ya kuwaadhibu watuhumiwa kwa kuwachapa viboko ni kujichukulia sheria mkononi na ni kinyume na sheria.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwani tunaishi kwenye karne ya ngapi mpaka watu kujichukulia uamuzi wa kuwapiga viboko vijana na wasichana wanaovaa nguo hizo zikizotajwa hapo juu hii ni dunia huru mtu huvaa au kunyoa ndevu apendavyo acheni mambo yaliyopitwa na wakati

    ReplyDelete
  2. Mngeanza na kuwachapa wabunge wanaotukana bugeniiiiiiiiiiiiiii
    FYUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUU

    ReplyDelete
  3. Labda hiyo milegezo na hizo sketi fupi, hawa vip kupinga na uvaaji wa suruali juu, mataifa mengi duniani sasa ndio limekuwa ni mmja ya mavazi kwa mwanamke, sababu 1.vazi la suruali linampa uraisi wa kutembea mwanamke, linampa kujiamni ata akikaaa chini au kunyanyuka kwamba zitaonekana nguo za ndani pili, hata kama huko kijijini wanaume wenye tabia mbaya dhidi ya wanawake inawawia ngumu kufanya uovu wao, mpka avue suruali saa ngapi? Mwanamke kesha jinasua, si sawa na gauni litanyanyuliwa tu, kuna faida nyingi za kuvaa suruali kwa mwanamke, kwanza zimetengenezwa tofauti na zile za wanaume, tusijurudishe nyuma kwa mambo ya karne hizo, za age stone age au middle stone age tuko millennium sasa dunia yote inaenda ikibadilika, mwanadam anabadilika kila wakati.nyie ndio mkipewa majiko ya gesi mtapinga tumezoea utamaduni wetu kupikia kuni na wakati sio karne yake tena, mmekata sana miti kiasi mmesababisha jangwa.mvua hakuna,hewa chafu si hamtaki kwendaa na wakati huo ni mfano tu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad