Rais John Magufuli aliwasili Uganda jana asubuhi kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule wa nchi hiyo, Yoweri Museveni zinazofanyika leo na Makamu wake, Samia Suluhu Hassan alikuwa Kigali, Rwanda kuhudhuria mkutano wa dunia wa uchumi.
Taarifa zilizopatikana na kuthibitishwa na Mwandishi wa Makamu wa Rais, Penzi Nyamngumi zimesema, Makamu wa Rais aliondoka nchini Jumanne akitokea Dodoma na angerejea kesho baada ya mkutano huo.
Kiongozi anayefuatia kwa wadhifa, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisafiri juzi kwenda London, Uingereza kumwakilisha Rais Magufuli katika mkutano wa wakuu wa nchi kujadili mapambano dhidi ya rushwa.
Majaliwa katika ziara hiyo ameongozana na Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju alipotakiwa kutoa ufafanuzi juu ya anayepaswa kukaimu urais, alisema Makamu wa Rais amekwisha rejea nchini na yuko Mwanza.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 37 (3), inaeleza kuwa endapo Rais atakuwa hayupo katika Jamhuri ya Muungano, kazi na shughuli za Rais zitatekelezwa na Makamu wa Rais, kama naye hayupo, yatatekelezwa na Waziri Mkuu.
Hata hivyo, Ibara ya 37 (6) (b) inasema Rais hatahesabiwa kwamba hayupo iwapo atakuwa nje ya Jamhuri ya Muungano kwa kipindi cha saa 24.
Kati ya Mahakama au Speeker wa Bunge. Kama kuna mwenye uhakika anisaidie hapo, Ila mmoja kati ya hawa wawili anastahili.
ReplyDeleteUnauliza swali ama unauliza jibu??? Wewe nyang'au kwelikweli. Anayeiongoza Nchi ni Babako......
ReplyDeleteUNAKICHAA WEWE MWEKE BABA YAKO AONGOZE NCHI SWAINI KAZI KUPOTOSHA
ReplyDeleteSpika WA bunge
ReplyDeleteAnayekaimu kama viongozi wakuu hawapo ni spika WA bunge
ReplyDeleteAnayekaimu kama viongozi wakuu hawapo ni spika WA bunge
ReplyDeleteNdungai ataongoza nchi.bunge lenyewe shida. Hivi uko serious.au
ReplyDeletekazi mnayo
ReplyDeleteOya Mie stelingi nipo!! Unataka nikusaidie nini?? Hivyo hatuna cha maana zaidi ya Hii...unataka ukweli Kula mmoja wetu anaongoza nchi..Wajinika ulipo..katika utendaji na izalishaji...Hapo umeongoza nchi na uwe Raia Mwema...Tummemaliza nna utakuea umemaliza...Mimi na wewe Tuna Jukumu la kumsaidia JPJM..USIKU NA MCHANA..NCHI YET NA WATU WAKE..ITANYOOKA..WE NEED AND HAVE TO BE RESPONSIBLE CITIZENS
ReplyDelete