Wabunge Waja Juu...Wadai wao Sio Wanafunzi Wakusign Kila Waingiapo Bungeni Asubuhi na Wakitoka Jioni


Wabunge wameitaka Ofisi ya Bunge iwaondolee mara moja utaratibu wa kusaini kwa kutumia vidole mara mbili kwa siku kwa kuwa wao si wanafunzi.


Hoja hiyo iliwasilishwa kwa njia ya mwongozo na kuungwa mkono na wabunge wote isipokuwa mawaziri na Mbunge wa Konde, Khatib Said Haji (CUF) mjini Dodoma jana.


Katika Mwongozo wake, mbunge huyo alisema kitendo cha kutakiwa kusaini mara mbili kwa siku ni kero kwa wabunge na uonevu kwa kuwa hata Bunge limekuwa likitumia muda wa mapumziko wa wabunge kwa kazi za Bunge.


“Mheshimiwa Naibu Spika wewe mwenyewe muda mfupi umetangaza matangazo mbalimbali yanayotaka baadhi ya wajumbe wa kamati wakutane baada ya saa saba mchana, tunafanya kazi nje ya mapumziko yetu, haya haina tatizo... “...tatizo langu ni kitendo cha wabunge kutakiwa kusaini mara mbili kwa siku asubuhi na jioni, wakati mwingine tunatoka hapa saa saba, wabunge tunashughulikia mambo mpaka saa 12, mbunge anatumia muda wake wa mapumziko na ule wa kuhudhuria kikao cha jioni,” alisema Haji.


Alisema inasikitisha kuona mbunge anatolewa kwenye kazi za kujenga taifa ili aje tu asaini kwa kidole tena mara ya pili.


Alisema jambo hilo linawatatiza wabunge kwa kuwa wanajiona kama wanachukuliwa kama wanafunzi kwa kufuatiliwa kwani hata kwenye benki wafanyakazi hawasaini na kufuatiliwa kama ilivyo kwa wabunge hao.


Alifafanua kuwa kabla ya kuomba Mwongozo huo, alifanya utafiti kwenye benki mbalimbali ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambao nao wana utaratibu kama huo wa Bunge lakini hakuna mahali wanapotakiwa kusaini kwa vidole mara mbili.


“Kutokana na uzito wa jambo hili naomba kutoa hoja wabunge mniunge mkono mpango huu ukome,” alisema na wabunge takribani wote walisimama ishara ya kumuunga mkono na kumpigia makofi na vigelegele.


Kwa upande wake, Naibu Spika, Dk Tulia Ackson alisema kutokana na namna wabunge hao walivyopokea suala hilo, pamoja na kwamba kikanuni jambo hilo halikutakiwa kuombewa mwongozo bado litaangaliwa.


“Hata hivyo, nifafanue kuwa kusaini mara mbili lengo lake si kuwafanya wabunge wanafunzi, ila lengo ni kutaka kujua nani wapo humu ndani (bungeni),” alisema Dk Ackson.
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hao wabunge wameshazoea kutoroka vikaoni.....hovyo

    ReplyDelete
  2. Hata makazini tunaweka dole mara mbili na sisi si wanafunzi ! Acheni uvivu hiyo manifest lazima khaaaa!

    ReplyDelete
  3. Bunge letu limedhihirisha. Kwa kiasi fulani utovu WA nidhamu Na majukumu...angalia hoja wanayotoa kutotaka kusaini Ni kwamba Mimi au siai siyo wanafunzi..Je hii inaingia kichwani kwa Mimi nilieluamini uende kuniwakilisha Na wewe uwe sauti yangu!!! Naomba Bunge letu liweke hii as mandatory kwa wabunge wote.. Na wabunge wawe monitored kwa behaviour zao Na hoja sisizokuwa Na kichwa wala miguu Na ubishi usio Na maana..Tunatala wabunge walio komaa kimaadili Na wenue nia Na lengo la kuoma wanajenga misingi ya maana WA Maendeleo Na kamati ya nidhamu iweze kumonitor wabunge wanaoingia katika Bunge ambao hawako katika hali ya kawaida kwa Saba u moja au nyingine..Je hawapo katika Bunge letu??? Nakuombeni muwajibike Kama tunavyo tarajia..ioneeni huruma kura yangu kukupa wewe mheshimiwa tunaomba mjiheshimu wenyewe Na kutenda qajibu wenu ikiwemo kuhudhuria kiakili Na kimqili ndani ya Bunge letu..Mh Ndungai Na Mh Majaliwa pls streamline process and norms za Bunge letu..wanaoaema si wanafu zi au walevi Tu wakatie posho ikiwa Ni adhamu ua mwanzo..na akirudia anazidishiwa muda Na ikibidi anakua hafai Na hqna sifa xa kuingoa ndani ya Bunge unamrudisha kwa wapiga kura wake Na by election inanafanywa watanyooka..tunataka wabunge WA kuleta Maendeleo Na siyo Sera za vyama...mungu libariki Bunge la MABADILIKO NA MAENDELEO ASIYE WEZA ARUDISHE HIYO HEAHIMA ALIYOPEWA MANAKE HALINGANI NAYO...HAPA NI KAZI TU. ..JPJM PLS FATILIA SAFARI INAHITAJI WATU WALIO AMUA KUSHIRIKI AAIYW WEXA MLANGO UKO WAZI

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kweli mdau..wakinda Dodoma wanajua wamekwenda Likizo toka familia zao halisi..huko Ni michepiko Na ndovu...Lazima wadhinitiwe

      Delete
    2. Mdau kweli kabisa..si umeiona ya Waitara libidi polisi wawajibike nae...

      Delete
  4. Wengine Ni basi Tu..hawana hata sifa za kuwa bungeni..serikali. Itabidi wakija kuchikua fomu WA wanafanya. Uadilifu Na kuwa mitihani ya aina tatu..moja ya uzalendo ..pili ya elimu ma tatu uhahiai ukipewa hii nafasi utaleta mabadiliko gani kwa taiga Ili ajieleze Na Kama utumbo..ananyimwa manake atakiwa mleta shida Na si Maendeleo...JPJM NA sisi wote

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad