Wahitimu Chuo cha Utumishi wa Umma Waonywa

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Tawala Bora, Angela Kairuki amewataka wahitimu wa Chuo cha Utumishi Umma nchini (TPSC)  kutojihusisha na masuala ya ufisadi, rushwa na matumizi mabaya ya madaraka kazini badala yake wawe  wachapakazi watakapowatumikia Watanzania.

Kairuki alitoa kauli hiyo kupitia hotuba yake iliyosomwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla alipomwakilisha waziri huyo kwenye mahafali ya 24 ya chuo hicho  yaliyofanyika tawi la Mbeya.

 Alisema   wakati Serikali ya awamu ya tano ikiendelea kupambana na watumishi hewa, mafisadi na wazembe kazini, wahitimu katika chuo hicho wahakikishe wanakwenda kufanya kazi kwa  weledi kwa  kuzingatia kanuni, sheria na taratibu za utumishi popote watakapoajiriwa.

  “Huu ni wakati wenu kuonyesha utofauti kati ya aliyehitimu chuo na kuwatumikia wananchi kwa uadilifu, yule ambaye hajapitia chuo chochote, lakini yupo ofisini utendaji kazi wake unadhihirisha kuwa hakustahili kuwapo mahali hapo,” alisema.

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Samaki mkunje bado mbichi...tena wawe wanafanyiea semina Mara kwa Mara kuwakumbusha mbinu Na uelewa WA jinsi ubadhirifu unavyoanza pindi tamaa inapoingia katika maisha kwa njia Na vigezo Na ushawishi WA aina tofauti...Ili tuweze kuwajenga katika hizi Na mwamko WA kuijrnga Tanzania mpya ya maendeleo..hapa nii. Kasi tuu misingo ndiyo tunaiweka Ili waiendeleze naa masilahi ya nchi Ni juu ya kitu chochote including ya binafsi Na tamaa za maisha...mungu ibariki Tanzania Na watu wake

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad