Mbali na kuzindua mtandao wa 4G LTE kampuni hiyo pia imeimarisha mtandao wa 3G ambao unapatikana katika maeneo yote ya miji mikubwa nchini Tanzania. Akizungumza katika uzinduzi huo Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia alisema “huduma hii ni mpya kabisa yenye kasi ya ukweli na kwa kuanzia itatolewa kwa wateja wote wa Vodacom walio jijini Dar es Salaam na kisha itasambazwa mikoani ili kufikia Watanzania wengi zaidi”
Jinsi ya kubadilisha kadi ya simu kwenda 4G
Mteja wa Vodacom Tanzania atatakiwa kuwa na simu yenye uwezo wa kupata mtandao wa 4G LTE kisha atatembelea duka la Vodacom lililo karibu nae na atapatiwa kadi ya 4G BURE. Mbali na kupata kadi hiyo bila malipo mteja pia atazawadiwa kifurushi cha intaneti chenye 4GB BURE. Baada ya kubadilisha sim card yako, fanya speed test kupitia http://speedof.me/ kushuhudia spidi ya hatari na #Vodacom4G #HapaKasiTu!
Unaweza kufahamu zaidi kuhusu mtandao wa 4G na maeneo unapopatikana kwa kubofya HAPA
http://vda.cm/HapaKasiTu
Tazama video ya msemaji kutoka Vodacom kuhusu 4G
Mmmh ngoja niwatunzie ya moyoni kwa leo...kesho nitakuja kuandika vzr kuhusu hii 4g yenu nyie vodacom..
ReplyDelete