Wimbo wa 'Panya' Wakiponza Kitua cha EATV, Chapigwa Faini ya Milioni 3 na TCRA

Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), imevitoza faini vituo vya East Africa Television na Entertaiment FM (E- FM) baada ya kukiuka kanuni za utangazaji.


Akisoma nakala ya hukumu hiyo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Joseph Mapunda alisema baada ya kupitia maelezo ya utetezi kutoka kwa viongozi wa vituo hivyo, kamati hiyo imeamua kuitoza EATV faini ya Sh3 milioni na Sh4 milioni kwa E-Fm.


“Pamoja na adhabu hiyo tumetoa onyo kali kwa kukiuka kanuni ya maudhui, lakini pia endapo kosa hili litajirudia tunaahidi kutoa adhabu kali zaidi,” alisema.


Katika maelezo ya awali ya hukumu hiyo, Mapunda alisema adhabu ya EATV imetolewa baada ya kituo hicho kupitia kipindi chake cha muziki mnene kurusha video ya wimbo wa Panya wa kundi la muziki la Bracket kutoka nchini Nigeria uliomshirikisha msanii Techno.


“Baadhi ya mavazi yaliyotumika katika wimbo huo hayaendani na maadili ya Kitanzania. Na kwa upande wa E-FM wameadhibiwa baada ya kurusha kipindi cha Ubaoni kilichotoa simulizi ya msichana mchawi aliyekiri kuua,”alisema Mapunda.


Baada ya kupokea nakala ya hukumu hiyo, Mkurugenzi wa EATV, Regina Mengi alisema hawana tatizo na adhabu hiyo na kwamba, atalifikisha suala hilo kwa uongozi wa kampuni yao.


“Bado siwezi kujibu lolote, uamuzi wa kuikubali au kukata rufaa itategemea na uamuzi wa bodi,” alisema.


Mkurugenzi wa E-FM, Scolastica Mazula alisema ameridhishwa na hukumu iliyotolewa, hivyo haoni kama kuna sababu ya kukata rufaa.


Mamlaka hiyo imevitaka vyombo vyote vya utangazaji nchini kuzingatia maadili na taratibu za sheria zinapofanya kazi ili kuepuka kuleta athari katika jamii.
Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. TCRA hatua hii ni muhimu kwa sisi sote tuna jukumu la kulinda maadili na vizazi vyetu kupitia sehemu zetu zote za uwajibikaji..na katika fani zote ambazo zinawafikia jamii...na wafainiwa na shauri waliunge mkono ipasavyo kudhihirisha kwamba wao pia ni wana jamii yenu nia na lengo la kudumisha maadili mema na utamaduni wa Kitanzania..kama utakumbuka watu wa Siha wamefanya bylaws kunusuru mwenendo wa vijana ambao ndiyo taifa la kesho..nawapongeza kwa mwamko huu hii ndiyo nchia mojawapo wa kunusuru Taifa letu la baadae..ambao sisi tutakuwatumeshachoka..to act is Now!!!! hakuna kulala... we should act even faster..Hongera kwa ukemeaji na hongera kwa vituo kulipokea hili..Swebe / Dina tunahitaji ushirikiano wenu positively..ktk kuandaa na kupeperusha maadili ni wajibu wetu sote...

    ReplyDelete
  2. TCRA hatua hii ni muhimu kwa sisi sote tuna jukumu la kulinda maadili na vizazi vyetu kupitia sehemu zetu zote za uwajibikaji..na katika fani zote ambazo zinawafikia jamii...na wafainiwa na shauri waliunge mkono ipasavyo kudhihirisha kwamba wao pia ni wana jamii yenu nia na lengo la kudumisha maadili mema na utamaduni wa Kitanzania..kama utakumbuka watu wa Siha wamefanya bylaws kunusuru mwenendo wa vijana ambao ndiyo taifa la kesho..nawapongeza kwa mwamko huu hii ndiyo nchia mojawapo wa kunusuru Taifa letu la baadae..ambao sisi tutakuwatumeshachoka..to act is Now!!!! hakuna kulala... we should act even faster..Hongera kwa ukemeaji na hongera kwa vituo kulipokea hili..Swebe / Dina tunahitaji ushirikiano wenu positively..ktk kuandaa na kupeperusha maadili ni wajibu wetu sote...

    ReplyDelete
  3. Mbona huku mitandaoni hamfiki mkajionea madudu?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kileo.. Ondoa shaka.. Kote tupo na panapostahili wala usiwe na wasi.. hatua tunachukua.. kwa njia tofauti ikiwemo Onyo/Faini / na usitishaji wa muda..na mengine yanafatia baadae... We are everywhere kwa manufaa ya Jamii na kulinda Utamaduni wetu na Maadili ya Mtanzania..

      Delete
  4. Mbona huku mitandaoni hamfiki mkajionea madudu?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kileo.. Ondoa shaka.. Kote tupo na panapostahili wala usiwe na wasi.. hatua tunachukua.. kwa njia tofauti ikiwemo Onyo/Faini / na usitishaji wa muda..na mengine yanafatia baadae... We are everywhere kwa manufaa ya Jamii na kulinda Utamaduni wetu na Maadili ya Mtanzania..

      Delete
    2. Kileo.. Ondoa shaka.. Kote tupo na panapostahili wala usiwe na wasi.. hatua tunachukua.. kwa njia tofauti ikiwemo Onyo/Faini / na usitishaji wa muda..na mengine yanafatia baadae... We are everywhere kwa manufaa ya Jamii na kulinda Utamaduni wetu na Maadili ya Mtanzania..

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad