Watu wengi wanashindwa kumuelewa Zari anaposema tatizo ni Chibu yani Diamond.
Ali Kiba akitoa wimbo mashabiki wake wanakimbilia kwenye page za Diamond au watu wa karibu yake kulazimisha wausapoti uwezi kuwaona kwa wasio mhusu.
Diamond akipata dili ya tangazo wanaibuka watetezi feki wa haki za wanawake na kulia kwa uchungu kwa nini apewe tangazo ilihali anadhalilisha wanawake! Ukiuliza kamdhalilisha nani? Watakwambia Wema. Kivipi? Hakuna majibu ya msingi.
Tuzo zikitangazwa duniani kote lisipokuwepo jina la Diamond zinapita kimya kimya.. Likiwepo jina lake inaanzishwa kampeni kumpigia kura mnaijeria yoyote ili kumpa upinzani Chibu.
Diamond akisaidia wasanii wachanga kwao sio habari nzuri. Diamond akijenga msikiti kwao sio habari nzuri. Diamond akisaidia mashuleni kwao sio habari nzuri.. Diamond akifanya wimbo na mnaijeria na akitolea video south Africa.. Utasikia sioni kwa nini wasanii wanakimbilia kufanya video nje, mara muziki wetu unakuwa wa kinaijeria.. Kesho nao unasikia wamepanda ndege kufanyia video South Africa au wanafurahi wamepata collabo na mnaijeria.. Kwa Diamond muziki unakufa, wao wakivuka boda muziki unakuwa.
Lazima tukubali Diamond kwa sasa ndio daraja letu la kuivusha bongo fleva.. Wapo wasanii wamefanya makubwa kuufikisha huu muziki hapa kina Prof J, AY, Sugu nk lakini kiukweli Diamond amekuja kufanya mapinduzi makubwa mno. Kuna watu walifanya harakati nyingi kuubadili muziki umlipe zaidi msanii wengine waliishia kutukana matusi na ubabe ila Diamond katumia njia za kisayansi kuibadili game yetu na kiukweli game kaibadili mno ata km atupendi kukubali hili. Vitu wanavyofanya na njia wanazopita sasa yeye ametoka huko miaka 4 iliyopita.
Wakati Kiba anafurahi kusainiwa label ya kimataifa. Diamond anapambana kuipeleka label yake kuwa ya kimataifa, baada ya miaka mitatu wengi ndio mtaelewa tofauti ya Chibu na wengine.
Mtamchukia Tiffa, Zari, Babu Tale, Sallam, Fella, Kifesi lakini awa ni kafara tu ishu hapa ni Diamond. Awa wangekuwa mtaani huko awausiki na mafanikio ya Diamond wasingekuwa tatizo.
Ata ugomvi wa kifamilia kati ya Esma, mama Diamond na Zari ishu sio Zari anajisikia ishu ni Diamond kashindwa kubalansi upendo, upendo umeelemea kwa Zari na Tiffa.. Mama na dada wanaona ule umiliki wa imaya unapungua siunajua tena mambo yetu waswahili kukaba ata kama mtu kashaanza maisha ya familia . Kwa hiyo jamani kelele zooote tatizo ni Chibu.
Zari Hassan Anaposema Tatizo ni Diamond, Hii ndio Maana yake
11
May 22, 2016
Tags
Sijaelewa chochote naona umeandika non sense tuuu...nawaelewa zaidi wenye vipaji vya muziki hawa wengine sielewi wanafanya nn wala wanaenda wapi...wenye vipaji akiwemo kibaaaaa....barnabaa banana zoroo ukisikia vokali zao lazma ulale the rest....to me thy r just.......noninooo hahahaha
ReplyDeleteMsemaji ndio mawazo yake yeye ila anajifanya ni ya watu wengine. Diamond adui yake ni wewe mwandishi. Tena unajikomba tu. Mi hapa nilipo napenda mziki wa D na naona anafanya vizuri ila sipendi maneno yako mchonganishi tu na huna kazi. Get a life!
ReplyDeletetoa funza kichwani. maoni yako hayana mshiko wala hayana mtazamo muhimu.
ReplyDeletehuyo muuza tomato za wahindi anaporomoka kama si kuanguka. wewe mpambe tuu na bibi kizee wake. hana jipya kwa sasa
ReplyDeletesasa si umngoje aporomoke? mbona una haraka hivyo? watu wengine bwana wivu mpaka unashindwa kujielewa? mtabaki ohhh muuza tomato, mwenzenu anaingiza hela. mkalage baho. pole we, kasafishe moyo wako na sabuni basi utasikia nafuu. watu gani nyie msio na jema!
DeleteJamani mbona Lady Jay Dee kanenepeanaaa????? Nyimbo ni nzuri lakini kwa ile figure hata hapendezi kwenye stage.
ReplyDeletekaanza dozi
Deletesi ndo hao watu wazima wasotaka kuitwa bibi? Anony 11.49 AM
ReplyDeleteDomo siku hizi akifanya shoo mpaka aletewa staa kutoka nje ili watu wajae. naona hata kibib chake kimechoka kumpa kiki. ale tomato tuu.
ReplyDeletenahisi unatafuta kujisogeza kwa D, maana haya mawazo unayoandika ni mawazo yako . Umelala umeamka na kuwasha kompyuta yako na kuanza kuandika.Kiufupi pointless!!!!
ReplyDeletekwa kifupi bila kutaja jina la mtu. tuangalie maeneo machache tufanye analysis kwa wanamuzki wetu wa bongo:
ReplyDelete1. awards achievements; local and international wards, nani anazo nyingi?
2. mafanikio ya kimaisha, vitu kama nyumba, magari
nk.
3. mikataba na makampuni mbalimbali, local and international.
4. balance za bank accounts, hili najua ni vigumu kulithibitisha.
5. show nying za kimataifa.
6. idadi ya hit songs
7. idadi ya collabo, both local na international
8. strenth ya label ya wanamuziki wetu
alfu muanze kutoka mapovu mbwa koko nyie....