Zitto: Millioni 50 za Magufuli Kila Kijiji ni Hadaa Kwa Wananchi.

MBUNGE wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe, amesema Serikali ya Awamu ya Tano imewahadaa wananchi kuhusu kuwapa Sh. milioni 50 kila kijiji/mtaa huku akiamini ahadi hiyo haitekelezeki.

Zitto alisema ahadi hiyo "kimahesabu, haitekelezeki."

"Kwanza kwenye bajeti ya Waziri Mkuu, fungu lililotajwa la Sh. bilioni 59 halipo. Na hata kama lipo Tamisemi wanakodai wao (Ofisi ya Waziri Mkuu), halitoshi kuvikopesha vijiji vyote Tanzania," Zitto alisema na kuongeza:

"Sh. bilioni 59 katika mwaka wa fedha 2016/17 maana yake vijini 1,000 tu vitapatiwa fedha. Kama serikali inatekeleza ahadi hiyo kwa vijini 1,000 kila mwaka, maana yake ni kwamba katika miaka mitano ya Rais Magufuli Ikulu, ahadi hiyo itatekelezwa katika vijiji 5,000 tu.

"Huku ni kuwahadaa wananchi. Tanzania ina zaidi ya vijiji 15,000. Kwa fungu linalotengwa, vijini zaidi ya 10,000 havitapata fedha hii."

MASHARTI MAGUMU

Wakati Zitto akitoa tahadhari hiyo, imebaini kuwepo kwa vigezo vya kupata fungu la Sh. milioni 50 za kila kijiji/mtaa ni vigumu.

Akihitimiha mjadala wa makadirio ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu katika mwaka wa fedha 2016/17 wiki iliyopita Majaliwa, alivitaja vigezo saba vitakavyotumika kugawa fedha za mradi huo, huku vyote vikionekana vitakuwa na ugumu kunufaisha wananchi wengi hasa katika maeneo ya vijijini.

Majaliwa alisema mradi huo unalenga kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa njia ya kukopesha vikundi vya wajasiriamali kupitia ushirika wa kuweka na kukopa katika vijiji.

Alivitaja vigezo vya kukopeshwa fedha hizo kuwa ni kikundi cha kifedha kiwe kimesajiliwa na Halmashauri na Tume ya Ushirika, kikundi kiwe na Katiba, uongozi uliochaguliwa kidemokrasia na kupata mafunzo ya mikopo pamoja na kikundi hicho kuwa chini ya Asasi ya Kiraia inayotambulika na yenye uzoefu wa shughuli za mikopo.

Majaliwa alikitaja kigezo cha nne kuwa ni kikundi husika kionyeshe uzoefu wa kukopeshana kwa muda wa mwaka mmoja tangu kuanzishwa na historia ya urejeshaji mikopo ya asilimia 95 na cha tano ni kuwa dhamana ya serikali itakuwa kwenye kiasi cha msingi cha mkopo na si kwenye kiasi riba.

"Kigezo cha sita ni kikundi kuweka amana ya akiba ya fedha kwenye benki katika akaunti maalumu (Fixed Deposit) asilimia 10 ya mkopo," alisema.

Majaliwa alisema kigezo cha saba ni kuzingatiwa kwa Sheria ya Vyama vya Ushirika ya mwaka 2013 kuhusu mkopo kwa SACCOS.

Alisema serikali imeandaa mpango wa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu suala hilo hususan masuala ya ujasiriamali na biashara

Chanzo: Siasahuru.com 

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kabwwe nani walokupa kura. .i deem you to be so negative..yaani umeguubdua uongo WA huu mchakato WA Nia njema kabisa...umejuwa mjabja unaukosoa!!! Ama kweli... Unahitaji. Kujua kifikra na. Kimaadili... Mimi ningekuwa nafasi yako wewe bado ningelipongeza na kusema huu Ni mwanzo Tu... Na urudishaji ukiwa nzuri na vigezo kufatwa. Pesa zingine zitaongezwa kwa kuzizingusha na Kula mjasiriamali akifanikiwa ajiangalie mwenzake ataweza kushirikiana naw vipi; hapo ttutajenga hisia na mwamko..Badilika Zitto na uwe positive rather than negative as demonstrated...SWEIKALI HII YA AWAMU YA TANO INA NIA NJEMA..NADHANI WEWE PIA UNAJIA ILA HUTAKI UELEWWKE HIVYO..JPJM ANAFANYA WAJONU WAKE..TAFADHALI KAA PEMBENI KIMYA..USIJIFANYE MJUAJI WA KILA KITU..KUNA METHALI NATAKA UITAFAKARI INASEMA HIVI " ONLY FOOLS KNOWS EVERYTHING" NAOMBA UTAFAKARI MARA KUMI. HALAFU UPATE JIBU ZITTO..HAPA NI KAZI TU..WE MEAN BUSINESS

    ReplyDelete
  2. Hawezi kaa kimya na kwanini akae kimya dunia haijabeba Malaika jamani

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huyu kijana Ana yake Aombe mungu hiyo miaka ijayo Kama watampa kur zao..Lakini Mimi kwa hii tabia yake. Yangu haipati

      Delete
  3. Mbona comments hazichapishwi za huyu Dogo

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad