Afariki Baada ya Kuchapwa na Wazee wa Kimila

Picha ya Tukio jingine
Mtu mmoja mkazi wa Kijiji cha Kandashi, wilayani Siha, mkoani Kilimanjaro, Abedi Akyo (53), amefariki dunia baada ya kudaiwa kuchapwa viboko na wazee wa kimila kwa tuhuma ya kujihusisha na wizi wa kuku.

Akielezea mazingira ya kifo hicho, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilfred Mutafungwa amedai kuwa Akyo alichapwa viboko 70 na wazee hao wa kimila wa Kimeru na Kimasai.

Mutafungwa amesema watuhumiwa watafikishwa mahakamani baada ya kuwasiliana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Mwezi uliopita  wakazi wa Kata ya Karansi wilayani hapa  walitoa uamuzi kuwa wanawake watakaovaa sketi fupi na vijana watakaovalia suruali chini ya kiuno, wataadhibiwa kwa kuchapwa viboko 60 hadi 70.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hizo ndizo mila na desturi zili-funktion enzi zile za stone age sasa hivi kuna kitu kinachoitwa "usalama"au"Police"na mahakama huko ndiko hupelekwa mtuhumiwa ili sheria itendeke na siyo vinginevyo haya sasa mmemuua huyo mume wa mtu na baba wa watu bure utampigaje mtu mmoja viboko X70 nyinyi mnaojiita eti wazee wa kimila hamfai kabisa yaani ni wazee hovyoooooo sometimes mnakera kweli na mila zenu zilizopitwa na wakati people wake up we're going forward and not backward

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad