Mshambuliaji wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe ameushauri uongozi wa klabu hiyo kuhakikisha unasajili kiungo mkabaji (namba sita), wa nguvu katika kipindi hiki cha usajili ambaye atakuwa msaada mkubwa kwa timu hiyo.
Tambwe ambaye ndiye mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu huu akiwa na mabao 21, amesema Yanga inakabiliwa na tatizo kubwa la kiungo mkabaji mwenye uwezo kupambana muda wote wa mchezo.
Alisema hali hiyo ndiyo imekuwa ikiisumbua timu hiyo katika mechi zake za kimataifa jambo ambalo uongozi wa timu hiyo unapaswa kulifanyia kazi katika kipindi hiki cha usajili.
“Tuna viungo wengi wazuri lakini bado tunahitaji kiungo mkabaji wa nguvu ambaye atakuwa anashirikiana vilivyo na mabeki wetu katika safu ya ulinzi.
“Uongozi wetu unatakiwa kuliona hilo na kulifanyia kazi katika kipindi hiki cha usajili kabla ya kuanza kushiriki michuano ya kimataifa ambayo itakuwa na ushindani mkubwa kutokana na aina ya timu tutakazokutana nazo,” alisema Tambwe.
Tambwe uko sahihi 100%, mimi Mwana Yanga nakuunga mkono. Timu kwa sasa imekamilika isipkuwa mambo machahe ya kurekebisha kama hilo alilosema Tambwe. Pamoja na changamoto na hujuma zinazotukabili Wana Yanga sasa hivi, naomba uongozi, wanachama na mashabiki wote tuwe watulivu tuzidishe umoja kipindi hiki muhimu cha kuongeza mafanikio kwenye Kombe la Shirikisho. Naamini tutawashinda maadui na wapinzani wetu wa ndani na nje na kuchukua ubingwa. Ushauri wa Tambwe uzingatiwe haraka, 'DAIMA MBELE, NYUMA MWIKO'.......
ReplyDelete