Askari Wasiopigia Saluti Wabunge Kukatwa Mishahara


Agizo hilo limetolewa leo bungeni na Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Tate Ole-Nasha wakati akijibu swali la nyongeza kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani la mbunge wa viti maalum kutoka Zanzibar Fakharia Shomari aliyetaka kujua ni kwanini askari wa jeshi la polisi hawapigi saluti kwa wabunge.

Katika maelezo yake, Ole Nasha amesema kuwa askari wote nchini ni lazima wazingatie taratibu hizo, na kwamba wanapaswa kupiga saluti kwa wabunge kila wanapowaona, na endapo hawatafanya hivyo, watakumbana na adhabu za kijeshi.

Ametaja baadhi ya adhabu watakazokabiliana nazo kuwa ni pamoja na kukatwa mshahara, kufanyausafi wa mazingira, kuondolewa kikosini kwa muda n.k. na amewataka wabunge ambao hawatapigiwa saluti, kuripoti haraka mahali husika.

Akiongozea majibu hayo, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi amesema agizo hilo linakwenda hadi kwa askari wa makampuni binafsi ya ulinzi ambao mara nyingi hupuuza kutoa heshima hiyo kwa viongozi hususani katika mabenki.


Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Si wanaona sakata zao za utovu wwa nidhanu .sasa akinkuta anacuta sigara zile za marufuku au unga. Amkanate. Ha anfukishe mahali husika Na mkondo WA sheria ufate .

    ReplyDelete
  2. Makubwa
    Poleni polisi
    Kamatani wapinzani kwa kuwapigia saluti
    Ipo haja ya kurudidha neno ndugu kote Tanzania

    ReplyDelete
  3. Msiwanyime watoto wa Askari chakula kwa kupenda uheshimiwa. Kama lazima sana hiyo heshima wapeni push up 100 ndio adhabu za kiaskari. Wabunge wa sasa wanaanza kunikera si uongo.

    ReplyDelete
  4. dah,samahani wangu hio kometi hp nimeisoma lkn sijaielewa,naomba kuwasilisha

    ReplyDelete
  5. Fyuuu eti hata walinzi binafsi
    Stela ukienda benki panga foleni Kama wengine
    Wabunge wa ccm hao
    Polisi mpo

    ReplyDelete
  6. only in TANZANIA LOL!

    ReplyDelete
  7. Magufuli hili nalo jipu bungeni
    Saluti kwa wabunge
    Fyuuuuuuuuuu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad