Baada ya kuoa mwanamke mwingine, Isabella adai ni yeye ndiye alimpiga chini Kalama, adai ni mwanaume asiye na future

Baada ya rapper wa kundi la Gangwe Mobb, Luteni Kalama kuoa mwanamke mwingine na kumwacha mchumba wake aliyemvisha pete, Isabella ameibuka na kudai kuwa ni yeye ndiye aliyemwacha baada ya kumuona ni mwanaume asiye na future.

“Mimi na Kalama tulikuwa tumeshaachana muda mrefu kwasababu nimeona ni mwanaume ambaye hana future hawazi chochote, kwahiyo nikaona kwanini nijipotezee muda. Mwanaume anaamka saa saba, kwahiyo nikaona niachane naye,” Isabela alimuambia mtangazaji wa Jembe FM, Natty E.

“Lakini watu wameona ilivyotokea gazeti wanahisi labda Kalama aliniacha mimi kitu ambacho sio kweli, hana uwezo wa kuniacha, mimi ndio nilimuacha. Na nafikiri stress zake ndio zimemfanya aende akamuoe rafiki yangu sasa si ni uchizi. Halafu mwanamke unaoa unaenda kukaa kwa mwanamke tena, yeye si ndio anakuwa ameolewa, kwahiyo yeye ni mwanaume ambaye ni kilaza,” aliongeza Isabela.

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. SIZITAKI MBICHI HIZI

    ReplyDelete
  2. Inaelekea imekuuma sn jamaa kuoa?!mbona unamwongelea sn?

    ReplyDelete
  3. Hata Wema alidai kuwa ndie aliemuacha ndomo. Lakini anaumiaaa akimuona ka move on.Haishi kulipa watu ili wamchambe mama Tiffah. Halafu anapoza kwa kumuombea kura Domo.Kasubiri arudiwe kaona siku zinapita. Pole na wewe

    ReplyDelete
  4. Na ww olewa basi km rahisi.si useme tu km imekuuma mshkaji kuowa.

    ReplyDelete
  5. kwa unavyoelezea kama ni kweli alikuwa anaamka saa saba na kama kweli kaenda kuishi kwa bibi harusi basi ni kweli huyo mwanamme kaolewa na kule ameenda kuganga njaa wala sio upendo! ila ni kwa maisha ya siku hizi ni kawaida vijana wa kiume kuolewa na majimama. ni uvivu si mapenzi.

    ReplyDelete
  6. nimesoma kwenye blog eti unataka kufanya biashara ya kupiga picha za uchi kwa dili la mamilioni? tatizo nani anataka kukuona wewe ukiwa uchi kwanza sura huna wala si mrembo

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad