Babu Tale asema ni bahati kwa wasanii wa ‘WCB’ kupata wanawake wenye umri mkubwa zaidi yao (Video)

Baada ya kambi ya WCB kuonekana wasanii wake wanapenda kutoka kimapenzi na wanawake wenye umri mkubwa zaidi yao, uongozi wa kambi hiyo umelizungumzia swala hilo.
Diamond, Harmonize

Akizungumza na waandishi wa habari Alhamisi hii, Mmoja kati ya viongozi wa juu wa kambi hiyo, Babu Tale, amesema ni bahati kwa wasanii wake kupata wanawake waliowazidi umri.

“Sisi tunameneji wasanii hatumeneji hisia zao, lakini ikitokea msanii fulani amempenda mwanamke fulani tunamuacha kwa sababu ni mapenzi yake,” alisema Tale. “Tunaona ni bahati kwa wasanii wetu kupata wanawake waliowazidi umri, hiyo ni bahati (anacheka) kwa sababu wanamuenzi Mtume Muhammad (s.a.w.w.) alimuoa Bi Khadija ambaye alimzidi umri,”

Hata hivyo, Tale alisema ndani ya WCB hawameneji mapenzi bali wanammeneji msanii pamoja na kazi zake.
Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. wacha ujinga Tale, kwani hao wasanii wako wameoa mpaka wamuenzi mtume?

    ReplyDelete
  2. MTUME MUHAMMADI HAKUZINI WALA KUZAA NJE YA NDOA. ALIMUOA BI HADIJA. USIIPOTOSHE JAMII NA WAISLAM KWA SABABU YA KUWASAFISHA WAJINGA WENZIO TALE.

    ReplyDelete
  3. babu tale mbona wewe hukuoa mzee! usijinyanye unajua kuwangia kifua wakati ni wachafu wa zinaa! rudi shule kasomee Qur an.

    ReplyDelete
  4. kwa nchi nyingine ungenyongwa kwa kosa la kumfananisha mtume na makahaba yaliyoshindikana!

    ReplyDelete
  5. ksjifundishe dini kwanza halafu uje uwafananishe hao mabwege kwanza Mtume hajaoa mke kafiri walevi wewe tale unajua umekosea sana na Mwenyezi Mungu atakuadhib sana haya tuone wcb muendele sasa wote hao wanayo fanya ni laana

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad