Barua ya wazi kwa Freeman Mbowe na UKAWA wote

Na Thadei Ole Mushi.

Kama ni mfuatiliaji wa siasa za Tanzania mbinu ya wapinzania kutoka njee ya bunge kwa sababu mbali mbali haikuanza leo. Na tangu wameaanza kuitumia mbinu hii haijawahi kuwasaidia au hata kueleweka kwa wananchi badala yake sisi wananchi ndio huwa tunapata hasara.

Kwa mara ya Kwanza wapinzani walitoka njee ya Bunge wakati raisi Kikwete alipoingia madarakani kwa mara ya pili kwa kile walichokidai kuwa ni kutomtambua. Walitoka njee wakati wa kuhutubia bunge na kulifungua bunge.

Je waliposusia bunge mwisho wa siku hawakuja kumtambua raisi Kikwete?? jibu ni NDIO wakikuja kumtambua na walivunja rekodi kupiga hodi ikulu kuomba busara za raisi kuliko vipindi vingine vyote.Tuliwashuhudia wakiburudika na juice mara nyingi tu Ikulu wakipata picha ya pamoja nk.

Mara ya pili tunawaona upinzani ukitoka njee kususia bunge la katiba. Mwisho wa siku bunge liliendelea na katiba pendekezwa ikapitishwa bila kuwa na mawazo mbadala ya wapinzani ndani ya katiba ile inayosubiria kupigiwa kura.

Mara ya tatu upinzani unatoka njee kupinga matokeo ya uraisi yaliyompa raisi Magufuli ushindi. Wanatoka siku ya raisi kulifungua bunge kama walivyotoka kipindi cha Kikwete. Raisi analifungua bunge na baada ya hapo bunge lilelile lililopewa uhalali na rais Magufuli baada ya kulifungua wapinzani wanarudi na kulitumia. Na hata sasa wapinzani wameshamtambua raisi Magufuli kuwa ni raisi halali na aliyechaguliwa kihalali.

Mara ya nne ni hili la kumkimbia Dr Tulia. Katika hali ya kawaida nilifikiri wangelifanya hivi kwa siku moja tu. Mpango wa kususia kila siku kumetuathiri sana sisi wananchi kuliko kulivyomuathiri Dr Tulia. Tena wapinzani wanatoka njee kipindi muhimu kabisa ambacho walipaswa kuombea majimbo yao miradi ya kimaendeleo toka kwenye bajeti ambayo itapitishwa muda mfupi ujao.

Upinzani umetoka kwenye mstari wa kujenga hoja hadi kususia kususia mambo ya ajabu ajabu.Nakiri kabisa kuwa kilichoijenga kambi ya upinzani nchini ni hoja zao nzito miaka ya 2005-2015.

Sote tunakumbuka jinsi upinzani ulivyopata umaarufu kwa kujenga hoja za kukataa ufisadi, kudai katiba mpya, swala la Buzwagi, na hata juzi juzi swala la ESCROW. Kafulila pamoja na kutukanwa tumbili alisisimama kidete hadi akafanikiwa kuwangoa kina Warema bungeni na wengineo. Nataka nikuonyeshe nguvu ya hoja ilivyo na mantiki kuliko hii zomea zomea na kutoka nje ya bunge.

Katika nchi zote za jumuiya ya Madola Tanzania upinzani ndio unaongoza kwa kuthaminiwa kuliko nchi zote. Thamani hii upinzani umeshindwa kuutambua na kuutumia kujijenga badala yake wamekimbia na kinachowakimbiza ni kanuni walizojiwekea wenyewe.

Ni Tanzania tu katika ukanda huu Kambi rasmi ya upinzani inatambulika bungeni, kuwa na baraza la mawaziri kivuli, na baadhi ya kamati nyeti zinazogusa maslahi ya Taifa kuwekewa kanuni lazma ziongozwe na upinzani kama PAC nk.

Hii ni fursa ambayo upinzani walipaswa kuitumia kujitangaza kuliko kuzurura njee ya viwanja vya bunge. Inauma sana kuona wanakosea na hawataki kujirekebisha.

Naamini si wabunge wote wa upinzani wanataka kutoka njee ya Bunge lah hasha. Prof Elton Mayo aliwahi kutoa nadharia ya Hawthorne Effect, nadharia ya kisaikolojia ambapo mtu hufanya jambo kwa kuwa tu kuna mtu anayemsimamia kufanya hivyo au anafanya tu kwa kuwa anajua anaonekana anachokifanya. Hivyo unafanya jambo si kwa kuwa unapenda kulifanya ila unafanya kwa kuwa kuna sababu zinakufanya ufanye.Nikiangalia huu utoto anaoufanya Mbatia pamoja na uelewa wake wote naona madhara ya mob psychology.

MBOWE nakuomba usitumie tena mbinu hii haiwajengi inawabomoa.

Ole Mushi.

MwanaCCM mwenye kujali maslah mapana ya nchi.
Tags

Post a Comment

16 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mwacheni Mbowe
    Kama uozo wenye miaka 54 Upo CCM

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe mwenyewe umeoza sio ajabu kumkingia kifua mtu hata anaposhauriwa cha maana kwa masilahi ya umma unaona watu wanakosea

      Delete
    2. sitakaa nipige kura kumpa mbunge wa chadema, wananiboa kuliko kawaida

      Delete
    3. 2tawapa cc

      Delete
    4. 2ta wapgia cc ila co hao ccm

      Delete
    5. waachen tuwapime uwezo wao, utasikia lijengwe sanamu la mond,mwingne uwanja wa pushapu wa mh.ukarabatiwe uwe makumbusho,mwingne bla aibu unamckia mim nmemuitia mwanangu jna la 2lia,cku zote hutumia muda mwing kuponda upinzan dk3 ndo anajadl muswada sasa upnzan hawapo point zakuanzia hawana vmebak vioja tu

      Delete
  2. Mdau Umenena ya Busara. Mimi naomba kwa sisi Watanzania bila kujali huyu ni CCM/CDM/TLP/NCCR/CUF nasema Watanzania na kitushike sote uzalendo Siasa hatuzijui na hatuziwezi.. Tuwe Wazalendo wenye kujali Maendeleo na Masilahi ya nchi... Naomba tukae tuwaze bila kufata au kujijua natoka Chama gani.. na haya mawazo ya sijui demokrasia na udikteta Kwanza hatuna uelewa mzuri wa haya... Lakini napenda kukumbusha Mtu kama raisi wetu Mwiteni mnavyo ona nyinyi Ukweli ni kwamba Mataifa yaliyopata Maendeleo Viongozi wake walikubali haya yote na waliwaweka ndani wote waliokuwa na firimbi firimbi ambazo zingerudisha Kasi ya Mabadiliko na WAMEFANIKIWA.. Kwa hiyo sijui Dikiteta / Bana Demoklasia yote mtayaimba na Sisi tutaziba masikio manake tukukusikilizeni tutaduwaa na kasi haitokuwepo na mwelekeo kukosa Dira... Sisi Wazalendo tunasema .. Mtaicheza ngoma hiyo peke yenu.. Kasi yetu iko pale pale na itazidi Chini ya awamu yetu hii ya Tano...JPJM endelea Baba na ziba masikio na tuko bega kwa bega... Hapa Kazi tuu...

    ReplyDelete
  3. Mdau Umenena ya Busara. Mimi naomba kwa sisi Watanzania bila kujali huyu ni CCM/CDM/TLP/NCCR/CUF nasema Watanzania na kitushike sote uzalendo Siasa hatuzijui na hatuziwezi.. Tuwe Wazalendo wenye kujali Maendeleo na Masilahi ya nchi... Naomba tukae tuwaze bila kufata au kujijua natoka Chama gani.. na haya mawazo ya sijui demokrasia na udikteta Kwanza hatuna uelewa mzuri wa haya... Lakini napenda kukumbusha Mtu kama raisi wetu Mwiteni mnavyo ona nyinyi Ukweli ni kwamba Mataifa yaliyopata Maendeleo Viongozi wake walikubali haya yote na waliwaweka ndani wote waliokuwa na firimbi firimbi ambazo zingerudisha Kasi ya Mabadiliko na WAMEFANIKIWA.. Kwa hiyo sijui Dikiteta / Bana Demoklasia yote mtayaimba na Sisi tutaziba masikio manake tukukusikilizeni tutaduwaa na kasi haitokuwepo na mwelekeo kukosa Dira... Sisi Wazalendo tunasema .. Mtaicheza ngoma hiyo peke yenu.. Kasi yetu iko pale pale na itazidi Chini ya awamu yetu hii ya Tano...JPJM endelea Baba na ziba masikio na tuko bega kwa bega... Hapa Kazi tuu...

    ReplyDelete
  4. Ole Mushi, Nasiha zako kwa hawa ndugu zetu ni sahihi.. Kwani wakikaa na kutafakari wanacho kifanya ni kwamba wanamyima haki aliyempa kura yake ya thamani kufikiria kwa dhana nzuri ya yeye kuwakilishwa lakini kinachoendelea ni kwamba inaonesha Kutojali wala Kutoathirika na anajua atamaliza hiyo miaka mitano aliyopewa mpaka wananchi watakapo mpata Mzalendo mwingine wa kuweza kusalisha matatizo yao ya kimaendeleo na kuwaombea mambo stahiki katika serikali. Labda wakisoma wanaweza kujirudi na kuwa Wazalendo wa nchi yetu.. na kurudisha mwelekeo.. Manaake kama wahisi hawawezi kufanya kazi na Dr.Tulia atabidi wahame nchi na siyo bunge kama wanataka kuendelea kuka viambazani hapo Bungeni... JIRUDINI BAADA YA KUTAFAKARI.. HII HAIJENGI NA MBOWE KAMA WEWE NI RING LEADER BASI JIUZULU NA UMWACHIE MZALENDO ATAKAE WEZA KUSHIRIKI KIKAMILIFU KULETA MAENDELEA NA SIO SIASA UCHWARA AMBAZO HATUZIJUI.

    ReplyDelete
  5. Acha waoneshe hisia zao tumechoka Na uongo WA ccm

    ReplyDelete
  6. watz maliyewaroga kashakufa na hamtakaa mjielewe hata siku moja. Fanyeni kazi zetu hayo ya wabunge wa upinzani waachieni wenyewe maana haiwahusu. Mwenye maslahi na ccm lazma atatetea upuuzi wa tu. We unadhani kama sio kumgomea jk angekua anawaita ikulu kuongea nao???How do you compare kumgomea kutokumtambua rais na huyo naibu spika aliyebebwa kwa maslahi ya watu........Kama unataka kuongozwa kama mbuzi ni ww tu lkn watu wenye akili na maono hawapo tayari kuburuzwa.kaa kimpa

    ReplyDelete
  7. hao waliong'olewa kutokana na escrow wengine wamerudishwa na kafulila kafanyiwa zengwe out......Hivi mnaongea nini nyie. Yani unaona kabisa refa anavyoibeba timu bungeni anapiga watu red kadi just kwa sababu mtu anapiga chenga nyingi halafu unasema unashundana.mnakurupuka tu hamjui ila Tulia hana uzoefu na bunge na anapewa maelekezo tu basi anasimamia humo anashindwa kubalance......acha wapinzani wagome tu.....kuwafukuza bungeni Lisu...Mdee....Lema....ZZK....nk ni hujuma iliyopangwa makusudically. Acha wapitishe hiyo bajeti yao ccm na hyo Finance bill yao maana hawataki kukosolewa. Then itakuja kula kwenu wananchi ndo mkome

    ReplyDelete
    Replies
    1. Pumbavu we Wananci ndiyo tukome??? Kivipi Tukome???

      Delete
  8. Navoona nenda bungeni ukaangalie mijadala inavokuwa then uje useme upande upi una makosa ila kwa sasa mm nahisi umetumia taarifa za mtandaoni ww kama mshauri ulitakiwa ukashuhudie live mzunguko mzima then comment

    ReplyDelete
  9. waacheni haohao,c ndo wanataka wabaki wao,ngojeni tuwapme uwezo wao,wengne utasikia ujengwe mnara wa mond,mwingine uwanja wa pushapu wa mh.ukarabatiwe,mwingne bla aibu anasema mimi nimemuitia mtt wangu jna la 2lia,cjui ndo matatzo yanayowasumbua wananchi wao,hawa cku zote hutumia muda mwingi kuwaponda upinzan zkibak dk3 ndo anaanza kuchangia muswada,sasa upinzan hawapo point hawana vmebaki vioja tu

    ReplyDelete
  10. Nivema tukafahamu kwa undani nini Kimepelekea Mh. Mwenye Chair ku mobilize wenzake ndipo tulaumu ila kimsingi wangebaki tu humohumo wakajaritu kujenga hoja ili waone ni vp wanaweza kutatua matatizo ya wananch wapga kura la sivyo wakiloba step tu 2020 inaweza kuwa ngumu kwa upinzani

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad