Ajali zimeendelea kutokea katika barabara za mabasi yaendayo haraka ambazo zimekuwa zikisababishwa na madereva wasiotaka kufuata sheria za barabarani ambapo leo katika mataa ya kuongozea magari Shekilango basi moja liendalo haraka limegongana na pikipiki.
Ajali hiyo ambayo haikusababisha vifo wala majeruhi imetokea majira ya saa sita ambapo kwa mujibu wa mashududa dereva wa boda boda akiwa na abiria mwanamke alikuwa akikatiza kwenye taa hizo akitokea upande wa soko la shekilango akielekea milleniam park huku taa zikiwa zimeruhusu basi hilo kupita na kusababisha kugongana na pikipiki kupinduka.
Askari wa usalama wakiwa katika harakati za kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo akatokea dereva
mwingine wa bodaboda kukatiza katika eneo hilo bila kufuata sheria ambaye nae alikamatwa na kuambatanishwa na waliosababisha ajali hiyo na kupelekwa kwenye vyombo vya dola kwa hatua zaidi.
Basi Moja Liendalo Haraka Limegongana na Pikipiki Shekilango Dar es Salaam
2
June 03, 2016
Itungwe Sheria Kama holand kwenye barabara za waendeshao baskel ukigongwa unamlipa mwenye kukugonga ukishindwa jella Miaka 6 bila fain ha kuna kuendesha kesi moja kwa moja jella Mbona iko poa mzee magufuri hapa kazi
ReplyDeletePeolpe here we go again!Wahenga hawakukosea kabisa waliposema masikini akipata na matako ulia mbwata na bado kwa ushamba wa wabongo jinsi walivyo tutayashuhudia matukio mengi sana kunako hizo barabara za mabasi yaendayo kwa kasi
ReplyDelete