CCM Yatangaza Kuzunguka Nchi Nzima Kuwakabili CHADEMA Waliojipanga 'Kumharibia' Rais Magufuli kwa Wananchi

Siku chache baada ya Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutangaza kufanya mikutano nchi nzima kwa lengo la kuishtaki kwa wananchi Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli, CCM wamejibu mapigo  kwa kuapa kuwafuata kila kona watakayopita.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka alisema kuwa chama hicho hakiwezi kuvumilia kuona Chadema wanazunguka kuharibu taswira ya Rais Magufuli na Serikali yake ambayo alieleza kuwa imefanya kazi kubwa kuwatumikia wananchi katika kipindi kifupi.

Alisema kuwa wamepata taarifa zisizo na shaka kuwa Kamati Kuu ya Chadema iliyokutana Mei 16 mwaka huu ilibaini kuwa kwa muda mfupi, Magufuli ametekeleza ajenda zote ilizokuwa ikinadi wakati wa Uchaaguzi Mkuu.

Ole Sendeka alisema kuwa utendaji wa Rais Magufuli unatuma ujumbe wa dhahiri kuwa Chadema watashindwa tena katika uchaguzi wa mwaka 2020.

Aliongeza kuwa malalamiko ya udikteta wanayoyasambaza yanaonesha kuwa hawana mjadala wowote wa kumkosoa Rais Magufuli.

“Tunawaonya viongozi wa Chadema. Wanapaswa kutumia majukwaa hayo kunadi sera za Chadema. Nataka kuwahakikishia kuwa, kama Chadema wataenda sehemu fulani Jumatatu, sisi tutakuwa pale Jumanne kusafisha hali ya hewa kwa kuwaeleza ukweli wananchi,” alisema Ole Sendeka.

Chadema wamepanga kufanya mikutano nchi nzima kwa kile walichoeleza kuwa ni kuishtaki Serikali kwa wananchi kuhusu mwenendo wa Serikali ikiwa ni pamoja na kubanwa kwa Demokrasia na Bunge kwa ujumla na utumbuaji majipu usiofuata sheria na taratibu.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wala haina haja. Vyombo vya dola vipi. Mchafuzi Na mchochezi WA kuvuruga Amani atashughulikiwa ipasavyo tena kwa nguvu zote kwanza wananchi wenyewe wameshaona Na kujua yapatapa Yao..hiyo ikitokea tutawafikisha panapo husika Na watoto zetu wakiumia jua hapo tutachukua sheria mkononi dhidi Yao. Halafu mahakama itachukua ya waliopoteza roho Na Itakuwa hadi mbaya zaidi Mbowe Na kundi laki jitambueni Na uchu wenu Na ikithibiti hata lowassa Yuko kimya Na fediliki..kingunge si mwenzrnu ameshachoka. Tunangoja Na kuangali au maneno?? Spidi JP. Ina dhihirisha ujrnzi Na nidhamu ya hali ya juu

    ReplyDelete
  2. CCM CHADEMA MUNAWAOGOPA MUNAJUA KAMA WANA NGUVU KWA WANANCHI, KAMA NYINYI MNA NGUVU KWA WANANCHI MUNGENYAMAZA KIMYA

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mdau Ni simba au maniyuu..au alisinali?

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad