CHADEMA Waishitaki Serikali Mahakamani

MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, jana alifungua kesi ya madai katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, kupinga amri ya polisi kuzuia mikutano ya vyama vya siasa nchini.

Kesi hiyo namba 79 ya mwaka 2016, ilifunguliwa jana na kusimamiwa na mawakili watatu Gasper Mwanalyela, John Mallya na Paul Kipeja.
  
Licha ya kuwepo na ulinzi mkali wa jeshi la polisi uliowekwa katika barabara zote za kuelekea Mahakama Kuu, viongozi na wafuasi wa Chedema walifanikiwa kuvuka vizuizi hivyo.
  
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoka mahakamani jana jioni, Mbowe alisema sababu za kufunguliwa kwa kesi hiyo ni baada ya kuona demokrasia ya vyama vingi "inabakwa nchini."
  
Mbowe alisema watu wanne waliotajwa katika kesi hiyo ya madai ni Kamanda wa Polisi wilayani Geita, Kamanda wa Polisi wilayani Kahama, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa polisi (Makao Makuu) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
  
Alisema wadaiwa hao wamefunguliwa kesi kutokana na kukiuka Sheria ya Vyama vya Siasa nchini, kwa kuchukua maamuzi ambayo hayaendani na demokrasia.
  
“Tunaiomba mahakama itangaze amri ya jeshi la polisi ya kuzuia mikutano ya vyama vya siasa ni batili, utekelezaji unaofanywa ni batili, polisi wapewe tangazo la kutowanyanyasa wapinzani na pia itoe amri ya vyama vya siasa kufanya mikutano yake na polisi wawe walinzi wa mikutano hiyo,” alisema Mbowe.
  
Alisema pamoja na polisi kuwabana hawataondoka jijini Mwanza, na wataongezeka zaidi mpaka kieleweke.
  
Alisema upo mkakati wa makusudi kuhakikisha Chadema inafutika katika mikoa ya Kanda ya Ziwa kutokana na baadhi ya viongozi wake kutekwa na kunyanyaswa na polisi.
  
Mkutano huo na waandishi wa habari ulihudhuriwa pia na Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Saidi Issa Mohamed, Dk. Vincent Mashinji (Katibu Mkuu), Salum Mwalimu (Naibu Katibu Zanzibar), Halima Mdee (Mwenyekiti Bawacha) na Pastrobass Katambi (Mwenyekiti Bavicha) na baadhi ya wabunge wa chama hicho.
  
Kesi hiyo ya madai inatarajiwa kupangiwa Jaji Jumatatu ijayo.
  
Polisi ilisambaratisha mkutano wa Chadema uliokuwa ufanyike Kahama katikati ya wiki, ambapo mabomu ya machozi na magari ya 'washawasha' vilitumika kuondoa wafuasi wa chama hicho waliokuwa wasikilize hotuba za viongozi wa kitaifa.
  
Chadema imepanga kufanya mikutano nchi nzima kulaani inachodai uonevu unaofanywa dhidi ya wabunge wake Bungeni.
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Chadema hamna sera ni vurugu ti. Subirini uchaguzi mkuu au Mbowe rudi kwenye biashara zako

    ReplyDelete
  2. Hizo unazo zungumzia Ni djana zako potofu. Kwa ukijua jeshi letu la polisi kazi take Ni kulinda usalama. WA wanancchi Na Mali zao.. Na wewe unayejiita mwenye kiti WA Taifa ..taifa gani Hilo inaelizungumzia Na Kama tumeona dalili ya ku uruga Amani hjatutosita kuingia Na kuleta hali ya utulivu ambacho ndiyo kazi yetu wakati wowote Na mahali popote...na itabidi sisi wananchi. Na aerkali yetu tukufungulie mashtaka dhidi ya uhamasishaji wako wenue nia NA lengo la kuvuruga uutulivu WA nchi kwa ichu wako WA madaraka kwa kisingizio potofu cha Demolrasia ambayo pia maana yake huielewi ipasavyo...upo mbowe.. Issue yako inaeleweka ya Lai u not laivu Na posho. Baada ya kuona Hilo mafaanikio yake Ni madogo unaona bora ulete u hochezi haina ya serikali Na wananchi..tuakwambia hapo umechemsha Na tumeshakushtukia..hii Ni Tanzania mpya...HAPA Ni Kazi Tu

    ReplyDelete
  3. Chadema safari hiyo,, kama mmefikia hatua ya kuishitaki serikali au vyombo vya dola basi jua mnaikaribia ile sehemu wazungu huiita DESTINATION karibuni kijiweni siasa hazina mitihani mngesoma Fizikia au Kemia au Hisabati na kama masomo yote ni magumu kwa VILAZA kama nyie basi Jiografia au Historia mngesoma na kupata kazi Maktaba Kwani Siasa si kazi ndio kama hivyo mnataka kusikika wakati hamna point ni aibu tupu,,Poleni sana kwani mnaonekana kama mupo ONE FOOT IN THE GRAVE

    ReplyDelete
  4. ukawa ahamna akili nyinyi eti unaishitaki serikali mahakamani mbona hamuelewekinyie kasi inawatesa mbowe achana na siasa uziwezi hivi kwanini usirudi kwenye kazi yako mbona inakulipa sana unaropoka ropoka kama nini HAPA KAZI TU

    ReplyDelete
  5. ungua hata zikiwa miambili hizo kesi hazina maana yoyote ile mjinga mkubwa wewe

    ReplyDelete
  6. kWANI KATIKA SARAKASI HUWA WANAWEKA FIGISU FIGISU HUWA WANAWAITA CLOWNS... hII NDIYO STAGE ILIPOFIKA.. LEO MTU UNAJIITA (KAMA ULIVYOJIPA MAJINA) MMKITI WA TAIFA/ KAMBI LASMI YA UPINJANI... NA MENGINE MENGI... HII YOTE YA NINI SASA NASITAKI SELIKALI ... JAMANI SI SALAKASI NA CLOWNS TO ENTARTAIN THE AUDIENCE... CHA AJABU ITS FREE... FREEE.. SEMA TUMESAHAU KUWAJULISHA KUWA HATUNA FREE TIME AJILI HAPA NI KAZI TU.. CHINI YA MH. JPJM NA K. MAJALIWA.. SAMAHANI HATUTOHUDHURIA HAYA MAONESHO NA TAFADHALINI MJARIBU MIAKA IJAYO KAMA BADO MKO HAI.. TAFADHALI FIKISHA UJUMBE KWA WENZAKO... MBOWE UPO MWANANGU!!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad