CHADEMA Wataka Mkutano Mkuu wa CCM Kumkabidhi Uenyekiti Magufuli Nao Uzuiliwe

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetoa tamko zito kikitaka Polisi kuzuia Mkutano Mkuu wa CCM utakaofanyika mwezi ujao, vinginevyo watatumia nguvu ya umma kuuzuia.

CCM kimeitisha mkutano mkuu maalumu unaotarajiwa kufanyika Julai 23 mjini Dodoma, kwa lengo la Mwenyekiti wa chama hicho, Jakaya Kikwete kumkabidhi uongozi wa chama, Rais John Magufuli.

Kauli ya kutaka Polisi kuzuia mkutano huo kama inavyofanya kwa vyama vingine vya siasa, ilitolewa juzi mjini Moshi na Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), Julius Mwita.

Msimamo huo wa Chadema ambao uliungwa mkono na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Salum Mwalim unafuatia Polisi kuzuia mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu ambao ni wanachama wao.

Akizungumza na wanahabari, Mwita alikwenda mbali na kudai kuwa, Chadema watalifungulia Jeshi la Polisi kesi ya madai ya fidia kwa kuvuruga mahafali ya Chaso mjini Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita.

“Ukisoma barua yao wamesema wamezuia mikutano ya hadhara sasa kama wanakuja hadi kwenye vikao vya ndani, hatuwezi kuendelea kukubali jambo hili.Tumetumia busara sana,” alisema Mwita na kuongeza:

“Msipouzuia Mkutano Mkuu wa CCM Dodoma Julai 23 tunakuja kuuzuia sisi... yaani muwe tayari kusafiri kwenda Dodoma tukauzuie ule mkutano la sivyo, wauzuie kama walivyouzuia mikutano yetu.”

Mwita alimgeukia Mwalimu na kumweleza kuwa hiyo ni lugha ya ujana na inatekelezeka, akawahoji vijana wa Chaso waliokuwapo: “Wangapi mko tayari kuja Dodoma?” Wote wakaafiki.

“Intelijensia ya polisi ni ya kiumbea, inayoweza kujua tu Chadema wanakwenda kwenye mkutano, haiwezi kujua watu wamejificha wana bunduki na risasi 300 kwenye mawe kule Mwanza,” alidai.

Mwalimu alisema utaratibu wa Polisi na Serikali lazima ukome na kwamba wao ni viongozi.
Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Patamu hapa tunasuburi hii sinema ya bure
    Itakuwa chagulaga

    ReplyDelete
  2. Kama CCM watakuwa wanaongea yanayohusu chama chao na sio uchochezi au kutoa lugha za uchochezi waachwe waendelee na huo mkutano maana tunataka mkuu wa nchi apokee kijiti kama katiba yao inavyosema,lakini kama nao wataanza kuchambua mambo ya vyama pinzani na kukosoa mambo ya UKAWA,hatua kali dhidi yao ichukuliwe.

    ReplyDelete
    Replies
    1. kweli mdau,tatizo la ukawa wanadhani wanaonewa au hawatendewi haki wakati wote na jeshi la polisi,kumbe kuna wakati matatizo na jeshi la polisi wanasababisha wenyewe.Mfano wanasema wanaenda kwenye mahafali la kushangaza wanaleta mambo ya kampeni,kusemea lugha mbovu na uchochezi kana kwamba hawajui kama kuna watu wako kazini na yote wanayongea yatapelekwa kunakohusika.Ni makusudi na ni chokochoko.Eti mnaonewa mbona tuko wengi vyama pinzani mbona hatufanyi/hatufanyiwi hivyo?Vijana tuacheni na tusikubali kutumiwa.

      Delete
    2. We gala kuma

      Delete
  3. Hivi hawa Ukawa kwani vipi??? Mkutano Mkuu wa CCM sio Mkutano wa Hadhara hivi hawaelewi lolote hawa
    Kinachozuiliwa ni mikutano ya hadhara na siyo ya viongozi wa vyama na si kuhamasisha uchochezi ati tunataka kuishtaki serikali kwa wanachi ni utumbo gani huo???
    Kwenye Mkutano mkuu waalikwa siyo sisi wa bodaboda wala wakulima ni wajumbe na wawakilishi wa CCM

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad