Baba Mzazi wa Diamond Platnumz |
“Msongo wa mawazo ni tatizo kubwa duniani linalotokana na kusheheni kwa mawazo ya kila wakati, husasan kuhusu maisha au afya. Kwa hiyo anachofanya Diamond kwa baba yake ni sawa na kumuua kwa sababu ya kumsababishia msongo,” ndivyo alivyosema daktari Rweyemamu wa hospitali moja ya jijini Dar.
Daktari Rweyemamu alizungumza na Amani hivi karibuni kufuatia habari zinazoandikwa na Magazeti Pendwa ya Global Publishers kuhusu nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwamba amemtelekeza baba yake, Abdul Juma.
AZUNGUMZIA HISTORIA
“Nimekuwa nikisoma habari mbalimbali kwenye Magazeti Pendwa ya Global, lakini hili la Diamond kumtelekeza baba yake mimi naona lina mapana yake. Najua utetezi wa Diamond ni kwamba, baba alimtelekeza mama yake (Sanura Kasim) yeye akiwa mtoto.
“Kwa hiyo malezi yote, ameyapata kwa mama mpaka kufika kwenye kiwango cha mafanikio. Lakini pia nimewahi kusoma kwamba, baba aliomba msamaha yaishe, atambulike kama baba lakini mtoto akagoma.”
MAGONJWA YA BABA
“Kuna wakati nikasoma kwamba, yule mzee anasumbuliwa na miguu, mara sijui ugonjwa wa kansa ya ngozi. Pia amekuwa mtu wa kuumwa mara kwa mara.”
MSONGO WA MAWAZO NI CHANZO
“Yule mzee atakuwa na magonjwa mengi, hasa yanayotokana na msongo wa mawazo. Mawazo yake kwa sasa ni kitendo cha kuona mafanikio ya mwanaye akilinganisha na maisha yake magumu bila msaada.
“Binadamu yeyote, anapomwona mtu wake wa karibu amefanikiwa na yeye hali duni lakini huyo aliyefanikiwa anaweza kumsaidia yeye akaondokana na hali duni, lazima asumbuliwe na msongo.”
MIGOGORO, UGUMU WA MAISHA
“Lakini pia migogoro inayotokea katika familia, ni moja kati ya sababu zinazoweza kumpa mtu msongo wa mawazo, hasa pale ambapo utaichukulia ‘serious’ kwa kuwa inagusa moja kwa moja maisha yake. Ugumu wa maisha unachangia pia.”
MWILI UNAVYOATHIRIWA NA MSONGO
“Moja ya sababu ambazo zinachangia kwa kiasi kikubwa kuzorota kwa afya na kusababisha vifo vingi ni msongo wa mawazo. Mwili unavyokutana na hali tofauti aidha kitu cha kutisha au kinacholeta mawazo ndani ya muda mfupi na tofauti hiyo ikashindwa kutambuliwa haraka na ubongo mfano pale unapokutana na jambo usilolitegemea, basi mwili hutoa kichocheo kinachoitwa cortisol ambacho kinamwagwa kwenye damu ili kuuandaa mwili aidha kupigana au kukikimbia kitu hicho.
“Mapigo ya moyo huongezeka, mapafu huchukua kiwango kikubwa cha hewa na mzunguko wa damu pia huongezeka na baadhi ya sehemu za kinga huzidiwa na mzigo mkubwa hivyo kutoa nafasi kwa viumbe adui kuushambulia mwili kirahisi.
“Msongo wa mawazo unapokuwa mkubwa siku hadi siku ndipo kinga ya mwili inavyozidi kushindwa kubaini uwepo wa kichocheo cha cortisol, msongo unapunguza makali ya kinga ya mwili, hivyo matatizo ya afya huongezeka.”
UTAFITI
“Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na World Health Organization, Shirika la Afya Duniani ‘WHO’, maradhi ya moyo, akili, ugumba, ukosefu wa nguvu za kiume na vidonda vya tumbo, pia yanacha-ngiwa na msongo wa mawazo.”
LAZIMA BABA DIAMOND AWE HIVI
Kwa mujibu wa daktari huyo, lazima baba Diamond wa sasa atakuwa amebadilika tabia, kwamba atakuwa mpole na siyo mwenye furaha kwa muda mwingi.
“Kuishi kwa kubangaiza pesa za kula huku akiwa anajua mwanaye anazo, tena mpaka zinamzidia, baba Diamond atakuwa anamalizika polepole. Lazima kila akiamka, anasema; ‘mateso yote haya, mwanangu yupo lakini hataki kunisaidia.”
WITO WAKE KWA DIAMOND
Daktari huyo alisema kuwa, anamtaka Diamond kurejesha moyo wake nyuma, amtunze baba yake ili amuokoe na kumalizika.
“Namtaka Diamond ajue kuwa, anachomfanyia baba yake ni kumuua bila yeye kujua. Ukuta anaomuwekea katika usaidizi unamfanya mzee huyo kunyemelewa na magonjwa ya moyo na vidonda vya tumbo ambavyo kwa mazingira ya maisha yake yanaweza kumsumbua kwani yanahitaji kipato kizuri.
Chanzo:Global Publishers
Dogo haijui laana ya mzazi. Pia ni kosa kuingilia ugomvi wa wazazi.
ReplyDeleteHaingilii ugovi wa wazazi bali analipa jinsi aliyo mtelekeza bila kumjali kwa maradhi,mavazi,chakula, Elim, kwani yeye mtto alikuwa anakosa gani? Mpaka amfanyie ukatili huo?
DeleteLeo ndo anakumbuka ana mtto?
Je angekufa kutokana na kukosa maleze mema ange muomba nani msaada?
Mi naona Daimond yuko sawa mwanaume wengi wanatabia ya kuwasusa watto na kuwaachia kina mama wakihangaika sn pindi wanapopata mafanikio ktk maisha hujitokeza na kuomba samahani za kinafik tu
Hiyo ndo fundisho la wanaume wote wanaotelekeza watto wao
Kama mtoto ameshapata ufahamu,hana sababu ya kutomsaidia baba hata kama yeye hakumjali akiwa mdogo.Ukiwa na hofu ya Mungu lazima utajua kusamehe,maana Mungu katuagiza kusameheana.Kama ni Mungu kampa Daimond basi iwe msaada kwa wengine,kama amevipata kwa njia za kishetani na asimamie msimamo wako wa kutomsamehe wa kutomsaidia mzee wako.
DeleteNI KWELI WANAUME WANATELEKEZA WATOTO WAKIPATA MAFANIKIO NDIO WANAJITIA MWANANGU MWANANGU!!!! HILI NI FUNDISHO. TENA NAMSHAURI AACHE KUMSEMA SEMA DIAMOND ANAVUNA ALICHOPANDA
DeleteHAKUNA LAANA KATIKA HILI.
Deleteyou said well Salama, wanaachaga wanawake na wtoto wakipata shida na wao wakiendelea na vimada vyao, kwahiyo hata vitabu vyadini vinasema mtu wakwanza kumsamini na mtuze ni mama yako, so he is doing just fine, bi Sandra ndio anahaki ya kutunzwa na huyu mtoto na iwe fundisho kwa wanaume wengine huko nje, maana unapotesa mtoto huwezi jua takuja kuwa nani katika misha yake. haukuwa kwenye maisha yangu i can careless about yours.
DeleteBwana hili zee linavuna lilichopanda, huwezi panda mahindi ukavuna mpunga, mond Kula Bata na mama adi kuku walalamike bandani. Angekua achokile angemfuata Hana lolote, hapo hakuna laana kwa mond laana Ni hiyo anayoipata huyo mzee sahizi. Laana Ya kutelekeza kiumbe kisicho na hatia. Na ole wenu nyie mliotelekeza vizazi vyenu kwa madai mtoto kwa Baba hapotei atakuja Tu akiwa mkubwa. Fundisho hilo
DeleteMsipende kutetea ujinga mzazi atabaki kuwa mzazi tu labda kama hamna hofu ya Mungu .Ukweli chanzo huwa ni wanawake wenyewe mnamkataza mzazi mwenzenu asimuone wala kumjulia hali mwanawe alafu mnapandikiza chuki kwa mtoto kuwa eti baba yako hakutaki kumbe ni uongo na mnafanyaga hivyo mnapoona MWANAUME UNAMPENDA LKN Yeye hakupendi na kaamua kuoa tena so ndo mnaamua kujenga chuki kwa mtoto ili am,chukie baba yake kumbe hakuna lolote ni kwa chuki zenu tu
Deleteugonvi wa baba na mama mtoto hustahili kuingilia hata kidogo kwani vitu utashindwa kuambiwa so jaribu kuwa mtazamo mpya kila siku kisasi hata siku moja hakitatui tatizo ila kinaongeza tatizo kumbuka hata kama unapesa bila maelewano wazazi wako ni zero.machon pa watu anaonekana ana furaha but in heart hana furaha
Deletewatu bwana eti kavipata kwa njia ya ushetani. Hapohapo mtu anasema amsaidie baba yake mbona hueleweki? km ni vya ushetani akimpa baba yake naye si atakuwa amevitumia vya kishetani acheni hizo kijana anajituma na mnaona
DeleteHivi angekuwa ansukuma guta haya yote yangesemwa??????
ReplyDeleteKWELI KABISA MDAU!!
Deleteyeye anaona diamond anamuonea alivyomtelekeza aliona sawa mie hata sioni shida anavyofanya kwani huyu mama lazima aliteseka na wanae sana
ReplyDeletehuyu dactari sikubaliani naye kwani mama yake diamond mbona hakufa alivyoachWA wahangaike bila msaada wowote wakati yeye ana hela? tena alikiri mwenyewe kwenye tivii kuwa alikuwa na hela sana. lakini hakuitunza familia yake?? JAMANI ACHANI UCHONGANISHI!!!
ReplyDeleteANGALIENI MANENO YA MWENYEZI MUNGU SIO YA BINADAMU,MAANA KUNA SIKU YA KUNYAMAZA KIMYA NA YOTE YATAPITA BALI YA MUNGU HATAPITI.HUYU DAI KWA SASA NI WA KUMUACHA MAANA HAYUKO KIKANISA WALA KIMSIKITI.MBAYA ZAIDI HATA WATU WAKE WA KARIBU HAKUNA ANAEMSHAURI,SI MAMA,WALA MZAZI MWENZIE.BORA YA WEMA ALISHAMSHAWISHI KWENDA KWA BABA NA WAKAENDA KUMUONA, LAKINI ZARI SIJASIKIA HATA.
ReplyDeleteDunia bana! Muanzaji uwa ahonekani siku zote ila mmaliziaji ndoo huonekana, Malipo kila siku ni hapa chini!...tutavuna tulichopanda....tumeambiwa mtoto ni malaika wa mungu!....kumsaidia au kutomsaidia ni nafsi yake D...non sense..
ReplyDelete------------------
ReplyDeleteukipanda matembele utavuna matembelee........
ReplyDeletenawchukia sana wanaume wa dizaini ya huyu baba!!!!!
ReplyDeleteHII NI DUNIA,NA DUNIA NI KIGEUGEU,TUPO MTASIKIA TU.
ReplyDeleteHIVI DIAMOND ANGEKUWA MPIGA DEBE BABA ANGEWEZA KUFA KWA MSONGO WA MAWAZO?????????
ReplyDeleteHASWA DACTARI JIBU HILI SWALI!!!!
DeleteMAMA KULA KWA RAHA ZAKO!!!
ReplyDeleteNYIE BINADAMU HACHENI UCHONGANISHI !!!
ReplyDelete