Diamond Platnumz Kwa Hili la Baba yake Mzazi Hana Washauri?

Katika hili la mzazi wake wa kiume mimi binafsi limenigusa hasa kwa imani yangu ya dini. Siwezi kuhukumu moja kwa moja kwa maana sijui chanzo cha ugomvi wao wala status yao kwa sasa na pia MIMI SI HAKIMU, lakini nina haki ya kutoa maoni yangu hasa kumsaidia pia diamond ajitambue.

Katika hali ya kawaidia inatakiwa ingekuwa rahisi kama mzazi wako anapata msaada wako by then kila siku awe analalamika au tunamuona kwenye mitandao huo tayar ni udhaifu wako wewe mtoto kwa kuruhusu mzazi wako awe anakutia aibu wewe au familia yenu kwa ujumla. Kwa namna yoyote ni lazima suala la wazazi wako ukalipa umuhimu mkubwa sana katika maisha yako.

Katika mafundisho ya dini yanatufunza nini kuhusu wazazi?

Hakika ametakasika yule ambaye amewajibisha na kuamrisha wema na kutimiza haqqi na kuiegemeza kwa kila anaestahiki na akawajibisha haki kwa wazazi wawili, na ikawa ni amri iliyoenea kwa walimwengu wote. Hakika ameamrisha ALLAH tabaaraka wata’la katika aya nyingi kuwafanyia wema na ihsani wazazi wawili.
Mfano wa kauli yake aliposema:

Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa hishima. Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma. Na useme: Mola wangu Mlezi! Warehemu kama walivyo nilea utotoni.

Akaamrisha ALLAH tabaaraka wata’la ihsani kwa wazazi wawili katika namna zote za wema, nao ni katika kauli [unapozungumza nao] pale aliposema [basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa hishima]. Vivyo hivyo kuwafanyia wema katika matendo; kimwili na kimali kwa kauli yake aliposema: (Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma).
Na akanyanyua ubora wanapofika katika hali ya uzee, kisha akakataza kuwavunjia adabu na kuwatusi, achilia mbali kuwaacha wakiteseka.

UWAJIBU WA KUWAFANYIA WEMA WAZAZI WAWILI:

Hakika ameamrisha Allah tabaaraka wata’la, na akawajibisha kwa njia ya wasia kuwafanyia wema wazazi wawili katika aya nyingi za qur’an. Pale ilipokuja amri ya wazi juu ya kuwatii, aliposema:
وَوَصَّيْنَا الْإِنسَانَ بِوَالِدَيْهِ إِحْسَاناً
Na tumemuusia mwanadamu awatendee wema wazazi wake wawili[1]

Ikaonesha wazi kuwa kuwafanyia wema wazazi wawili ni jambo la wajibu kwa kuwa ni wasia wa Allah kwetu. Bali akaliambatanisha jambo hilo la kuwafanyia wema wazazi wawili na twaa’ yake Allah tabaaraka wata’la pale aliposema:

وَقَضَى رَبُّكَ أَلاَّ تَعْبُدُواْ إِلاَّ إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَاناً
Na mola wako mlezi ameamrisha kuwa msimuabudie yeyote isipokuwa yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema.[2]

Na kauli yake aliposema:
وَاعْبُدُواْ اللّهَ وَلاَ تُشْرِكُواْ بِهِ شَيْئاً وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَاناً
Na mwabudieni Allah wala msimshirikishe na chochote, na muwafanyie wema wazazi wawili.[3]

Zikakusanya aya mbili hizi kuwa kufanyiwa wema wazazi wawili ni haqqi yao, bali akaifafanya haki hiyo kuwa ni ya pili baada ya tawheed yake Allah tabaaraka wata’la akionesha ukubwa wa jambo hilo [la kuwafanyia wema].

Amesema Al qurtwubiy [Allah amrehemu], kauli ya Allah “Na wazazi wawili kuwafanyia wema [ihsani]” maana yake ni:
برهما وحفظهما وصيانتهما وامتثال أوامرهما

Kuwafanyia wema na kuwahifadhi, kuwatunza na kutekeleza amri zao.

Katika kulisisitiza hilo, mpaka ikawa [wema kwa wazazi wawili] ni wenye kutangulizwa mbele hata kabla ya Sunnah za kujitolea kama vile Sunnah za kabla ya swala nk. Na kwa hili akaweka imamu muslim [Allah amrehemu] mlango katika swahih yake akiuita:
باب تقديم بر الوالدين على التطوع بالصلاة وغيرها

By the way mimi nimekubusha tu. Kama ni kweli mzazi hapati msaada basi ajitahidi kumsamehe, kama anapata msaada ila ndio umaarufu basi Diamond anisemehe maana binadamu tumeumbwa kukOsea. Na huu ni mwezi wa toba hakika atakuwa amenisamehe.

Asante.

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mwandishi umenigusa hata mimi.
    Daimond anadhani hatakufa,hataugua,au hizo mali alizo nazo atazikwa nazo akafaidi na huko baada ya kuzikwa?Kwa hapa hata kama unatoa sadaka kwa yatima/walemavu kama humsaidii mzazi wako ambaye amakuomba muyamalize sidhani kama kuna uhalali.

    ReplyDelete
  2. Dimond hakuna mkamilifu, samehe na sahau,fanya maishayawe mepesi,muangalie na babako, usidanganyike kumtupa, madem unawasamehe why c baba.utachekwa

    ReplyDelete
  3. MZAZI ni mzazi tu , bwana dayamondi inabidi usamehe tu

    ReplyDelete
  4. Mwandishi wewe ni mchochezi unagombanisha watu hapa tangu rais, TULIA ,wabunge
    Nashangaa hujakamatwa

    ReplyDelete
  5. Anafunga nini wakati baba yake mzazi anaangaika? Pili me pia ni mwanamke ila nawashauri wanawake wenzangu tusimwage sumu kwa watoto wetu juu ya baba zao hata Kama alikukosea mfundishe mwanao kusamehe hivi watoto wote tuliotelekezwa tukifikia hatua kama ya diamond na maneno ya Mungu tunakua tumeyasahau tutashika maneno na mawazo ya Mama zetu tu.diamond uwezi jua hao wazazi walitofautiana wapi hakuna wa kukueleza ukweli awe Mama au baba. sawa ulipata shida na Mama yko lakini Mungu kawafuta machozi inabidi umsaidie baba yko ili nafsi yake imsute.

    ReplyDelete
  6. Labda kazaliwa nje ya ndoa na dini ya kiislam inasema mtoto wa namna hiyo ni wa mama baba haruhusiwi kumlithi mtoto na mtoto pia hamlithi baba kama kazaliwa ndani ya ndoa anafanya dhambi kutomsaidia mzazi wake

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad