Ni ukweli usio pingika kuna muziki fulani uliokuwa umezoeleka ndio unatakiwa kupigwa radioni na hii ilikuwa ni uniform za Radio zote kana kwamba ilikuwa ni sheria ambayo imewekwa!
ilikuwa ni vigumu na hakuna uthubutu wa miziki ya mnanda ,visingeli na mchiriku kusikia ukipigwa radioni na sio kwamba hauna mashabiki bali una mashabiki wengi sana sema radio muda mwingine hulazimisha walaji kula hata wasicho kitaka!
Dj Majizzo baada ya kuanzisha kutuo cha E-FM imekuwa kama mkombozi wa miziki yetu ya asili na wamekuwa wakiupa muda wa kutosha kuupromote kiasi kwamba hata walio kuwa hawajui uzuri wake sasa wanaelewa!
Mimi sikuwa mshabiki wa miziki wa namna hii lakini sasa nimekuwa kama teja maana kwakweli nyimbo hizi kuna zenye jumbe nzuri sana kiasi kwamba ukisikiliza una hamasika hakika!
Kupitia DJ majizzo (E-FM) leo hii sasa nyimbo za mnanda,mchiriku na singeli zimeanza kusikika kwenye radio nyingine na wasanii hao wanapata showa kitu ambacho hakikutegemewa!
Leo hii ukisikiliza East africa radio utasikia wakipiga nyimbo hizi na hata Clouds na kwenye matamasha tunaona wasanii wa minanda,mchiriku na visingeli wanapewa show tofauti za zamani wale wa bongo fleva ndio walikuwa wanakula hela peke yao!
Ni wazi kabisa Wasanii wa minanda ,mchiriku na visingeli wanapaswa kumshukuru Majizzo kwani amechangia sana kwenye mafanikio yao na mapinduzi yao!
Mimi nimshukuru tuu Majizzo kwa kuwasaidia vijana hawa na kuupa thamani mziki wao!