Gardner: Jide Kitu Gani Bana!, Huyu Ndiye Mwendokasi Wangu Kwa Sasa


Miezi michache baada ya wanandoa Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ na Gardner Gabriel Fikirini Habash kutalikiana kwenye Mahakama ya Mwanzo Manzese Sinza jijini Dar, mwanaume huyo amemuanika ‘mtu wake’ wa sasa a.ka. ‘mwendokasi’ akisema ndiye mrithi wa mikoba ya mwimbaji huyo nyota wa Muziki wa Kizazi Kipya.

Katika Viwanja vya Escape One, Kawe, jijini Dar es Salaam Jumamosi iliyopita, ambako mwimbaji mahiri wa Muziki wa Dansi Bongo, Christian Bella alikuwa akifanya shoo ya kutimiza miaka 10 katika ‘game’, Gardner alionekana na mrembo huyo akizunguka naye kimahaba kutoka eneo moja kwenda lingine huku wadau wake wakihoji ni nani!

Garder alipohojiwa na mwandishi wa habari hizi alikiri kuwa ni kweli kwa sasa anamiliki kifaa kipya kinachokwenda kwa jina la Vestina.

“Yes! Ndiye huyo kaka. Huyo ndiye mtu wangu kwa sasa na kama nilivyowahi kukudokeza, nimekuwa naye kwa muda mrefu kidogo, lakini sikuweza kumwanika mapema kwa sababu zinazoeleweka au ninazozijua mwenyewe,” alisema Gardner.

Mwandishi: “Vipi kuhusu Jide sasa, ndiyo n’tolee moja kwa moja kwa sababu ya talaka?”

Gardner: “Jide kitu gani bwana? Huyo ndo’ mwendokasi wangu kwa sasa.”

Gardner alimtaja binti huyo aliyekataa kusema umri wake kuwa anaitwa Vestina Jax, mkazi wa jijini Dar es Salaam.

Mwandishi wa habari hizi alilitaka kufahamu kama kuna mipango yoyote ya kufunga ndoa katika siku za karibuni baina yake na mrembo huyo, lakini Gardner alikataa kusema lolote juu ya hilo.

“Duu! Acha basi kaka! Kwa hilo sina comment,” alisema mtangazaji huyo ingawa habari za ndani zaidi zinasema kuwa, mrembo huyo ndiye mkewe mratajiwa.
Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. tunashukuru kama amempata cha pombe mwenzie hapo mirembe. NDINDINDI

    ReplyDelete
  2. Ndoa ya 3?
    Hata wakati wanaanzana na Jide tuliambiwa hayo maneno.
    Kila la heri.

    ReplyDelete
  3. gadner chapombe

    ReplyDelete
  4. Huyu G si ana binti mkubwa tuu, anamfundisha nini kwa haya anayoyafanya? vp maisha yanamwendeaje au amejikalisha? naona kama anaelekea kubaya na kiangalia umri unaenda. Kuna kesho G, utashangaa hao unaosema ndiyo mwendo kasi wako watakukana na utaonekana TOYI.

    ReplyDelete
    Replies
    1. G hana mwelekeo,kinachoonekana alishikiwa akili na Jide,hivi mtu na akili yako ukope pesa ununue gari la bei mbaya(kifahari) wakati hata pa kuweka ubavu huna?AKLI?MATOPE?

      Delete
  5. anaitwa nani huyu? Gardiner umekuwa cha pombe mpaka unaokota akina Gigi Money wewe ni cha pombe mpaka unaokota huyo hapo Gardiner wewe ni cha pombe, wewe ni cha pombe haswa bila kusingiziwa, hehe

    ReplyDelete
  6. Gardiner tunaelewa wewe ni chapombe lakini pia umekuwa kipofu huoni, yaani huyo mwanamke uliyepiga naye picha hapo juu jinsi alivyo na sura mbaya na kujionesha nae mbele zawatu halafu unamwita mwendo kasi, ngoja nicheke kwanza , he he, du pole saana mzee

    ReplyDelete
  7. Wengine wanaseme G chapombe,wengine mwanamke ana sura mbaya kwan tatizo ni nn kama chapombe si yy,kama huyo mwanamke ana sura mbaya si kampenda yy,nyinyi inawahusu nn mwachen na maisha yake.....ndo maana wabongo hatuendelei kazi kuwasema wengine wakati yetu yanatushinda

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad