Hatma ya Kesi ya Chadema Dhidi ya Polisi Kuzuia Mikutano ya Kisiasa Kujulikana Jumatatu June 21

Hatima ya shauri lililofunguliwa na Chadema dhidi ya Polisi kupinga amri ya kupiga marufuku maandamano na mikutano ya kisiasa itajulikana Juni 21, Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza itakapotoa uamuzi kuhusu pingamizi lililowasilishwa na upande wa utetezi kuomba litupiliwe mbali.

Jaji Mohamed Gwae anayesikiliza shauri hilo, alifikia uamuzi huo baada ya kusikiliza hoja za mawakili wa pande zote za utetezi na mleta maombi.

Awali, Mawakili wa utetezi, Robert Kidando na Obadia Kajungu waliomba Mahakama kutupilia mbali maombi ya Chadema kuruhusiwa kufungua kesi yaliyowasilishwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, kwa madai kuwa hayajakidhi mahitaji ya kisheria.

Akifafanua, Wakili Kidando alidai mleta maombi hajataja baadhi ya vifungu muhimu ikiwamo kifungu cha 5(1)(2), vinavyoipa Mahakama mamlaka ya kisheria kusikiliza na kuamua maombi hayo.

Madai hayo yalipingwa na mawakili wa Chadema; Gasper Mwanaliela na John Mallya waliodai hoja za wajibu maombi hazina uhalali kisheria kwa sababu hati ya maombi yaliyopo mbele ya Mahakama yamekidhi mahitaji ya kisheria.

Wakili Mallya alidai kisheria, hati ya maombi inapaswa kuwa na vitu vitatu muhimu; hati ya kiapo, maelezo ya mleta maombi na ombi la shauri kusikilizwa kama inavyoelekezwa na kifungu cha 5(3).

Wakili Mallya aliomba Mahakama kutupilia mbali pingamizi la upande wa utetezi na kumpa nafuu mleta maombi, kesi yake kusikilizwa na kuamuliwa.

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote, Jaji Gwae aliahirisha shauri hilo hadi Juni 21, Mahakama itakapotoa uamuzi huku akiuagiza upande wa utetezi kuwasilisha hati kinzani kujibu hoja za mleta maombi.

Katika maombi ya msingi, Chadema inaomba Mahakama kutamka kuwa amri ya polisi na utekelezaji wake ni batili, kwa sababu ni kinyume cha katiba na sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mbowe Mbowe Mbowe... Maombi ya msigi " Chadema inaomba mahakama kutamka kuwa Amri ya Polisi na Utekeleza wake ni Batili" Haya ndiyo unachoomba... ili iweje na unataka kudhihirisha nini? na una lengo la kumuelewesha nani? na itakusaidia nini zaidi ya uchochezi... halafu unasema Demoklasia / Haki ya kusema... Kama huku ndiyo kusema na lawama zilizojifika na chokochoko ya uhamasishaji uliojificha.. Nakwambia wewe siyo mwenye nia nzuri na uliye jaaa Uchu na Tamaa ya Madaraka ambayo hutoyafikia.. inatosha unayoyafanya na ukasikilizwa na watu wenye mwelekeo kama wewe kuishia katika Vibaraza vya Bunge ambavyo tulitegemea kuwa utakuwa mshiraka katika Kuleta hoja zenye Vichwa na Miguu ,... hatima yake umekuwa ni Uchwara kama walivyo wengine waliojaa duku duku na Chuki kwa wenzao... Badilika uingie katika ujenzi ya Taifa letu.... Mungu ibariki Tanzania na Watanzania wenye uzalendo na wapenda Amani na Usalama...Hapa Kazi tu.

    ReplyDelete
  2. Kumpa nafuuu mleta maombi!!! Hatuna Discount katika sheria...Hukukamilisha Vipengele husika tukupe nafuu... Nadhani uanasheria wako unadosari... Mahkama inafata wajibu wake... Tarehe mmeshapewa na tunangoja Uamuzi... Inasikitisha ukiangalia ombi lenu la msingi!! Mnacho taka ni Kauli tu!! Ama kweli siasa bila kisomo inakuwa ni malumbano tu... Halafu unadiriki kujiita mwana sasa.. uliye kosa upeo na uelewa wa sasa Hapa kazi tu... Pole Mbowe!! Umeshaanza kuingia bungeni au bado??

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad