Kitendo cha wabunge wa Ukawa kutoka nje ya ukumbi wa bunge kilianza kama masikhara wengi tukidhani kisingeenda zaidi ya wiki moja, lakini kadri siku zinavyoenda kinazidi kuchora picha mbaya na kuweka msitari wa mpaka wa uadui kati ya wabunge wa kambi ya CCM na Ukawa.
Inavyoonekana hali hii itaenda zaidi ya hapo, itasogea mpaka kwa wananchi kama ilivyo kule kisiwani Pemba.
Kinachonisikitisha ni kule kukaa kimya kwa viongozi wetu wastaafu, mzee Ali Hassan Mwinyi na Ben Mkapa na hata mheshimiwa Rais ambaye ndiye tuliyemkabidhi ubaba wa taifa hili na ulinzi na usalama wetu kwa kipindi cha miaka mitano tuliyo nayo. Yaani wako kimya kama kwamba kinachoendelea bungeni hakiwahusu na hawakioni kama ni kitendo kinacholichafua na kulitia aibu taifa letu kimataifa.
Nawaomba wazee wetu mjitokeze na mseme neno juu ya hiki kinachoendelea bungeni, hivi tunawatunza kwa kodi yetu ili mle tu na kuwa wageni wa heshima kwenye makongamano lakini msilisaidie taifa hata pale mnapoona mambo yanaenda ndivyo sivyo. Mbona mwaka 1994 mwalimu aliingilia kati alipoona wabunge wa kundi la G55 wa bunge la JMT linapigania kuanzisha serikali ya Tanganyika ndani muungano.
Wazee wetu jitutumueni mliokoe taifa hili bado mkingali hai lisiparaganyike mkiwa mnaangalia kama kwamba ni jambo lisilowahusu.
Hivi kweli Rais Wetu Huguswi na Wabunge wa Upinzani Kutoka Bungeni?
10
June 21, 2016
Tags
Hili nalo neno watanzania
ReplyDeleteTusishangilie tu
Watapuuzwa hata kwa miaka mitano yote na hawatakuja kurudi mjengoni acha wapate huo mtaji wao kwa sasa kwani ukiongea nao ni kama unawabembeleza
ReplyDeleteKudharauliwa au kupuuzwa kunauma sana kuliko kipigo halisi na mwandishi unaonekana umeguswa sana na habari ya hawa WAKAWA vipi??
Aguswe na kitu gan!??? Wanaopaswa kuguswa ni wale wananchi wanaowawakilisha. Poleni sana wananchi kwa kuwachagua wawakilishi vilaza na vihiyo.
ReplyDeleteAcha habar za ujinga. Hao wabung waupinzan hawan lolot. Kwa nini rais azungumzie? hawan sabab yoyot ambao inawez tuma rais anazungumzia.
ReplyDeleteKaeni na dharau zetu iko siku mtawaona watu
ReplyDeleteHistoria haifutiki
Ukweli tulipoteza nguvu zetu kuwapa kura zetu ukawa. Lakini tatzo lipo kwetu tulowapa kura kwani wao hawana tatizo posho wanapata kila cku c wanaingia kusaini na kutoka na kiinua mgongo hizo m200 c watapata. Ingawa wanasahau posho ni pesa zetu masikini tulowatuma kwa kuwaamini.wanakula pesa ya masikini bila kuifanyia kazi.najiuliza mtagoma mpaka lini hao ccm wanabaki wanatetea wapiga kura wao,lakini wetu mnagoma mnamkomoa Nani rais? Wabunge wa ccm? Au cc tuloamka sa kumi kwenda kuwapigia Kura? Hakuna mtu mwenye uchungu na mwananchi masikini mnaangalia maslai yenu ila kumbukeni 2020 c mbali kabisa. Mungu tusaidie afya njema.
ReplyDeleteHawa wabunge wa UKAKWA wamepoteza mwelekeo. Great thinker wao wamempoteza I mean Dr. Slaa. Wamebakiza akina Mbowe wenye uwezo wa mob psychology na kuandamanisha watu. Sasa anguko takatifu linawakuta muda si mrefu. Kam ni mkenge wameuvaa. Wanaendesha siasa za kutafuta sympathy za wananchi, sasa wananchi wamejitambua wamewapotezea. Kweli waqnaisoma kuanzia Bungeni hadi mtaani
ReplyDeletePoleni sana kwa kukosa Strategist
halafu wakishamgusam inakuwaje?
ReplyDeleteSi rais wala mtu mwingine yeyote wa kuzungumza na wabunge wa ukawa bali constituency zao. Wapiga kura katika majimbo yao wanatakiwa kuwakumbusha wajibu wao kwa majimbo hayo.
ReplyDeleteMimi ni mtanzania mkazi wa Austalia kwa muda wa miaka 34
Hapa Australia kila chama kinapokuwa madarakani spika hupendelea wabunge wa chama chake iwe Labour Party au muungano wa vyama vya Liberal and National Parties.
Kwa mfano spika wa bunge lililopita (sasa hivi tuko kwenye campaign ya uchaguzi mwezi ujao) kutoka Liberal Party aliweka rekodi ya kuwaadhibu na kuwafukuza wabunge wa upinzani (Labour Party) bungeni.
Jambo hilo lilijulikana wazi wafuatiliaji wa siasa na vyombo vya habari vilizungumzia jambo hilo,
Wabunge wa upinzani (Labour Party) waliendelea na shughuli zao bungeni kama kawaida, hiyo ndiyo demokrasia kwa vile walitambua kwamba hawana namba za kushindana na chama tawala na sababu yenyewe ni kwamba wananchi waliwaamini chama tawala kuliongoza bunge. Uchaguzi umefika sasa hivi wanayo nafasi nyingine ya kuwa convince wananchi waweze kuwapa nafasi ya kulisimamia bunge.
Ukawa wapende, wasipende, bunge linasimamiwa na chama kilicho na wawakilishi wengi kupitia spika waliemchagua.
Miswada mingi ya upinzani huwa haipitishwi kwa sababu hawana namba za kushindana na wabunge wa chama tawala.
Kazi kubwa waifanyayo wapinzani ni kutoa mapendekezo ya masahihisho ya miswada ya chama tawala ikiwa ina kasoro kabla ya kupitishwa au hujiunga na wabunge wenzao wa chama tawala kujenga hoja za miswada yao ili iweze kupitishwa.
Sasa basi ikiwa wanaamini miswada yao ilikuwa mizuri na imezuiliwa au mapendekezo yao ya mabadiliko kwenye miswada ya chama tawala kikatupilia mbali basi ni kusubiri uchaguzi ujao kufikisha malalamiko kwa wapiga kura.
Mhe,rais hana haja ya kuingilia masuala ya wabunge, so far anafahamu fika kinachofanyika na UKAWA,siyo kwa bahati mbaya bali ni mikakati ya kumfanya yeye aongoze kwa shida na taabu. Anafahamika anayewaambia wafanye hivyo, hivi unafikiri wazee hasa marais wastaafu na watu maarufu hawajui kinachoendelea? wanajua na wanataka kujua mwisho wao. Nchi hii wameikuta na amani yake ambayo haikuja kama mvua ilitengenezwa kwa kipindi kirefu, wao kwa tamaa zao wanataka kuiharibu maksudi kwa sababu za kitoto. Kweli nawaambia hakuna atakaye kubali watu wenye hila na ghiriba na pia uroho wa madaraka kuchafua amani yetu, cha mtema kuni watakiona kwa sababu nchi hii ni ya kwetu wote na hakuna kwa sababu za kitoto atuharibie amani yetu, ataanza yeye na kundi lake na nchi itasonga mbele. Fanyeni siasa na siyo fitna na hila, Dr Maghufuli anayo mambo mengi ya kufanya na hasa sula la ulinzi na uchumi wa nchi kuakikisha wananchi wanaishi salama ikiwa ni pamoja na UKAWA. Aliyoyasema Maalim Seif akiwa Marekani yanafahamika kwa watanzania wote. Difenetely ni makubaliano yao ya kuwa zanzibar kusikalike na Bara hivyohivyo. Ila onyo kuna watu watamfuata Jean Pierre Mbemba gerezani, Kijani wao wanafuata sheria , taratibu na kanuni kwa sasa na mimi nawashauri waendelee hivyo kwani hao lazima watazivunja halafu watakiona kitakachowatokea. Iache Tanzania ibaki kama ilivyo. MUNGU IBARIKI TANZANIA.
ReplyDelete