Hivi vichwa vya habari Magazeti ya leo ni hatari kwa uhai wa Taifa, Serikali ijitazame upya

Sitaki niseme mengi ila tu nashauri Serikali ijitafakari, vichwa vya habari kama hivi tumezoea kuvisikia kwenye vyombo vya habari vya wenzetu, kwa kifupi vichwa hivi vya habari si vya kuvichekelea kwa sababu tu hayajakupata au kwa sababu yanaowafika si wa kundi lako ila ni vya kuchukua tahadhari sana, madhara yake huwa si madogo.

Serikali kuna mahali inakosea lazima ikosolewe, huwezi kutumia nguvu nyingi kiasi hiki kubinya Demokrasia, mshaurini vizuri Mkuu wa Kaya, Uhuru hauzuiliki kwa kitisho cha Bunduki na Mahakama zisizotenda Haki.

Hii ni dalili mbaya. "Taifa la hofu , mwisho wake ni majuto".

Wapo wenye akili ndogo watakaosema "Ukawa yamewafika, wameanza kulalama mitandaoni", lakini na mimi nawaambia "Si kila anayesema kweli ni UKAWA" sisi wengine hatuna hata mpango wa kutafuta Kadi za vyama, Chama chetu ni "Tanzania". Tusizibe midomo na Gundi za Mbao kisa tu tunatafuta Ukuu wa Wilaya

Huu ni Ushauri wangu

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ndugu mwandishi nadhani umepitiwa kidogo na taarifa kuwa kwa sasa msisitizo ni kazi tu. Yale mambo ya siasa siasa zisizokuwa na kichwa wala miguuu tupilia mbali kule. Muda wa maneno maneno umepitwa na wakati na sasa ni Hapa Kazi Tu. Hao wanasiasa uchwara ndio wanaotaka kuirudisha Nchi hii nyuma kimaendeleo kwa kufanya hujuma na vitendo ambavyo havistahiki. Na kama ni kutafakari kwa taarifa yako wewe mwandishi hii Serikali ya Sasa haina muda wa kukaa na kuyatafakari hayo maupuuzi ya hao wanasiasa uchwara wasiyoitakia Nchi hii Neema eti kisa na wao wanataka madaraka na uongozi kwa tamaaa zao zisizokwisha. Sisi Watanzania tuko imara kabisa na tuko pamoja na makini na Jemedari wetu ambaye ni Rais JPM. Hayo maupuuzi mengine na hao wapinzani uchwara hayatubabaishi na wala hayatatubabaisha na ni kwa sababu hawana hoja zozote za maana zaidi ya hizo agenda zao za kutaka kutukosesha AMANI yetu sisi Watanzania. Kusema ukweli kwa hilo wameshindwa. Watafute mbinu nyingine.

    ReplyDelete
  2. Uhakika ni kwamba Magazeti yamekithiri hapa nchi kwetu.. Na inaelekea Kupata biashara ya magazeti hasa kwa watu wa barabarani ni uzuri wa kichwa cha mvuto wa habari... Na Wahariri wa magazeti yetu wamelizoea na kuto kujua au kufikiria athari ya Vichwa hivi vya habari katika Jamii na mwanchi wa kawaida itamshinikiza vipi kwa mweleo aliokuwa nao.. Ningeomba Mantiki ya Habari na jinsi ya kuileta habari ifanyiwe tathmini na mhariri wa gazeti husika bila kuwa na mshinikizo mkubwa wa gazeti hili ni la nani na sera za chama gani.. manake inamuharibu fikra Mtanzania na Upotoshaji unalenga mgawanyiko wa itikadi... Kwa hiyo ni Kujua Sisi ni Watanzania na Tuwe Proffesional Journalist rather than being affiliated to Parties Ideology... Hii ni Mtazamo wangu na inaniuma nikiona magazeti wanatoa Vichwa ndivyo sivyo na Kuwaita watu Sijui Kiongozi Mkuu / Kambi Rasmi / na mengine mengi ya kutukusha kitu ambacho sicho sasa hii inamjenga mtu ambaye hatotaka hali ingine... Uthibiti unahitajika katika hili... Mungu ibariki Tanzania yetu na udumishe Amani Na Usalama ambao ni Jadi yetu sisi Watanzania.

    ReplyDelete
  3. Uhakika ni kwamba Magazeti yamekithiri hapa nchi kwetu.. Na inaelekea Kupata biashara ya magazeti hasa kwa watu wa barabarani ni uzuri wa kichwa cha mvuto wa habari... Na Wahariri wa magazeti yetu wamelizoea na kuto kujua au kufikiria athari ya Vichwa hivi vya habari katika Jamii na mwanchi wa kawaida itamshinikiza vipi kwa mweleo aliokuwa nao.. Ningeomba Mantiki ya Habari na jinsi ya kuileta habari ifanyiwe tathmini na mhariri wa gazeti husika bila kuwa na mshinikizo mkubwa wa gazeti hili ni la nani na sera za chama gani.. manake inamuharibu fikra Mtanzania na Upotoshaji unalenga mgawanyiko wa itikadi... Kwa hiyo ni Kujua Sisi ni Watanzania na Tuwe Proffesional Journalist rather than being affiliated to Parties Ideology... Hii ni Mtazamo wangu na inaniuma nikiona magazeti wanatoa Vichwa ndivyo sivyo na Kuwaita watu Sijui Kiongozi Mkuu / Kambi Rasmi / na mengine mengi ya kutukusha kitu ambacho sicho sasa hii inamjenga mtu ambaye hatotaka hali ingine... Uthibiti unahitajika katika hili... Mungu ibariki Tanzania yetu na udumishe Amani Na Usalama ambao ni Jadi yetu sisi Watanzania.

    ReplyDelete
  4. kwani ni uongo?watanzania mbona mnapenda unafiki,mtakapoambiwa hamna social media ndio mtajua nini maana yake.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Social media, kwani imeanza lini? Sidhani Kama itasumbua..

      Delete
  5. Hawa wenye magazeti au wandoshi uchwala, hili ni Taifa wakumbuke wasichanganye watu hakili kwa propaganda zao. Labda kwa tuhela kidogo walitopewa na kundi la watu wachache waliozoe kulitafuna Taifa hili, wakumbuke madhara ya v propaganda uwapa wote, bila shaka wanandugu familia,kama si watoto nchi yetu imempata kiongozi mtukufu na mwadilifu kwa msaala wa Taifa letu,nasi tunashudia hapa kazi tu, wazembe wavivu nye, wezi,mafisadi,nje na wale wote waliokuwa wenye kujifanya miungu watu wamekuwa wataratibu na huo ndio ubinadam, hata huduma muhimu za jamii zaonekana, wakina mama japo sasa wana angalau hauwezi. Huko kwenye mahospital ya kufwatulia binadam wote mnawaona hawa wazuri na wabaya, sasa wandishi uchwala wasilete shidaaa

    ReplyDelete
  6. Tunaweza tu kuishi bila magazeti. Kwanza social media ni umbea tu.....

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad