Je, Tundu Lissu Anajijenga ili Kugombea Urais 2020?

Hii ni kama strategy ya ukawa kujenga mgombea wake kwa mwaka 2020, baada ya kuone appointment ya Katibu mkuu kukosa mwito ndani na nje ya muunganiko huo.

Kauli na matendo ya Lisu yanaonyesha muelekeo wa kujijenga kisiasa kwa lengo la kugombea nafasi hiyo.

Ikumbukwe kwamba bado kuna pingamizi za ndani kwa ndani ukawa kama Lowasa atasimama kwa tiketi hiyo ifikapo uchaguzi mkuu, hii ni kutokana na yeye kuzidi kupungua ushawisi ukilinganisha na kipindi cha uchaguzi wa 2020.

Saikolojia ya mwanadamu unaonyesha kwamba mtu anayekipinga kitu flani sana either anakipenda sana au anahisi kama aliyenacho hastahili kuwa nacho isipokua yeye.

Saikolojia hii ndogo inapelekea wengi wetu kuanza kunyanyua kope za macho na kujiuliza nia halisi ya Lisu baada ya kuona na kusikia haya aliyoyafanya hivi karibuni.

Je huu ndio mwanzo wa safari ya kugombea nafasi hiyo 2020, na mwendelezo wa matukio toka kwa mwanasiasa huyo?
Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Labda,ingependeza kama Lissu angesimama
    badala ya Lowasa.Ukweli wananchi wengi tuliichoka serikali iliyokuwa madarakani kwa muda mrefu(CCM)na kuamini kwamba labda CHADEMA wangeshika nchi wangefanya vizuri,sasa imekuwa ndivyo sivyo mbaya au pengine nzuri zaidi rais Magufuli ameanza kukubalika japo kuna mapungufu ambayo kama akiweza kuyaboresha na hasa kwenye maslahi ya wananchi pamoja na kuboresha mishahara ya wafanyakazi,2020 itakuwa ngumu kama atasimama Lowasa tena,maana tatizo kwa Lowasa ilikuwa ni kitendo cha kutokea CCM,(HALAFU ILIKUWA KIMAGUMASHI MNO)ambako alikuwa tayari kugombea akiwa huko enzi za safari ya matumaini.Sikumchagua Magufuli wala Lowasa,niliamini CCM ni ileile na lowasa alitoka hukohuko ndani ya muda mfupi,na yale madongo ya ufisadi kwa viongozi wengi wa CCM ndio yaliyonifanya nitupe karata yangu kwa chama kingine.MUNGU IBARIKI TZ.

    ReplyDelete
    Replies
    1. SURE LISU ANAKUBALIKA KIASI KULIKO LOWASA,TENA WASIWAZIE TENA KUMUWEKA LOWASA AWE MGOMBEA.

      Delete
  2. LISUUUUUUU,ANAGANGA NJAA.

    ReplyDelete
  3. Kama ni kugombea nafasi ya Urais kwa mwaka 2020 ni lazima ajipange kweli kweli kwani sio mchezo. Ili aweze kukidhi hivyo vigezo inabidi aje na mitizamo hasi ambayo itatuaminisha sisi Watanzania kuwa atakuja kufanya kitu cha ziada cha kile kinachofanywa na Rais wa sasa aliyepo madarakani. Agenda za kimsingi na mipango thabiti atakayokuja nayo ya namna ya kuwaondolea wananchi umaskini, kuendeleza huduma za jamiii, kukusanya mapato ya Serikali kutoka katika vyanzo sahihi, pamoja na kubuni njia mbadala wa kuinua viwango vya Elimu na kupunguza uwiano wa aliyekuwa nacho na ambaye hana hizo zinaweza kuwa sababu za kimsingi za kutufanya sisi Watanzania tulio wengi walau kumuangalia na kumfikiria japo kidogo sana. Lakini kwa huu utoto anaoufanya wa kumkejeli Rais aliyepo madarakani ama kumtukana ama kupinga kila jambo jema analotaka kutufanyia sisi Watanzania haitamsaidia chochote kile na wala haitamuwezesha kugombania nafasi hiyo nyeti katika Uongozi wa Taifa hili zaidi na sana sana kama sio kujiletea kifo chake kisiasa kama walivyo wanasiasa uchwara wengine. Kama Zitto Kabwe na akina Mbowe na Lema. Kumkejeli na Kumtukana Rais aliyepo madarakani haitawasaidia chochote. Hizo ni kiki za kitoto sana ambazo inabidi wawaachie akina Wema Sepetu na Zari wa Diamond.

    ReplyDelete
  4. Lissu, anatetea haki ya watanzania na tanzania. period. Tusipoangalia nchi yetu itafika mahali hatutaweza tena kusimama kiuchumi kama hatutakuwa makini na maamuzi yetu!! Leo DW imesema kuwa watalii wengi kama 8000 wamecancel safari zao za kuja tz na wafanyakazi wa secta ya utalii wamelazimishwa kuchukua likizo za muda mrefu za bila malipo!! YOTE HII NI MAAMUZI YANAYO FANYWA NA BUNGE LA UPANDE MMOJA!! I AM VERY SAD AND SORRY FOR MY COUNTRY WALAHIH....

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad