Ulimwengu amesema ni kutokana na kufinya uhuru wa kujieleza na hususan kwa kufinya uhuru wa wawakilishi wa wananchi ndani ya bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Ulimwengu ameendelea kwa kusema katika hili hamna kifimbo cha uchawi cha kujinasua isipokuwa mchakato wa katiba ambao ulichukua fedha nyingi kisha ukaachwa njiani na Mheshimiwa Kikwete.
Mwandishi huyo wa habari na mchambuzi wa masuala ya kisiasa ametaka Raisi mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete kufikishwa mahakamani kwa kosa la kuisababishia serikali hasara baada ya kutokuufanikisha mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya.
Jenerali Ulimwengu alisema katika kipindi cha mchakato wa katiba mpya, fedha nyingi ambazo zilitokana na kodi za wananchi zilitumika katika shughuli mbalimbali lakini katiba mpya haikupatikana.
“Katika kipindi hiki tumeona viongozi mbalimbali waliopita wakichukuliwa hatua kwa kuisababishia serikali hasara… Kikwete anapaswa kufikishwa mahakamani kuelezea zile pesa za mchakato wa katiba zitarudi vipi,” alisisitiza.
Akijibu hoja hiyo, mwenyekiti wa mdahalo huo, Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa amesema wakati wa mchakato huo yeye hakuwa mshauri wa rais hivyo hawezi kulijibia suala hilo.
“Mimi sikuwahi kuwa mshauri wa raisi wala mshauri wa chama juu ya mchakato huo, ila niliombwa kutoa maoni kama wananchi wengine,” alisema Mkapa na kuongeza kuwa wasomi wanapaswa kufanya uchambuzi makini kabla ya kutoa hoja kwani kuna baadhi ya hoja hutolewa lakini sio muhimu kwa maendeleo ya taifa. Video:
kweli kabisa kikwete ashitakiwe
ReplyDeleteashitakiwe tena haraka ana makosa mengi sana huyo kwanza wafanyakazi hewa haiwezekani yeye alikuwa madarakani inamaana hakuwaona wafanyakazi hewa au walikuwa ni sehemu yake hiyo ni moja lakini pili macontena tena yameingia yeye akiwa madarakani mtu wa watu anakuja kupata shida bure tatu flo mita ya bandarini miaka kumi haifanyi kazi na kuisababishia taifa hasara kweli hyu jamaa hakutufaa basi tu jenerali ulimwengu uko sawa kabisa hjakosea ikiwezekana waondolewe kinga hawa marais ili wakikosea waadhibiwe
ReplyDeleteKwanza kwa kuiachia nchi ijiendeshe yenyewe na huku akijua wanachi wamepa jukumu la uongozi, kusimamia maslahi ya nchi, pili wifi, ufisadi uliopitiliza kwenye ungozi wake, tatu kukapelekea Taifa kila miundo mbinu yote kuwa hovyo hovyo kama kukosekana kwa huduma za jamii, nchi ikawa mikononi mwa kundi la watu wachache wanaitafuna mpka kupelekea kuitwa shamba la bibi
ReplyDeleteajipelike mwenyewe mahakamani kabla hatujalivalia njuga hili
ReplyDeleteNa Mkapa mkimuacha wapi??? aliuza mpaka nyumba za serekali hamuyaone hayo. Muacheni baba wa watu. Mkapa na mkewe wameiba weee lakini memuona JK tu ndio mwezi please give us a break.
ReplyDeleteSasa yeye wa awamu ya Tano angemuadhibu mkapa sasa nae kwa maovu yake alikolifanyia Taifa mpka Taifa kuendelea kutabika sasa nae ndio kwanza amelinda na kumfichia maovu yake, na akayachukua zaidi na kuendelea kuliumiza Taifa, hapa tuko kwenye mustakabali wa Taifa sio kuteteana ujinga ujinga tembo wakipigana ziumiazo nyasi. Yaani wanachi wa kawaida ndio wanaoumia,
DeleteMkapa ndiochanzo chote Cha matatizo bora kikwete tumekula tukekunywa tumevaa,leo toka aondoke madarakani hata mwaka bado,hali imekuangumu maishamagumu pesahakuna je hatahiyo kodi tutailipaje?napesahakuna?biashara zinazidikufa,kuenina shukurani na kikwete,
ReplyDeleteWachache ndio mmepata maisha hayo.kundi kubwa limetabika tu kwa kila kitu. Hii ni Tanzania ni Taifa tena lina wingi wa watu ndani yake na kila mmja anaitaji khaki yake kama mkazi wa Taifa hili, hata huko kula na kunywa kama ulivyosema, wengi wa Taifa hili mlo mmja kwa siku, huduma za jamii ni shidaa kama dawa, hospital, shule kata miundo mbinu tabu ukiachana na mijini, vijijini ni hoi, hamna cha afadhali ya likwete labda ilikuwa kwako ni mmjawapo wa wale, wezi,rushwa,ufisadi sasa ndio unaona afadhali,
Delete