Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete amesema nchi za Afrika haziwezi kukwepa misaada kutoka nchi za Ulaya kwa kuwa misaada hiyo ni jukumu lao la kihistoria.
Kikwete alisema hayo jana wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku mbili unaojadili malengo mapya 17 ya Umoja wa Mataifa yanayohusu ‘Maendeleo Endelevu kwa mwaka 2030’.
Mkutano huo umejikita kujadili lengo namba 16 linalohimiza haki, amani na jamii shirikishi, hasa katika masuala ya utawala wa sheria kama chachu ya maendeleo endelevu.
Kikwete alisema jukumu hilo linapaswa kuendelezwa kwa kuwa maendeleo ya nchi za Ulaya yalitokana na rasilimali walizozitoa Afrika kipindi cha ukoloni.
Alisema nchi za Afrika zina rasilimali za kutosha hivyo, ili zifanye kazi bado kunahitajika uwekezaji ambao utaweza kuinua viwanda na kukuza uchumi wa nchi za Afrika, kwani bila hivyo itachukua muda mrefu kufika mbali kiuchumi.
Hata hivyo, alisema nchi za Afrika lazima zijiwekee utaratibu wa namna ya kupokea misaada hiyo, lakini lengo liwe ni kunufaisha wazawa na kwa kufuata sheria za nchi husika na zile za kimataifa.
“Misaada tunayoizungumzia siyo lazima iwe fedha, bali tunahitaji wawekeze zaidi kwetu kwa mikataba ya kisheria inayolinda wazawa, kwa mfano Tanzania tuna rasilimali za kutosha kama gesi, madini na vinginevyo, lakini hivi vyote vinahitaji kuibuliwa na kutayarishwa. Lazima tuwape nafasi ili kufanikisha lakini kwa sheria zitakazowalinda Watanzania,”alisema Kikwete.
Kauli hiyo ya Kikwete imekuja wakati Rais wa Awamu ya Tano, John Magufuli amekwisha kuweka msimamo katika hotuba zake kadhaa akitaka Tanzania ijitegemee kwa asilimia kubwa badala ya kutegemea misaada ya nje.
Wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya kwanza ya juu (flyover) katika makutano ya Barabara za Mandela na Nyerere eneo la Tazara, Rais Magufuli aliita misaada ya wahisani ‘mkate wa masimango’ na kusema kuliko kula mkate huo ni bora kushindia muhogo.
Ingawa hakufafanua wala kuzungumza kwa undani juu ya kauli hiyo, lakini aliitoa ikiwa zimepita siku chache tangu Shirika la Maendeleo la Milenia (MCC) la Mareka ni kusitisha msaada wa Dola za Marekani milioni 472.8 karibu Sh1 trilioni kwa madai kuwa Tanzania ilikiuka misingi ya kidemokrasia kwa kurudia uchaguzi wa Zanzibar na kushindwa kusimamia She ria ya Makosa ya Mtandao.
Pia, Rais Magufuli Machi 29, akiwa katika kijiji cha Mlimani, Wilaya ya Chato mkoani Geita alisema jukumu kubwa lililo mbele ya Watanzania kwa sasa ni kushikamana na kujisimamia katika maendeleo ili kila mmoja ahakikishe anaongeza uzalishaji na utendaji kazi mahali pake pa kazi.
“Kwa hiyo ni lazima tujisimamie sisi wenyewe, na tukijisimama sisi wenyewe kwa kila mmoja kuwajibika mahali alipo, kama ni mfanyakazi afanye kazi kwelikweli, kama ni mkulima afanye ukulima wake kwelikweli, kama ni mfanyabiashara afanye biashara kwelikweli, kama ni mfugaji afuge kwelikweli, kama ni mvuvi avue kwelikweli, Tanzania hii tutavuka,”alisema.
Mkutano huo ulioandaliwa na Taasisi ya Kimataifa ya Maendeleo ya Sheria (IDLO) yenye makao makuu yake nchini Italia, ambayo kwa Tanzania mlezi wake ni Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa.
Akizungumza kwenye mkutano huo, Mkapa alisema katika nchi yeyote ili kupata maendeleo ni lazima kuwe na Katiba ya wananchi ambayo haitalenga kundi moja.
“Awali nchi nyingi za Afrika hazikuwa na Katiba ya wananchi, bali kulikuwa na Katiba ya chama ambayo kwa sasa ni nchi za kidikteta pekee zimebaki na mfumo huo, kwa sasa tulilenga kuweka sera, mikakati thabiti ili tuweze kutekeleza malengo mapya ya dunia chini ya dira mpya ya Umoja wa mataifa ya maendeleo ya dunia,” alisema Mkapa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki alisema kama ilivyo ajenda ya nchi za Afrika, nchi haiwezi kuwa na utawala wa sheria kama hakuna upatikanaji mzuri wa sheria.
“Lazima uweke mifumo mizuri ya kutatua migogoro pia, utoaji wa vibali bila kutoa rushwa, hata katika uwekezaji utakapokuwa huna sheria nzuri inayolinda upande huo ni vigumu wawekezaji kuwepo,” alisema Kairuki.
Mkurugenzi Mkuu wa IDLO, Irene Khan alisema mkutano huo umejikita katika kujadili haki, amani na jamii shirikishi.
“Lengo ni kuwa na dira mpya ya maendeleo ya dunia inayolenga kutokomeza umaskini, kulinda mazingira, kupambana na mabadiliko ya tabianchi na kushirikisha makundi yote kwenye jamii katika masuala ya maendeleo,” alisema Khan.
Kikwete: Nchi za Afrika Haziwezi Kukwepa Misaada ya Wazungu
12
June 02, 2016
Tags
Nyinyi marais mliostaafu kaeni chonjo na ushauri wenu mbuzi mlitawala nchi na mliifikisha wapi kwa hiyo omba omba yenu misaada kwenye nchi watu weupe?
ReplyDeleteFyuuuuuuu
ReplyDeleteMtu nzima unaropoka tu
Jukumu la wazungu kutusaidia
Viongozi wengi wa Africa ni mbumbu
Wazungu hawatoi msaada bla wao kufaidika
Ni hapa inaonyesha wazi bila haya maraisi wanaomba.ni aibu kubwa.pia maraisi waliopita wanamchanganya na kumwingilia manukumu Rasi wa sasa na kufanya kazi ya kuikatisha tamaa nguvu ya Raisi wa sasa.Bado mfume wao ulioliangusha Taifa wanazidi kuuendeleza. Lini waliisikia nchi ya ulaya su Marekani kuomba msaada hadharani.ni kujidharalisha. Je ndugu zangu Watanzania kwa nini tunaongozwa na kauli za maraisi wawili.sheria za nchi kwa nini zisimnyamazishe. Hivi Afrika haina mwongozo wa pamoja kukanusha.Elimu na utashi ni mali.kwa nini viongozi wa Afrika hawaoni mbali.unamwambia mzungu nchi zao zimejengwa na radlimali zetu nani hajui hii. Sasa sana mwambie akulipe na akurudishie alichokiiba we unamrundikia tena na elimu unayo na unashindwa kuitumia na unashindwa kujitawala, kujiongoza wala mbinu zako bonafsi huna baada ya miaka hamsini ya uhuru.unazidi kumbana msomi wako, kumyanyasa, kutomumsaidia na kumsapoti, unaua elimu, hujali afya za mtanzania, hupiganii maslahi ya mtanzania, hutaki mtanzania awe huru, apate katiba. Ajitawale, awe na elimu, afya bora, unasema mzungu atakusaidia lini ulimwona mzungu anasaidia bila kuweka maslahi yake mbele.bado unamrudisha, kumuomba na kumpigia magoti.unaruhusu mikataba isiyo na faida kwa nchi.hivi washauri nchi hii hawapo. Mbona unaidharalisha nci na watu wake wote.Ni kweli huoni makosa haya.ni dissappointment kubwa.huko ndiko unavyowapa kibali na nguvu waje watuhujumu, watutawale, watudharau. Unawapa padi huko nje waje wsgongane na sheria za nchi.
ReplyDeleteWhat a dissgrace.unamwongezea shida Magufuli.ona Bunge la ccm linafuata mfumo huohuo vichwa tupu vimejaa maji na kuwadharalisha watu waluochaguliwa wapinzani wenye sauti, utu, hekima.unaacha hewa iamue mambo makuu ya nchi.ni hawa hawa ccm bado hawajababilika. Hawajui kufikiri, nu nguvu za udicteta, challenge hawajui ni muhimu.
Kweli tuna endeshwa na mizoga.
Ni hapa inaonyesha wazi bila haya maraisi wanaomba.ni aibu kubwa.pia maraisi waliopita wanamchanganya na kumwingilia manukumu Rasi wa sasa na kufanya kazi ya kuikatisha tamaa nguvu ya Raisi wa sasa.Bado mfume wao ulioliangusha Taifa wanazidi kuuendeleza. Lini waliisikia nchi ya ulaya su Marekani kuomba msaada hadharani.ni kujidharalisha. Je ndugu zangu Watanzania kwa nini tunaongozwa na kauli za maraisi wawili.sheria za nchi kwa nini zisimnyamazishe. Hivi Afrika haina mwongozo wa pamoja kukanusha.Elimu na utashi ni mali.kwa nini viongozi wa Afrika hawaoni mbali.unamwambia mzungu nchi zao zimejengwa na radlimali zetu nani hajui hii. Sasa sana mwambie akulipe na akurudishie alichokiiba we unamrundikia tena na elimu unayo na unashindwa kuitumia na unashindwa kujitawala, kujiongoza wala mbinu zako bonafsi huna baada ya miaka hamsini ya uhuru.unazidi kumbana msomi wako, kumyanyasa, kutomumsaidia na kumsapoti, unaua elimu, hujali afya za mtanzania, hupiganii maslahi ya mtanzania, hutaki mtanzania awe huru, apate katiba. Ajitawale, awe na elimu, afya bora, unasema mzungu atakusaidia lini ulimwona mzungu anasaidia bila kuweka maslahi yake mbele.bado unamrudisha, kumuomba na kumpigia magoti.unaruhusu mikataba isiyo na faida kwa nchi.hivi washauri nchi hii hawapo. Mbona unaidharalisha nci na watu wake wote.Ni kweli huoni makosa haya.ni dissappointment kubwa.huko ndiko unavyowapa kibali na nguvu waje watuhujumu, watutawale, watudharau. Unawapa padi huko nje waje wsgongane na sheria za nchi.
ReplyDeleteWhat a dissgrace.unamwongezea shida Magufuli.ona Bunge la ccm linafuata mfumo huohuo vichwa tupu vimejaa maji na kuwadharalisha watu waluochaguliwa wapinzani wenye sauti, utu, hekima.unaacha hewa iamue mambo makuu ya nchi.ni hawa hawa ccm bado hawajababilika. Hawajui kufikiri, nu nguvu za udicteta, challenge hawajui ni muhimu.
Kweli tuna endeshwa na mizoga.
Basi tukiwa tumefikia hatua hiyo kwamba nchi au bara hili haliwezi endelea. Basi na arudi huyo mzungu kuja kutawala kuwa koloni tena, maanake sisi watu weusi tumeshindwa tumefeli kila nyanja, si kutokana na uongozi mbovu na corrupition zilizopitiliza, kama viongozi kuiba mali za nchi na kujilimbikizia na kujaza mifuko yao, pasipo maslahi ya nchi, watu wansjiliwa kazi hawafanyi kazi bali ni wizi kila kona,Kodi hawataki kulipa wale makabaila kama wafanyaboashara wakubwa nchi itaendelea vip. Mzungu akija akitwa hana mchezo ni kazi na sheria ni msumeno, ndio maana nchi zao waliowengi zinaeleweka. Hata wao wanajua Afrika ni bara tajiri ila watu wake wamefeli kila nyanja, na akitwa atakuja chap chap, s anajua huku wamelala usingizi,
ReplyDeleteMfyuu mtu na akili zote na marifaa na ujuzi ukiacha hata elimu ya darasani hii nchi au bara hili limejaliwa sana kwa utajili mkubwa duniani, lakini watu wake kama huyu baba mwenye picha hapo juu haoni na kukosa maarfa. Kukosa maarifa ni tabu na ujinga sana, kiasi kwamba unamuona mtu furani ndio msaada kwako pasipo yeye mambo hayaendi,kosa mali pata akili, wazungu bara lao halina raslimali za asili sana kama bara letu Afrika, lakini wamejaliwa akili ya maarifa. Kutatua matatizo yao
ReplyDeleteYani huyu Baba sijui anatokea wapi. Miaka yote aliyokuwa Rais wa Nchi hii pamoja na kujipendekeza kwa wazungu na hasa pale Marekani ndio haya matokeo tunayoyaona katika Nchi hii. 1) Rushwa iliyokithiri 2) Watendaji na hasa wa Serikalini kukosa uwajibikaji 3) Huduma mbovu kabisa za kijamii ikiwamo akina Mama wajawazito kujifungulia watoto wakiwa chini ya sakafu na pia ukosefu wa dawa 4) Miundo mbinu mibovu kabisa ambayo inakufanya ushindwe kuelewa kama kweli Nchi hii inakwenda na wakati na hasa katika kipindi hiki cha Teknolojia katika karne hii ya ishirini na moja 5) Wizi uliokthiri wa makontena na mafuta bandarini 6) Umasikini uliokithiri miongoni mwa Wananchi na tofauti kubwa ya walionacho na wasiokuwa nacho. Sasa leo hii anaposimama na kusema eti Nchi za Africa haziwezi kujisimamia na maendeleo yao wenyewe ana maana gani??? Hivi huyu Baba yukoje. Asije kutuambia hayo yote aliyoyasababisha wakati wa utawala wake alikuwa hapo anawasubiri wazungu waje na kutusimamia kuhusu Rushwa, Miundo mbinu pamoja na mambo mengine. Kimsingi hilo ni tusi kubwa sana kwa Waafrika wenye dhana endelevu ya kujitegemea. Afica ina wasomi chungu mzima katika kada mbalimbali ikiwamo hiyo kada anayoizungumzia yeye ya Sheria. Africa ina wanasheria wengi tena mahiri na wenye kiwango cha kimataifa ambao wanao upeo na uwezo mkubwa wa kuzijenga na kuzipambanua hoja za kisheria za kulisaidia Bara la Africa kuzilinda raslimali zake. Bara la Africa lina watu wengi wasomi na wasiokuwa wasomi ambao wana mwamko wa hali ya juu wa dhana kujitegemea. Kutudanganya kwa kusema eti misaada kutoka Ulaya haikwepeki kwa sababu ni jukumu lao kihistoria huo ni uongo wa hali ya juu na ambao hauwezi kukubalika. Huyu Baba inavyoelekea haendi na nyakati. Kwa taarifa yake Wazungu wametuchoka sana sisi WaAfica. Hawataki hata kutusikia. Na sababu mojawapo ya wao kutuchoka ni kila kukicha tunawaomba misaada. Usiku na Mchana tunakesha tukiwaomba msaada. Hilo jambo linawakera kupita kiasi na ndio maana misaada yao haiishi masimango na masharti magumu na ya hali ya juu. Hiyo yote ni katika kutupunguzia spidi ya sisi waswahili kukesha na kuombaomba. Huyu Baba sijui anaitoa wapi falsafa hii ambayo hata akina Malcom X na Martin Luther King Jr waliikataa pale Marekani wakati wa harakati za kupigania usawa kati ya mtu mweusi na mzungu. Na hasa Malcom X aliwakatalia kabisa wale weusi wa pale kulilia vitu ambavyo hawakuvianzisha wao. Alikuwa anawaasa na wao watu weusi waende wakaanzishe vitega uchumi vyao pamoja na mashule yao ili kuondokana na dhana ya kuwategemea wazungu. Kitu kingine ambacho huyu Baba anashindwa kukielewa ni kuwa wazungu wanatuchukia sana juu hatuwezi kujisimamia mambo yetu wenyewe mpaka tuwasubiri wao. Kwa kweli huo ni udhaifu mkubwa ambao unawachukiza sana wazungu kwa sababu wanabakia kutushangaa ni kwanini sisi WaAfrica tunashindwa kujisimamia vitu vyetu wakati tumebarikiwa kuwa na maliasili chungu mzima pengine kulinganisha na Nchi nyingi za kwao. Kwa kweli hilo linawaudhi sana. Na ukiangalia sana kuna ukweli ndani yake. Unawezaje kushindwa kujisimamia mambo yako ya Ndani halafu unaende kutegemea watu wa nje waje kukusimamia. Hicho kitu hakileti maana na wala mantiki ya aina yoyote ile na hasa katika kipindi hiki cha karne ya ishirini na moja ambacho WaAfrica wasomi na wenye upeo wa mambo wako wengi. Kwa kweli huyo Baba kama hayo ndiyo maudhui yake katika hilo kongamano basi atakuwa chukizo kubwa miongoni mwa WaAfrica ambao wao wanajikita zaidi katika dhana ya kujitegemea na sio dhana tegemezi. Kimsingi huyo Baba amechoka na maona yake yamepitwa sana na wakati. Alishindwa kuifikisha Tanzania na Watanzania pale tulipokuwa tunapatarajia. Sasa amebakia kuzungumza vitu ambavyo hata havieleweki. Huko ni kutuyumbisha na kutudhalilisha sisi WaAfrica na Bara la Africa kwa ujumla. Kama hana agenda za maana za kuzungumza ni kwa nini asiende kujipumzikia pale Bagamoyo kuliko kuwa chukizo kwa Waafrica???
ReplyDeleteHuyu Baba anaenda na kuongea maupuuuzi yake mpaka nadhani wazungu wanabakia kumshangaaa na kutushangaa sisi Waafrika na hasa Watanzania kuwa ilikuwajekuwaje tukawa na Kiongozi Mpumbavu kama huyu. Hizi ni zama ambazo kila mtu na kila Nchi Duniani inaelekeza mbinu zake katika kujitegemea yeye na bila ya aibu amekazana na dhana ya kuwategemea Wazungu. Sijui ni nani kamwambia kuwa Wazungu wanatupenda. Wazungu wametuchokaaaaaa kwa sababu ya hiyo dhana ya kuombaomba. Huyu Baba anashindwa hata kusoma alama za nyakati. Anashindwa hata kuelewa upepo ni wapi unapoelekea. Anaenda huko kwenye makongamano ya kimataifa na kuzungumza vitu vya kutuaibisha sisi Watanzania. Sijui ni nani kamtuma kuzungumza huo utumbo.
ReplyDeletemwenzio ataki misaada ya wazungu! tulisahau raha sako za kuruka majuu na safwali za hapa na pale, tulisahau kabisa kuangaliaga bunge la jamuhuri likiwa live, tulisahau kunywa kachai katamu sasa tunakunywaga kauji tunaunga na chumvi kidogo. ila tunamupenda bure huyu mutumbua majipu. tumekumisi handsam wa ukweli musee wa tabasamu ari mpya, kasi mpya! acha tuendelee na mzee wetu wa miayo. hapa kazi tu!
ReplyDeleteUtashangaaa sana punguani mkubwa sana wewe.Ulishazoea Rushwa na Wizi wa makontena.Nyang'au mkubwa sana wewe.
DeleteNa isitoshe kwa kipindi chake mataifa ya wazungu wa kutoa hiyo misaada wametoa sanaa. Na walikuwa na malengo yao miaka kumi ya mwanzoni millenium Afrika ipige hatua japo angalau iringane kidogo na pembe nyingine ya dunia, na watu wake wapunguze kuhamaa nchi zao kama si bara lao, maajabu yake hawa hawa viongozi ndio wakaona ni miradi na kama si kutia mifukoni Mwao. Na ndio karne ikaongezeka kwa wafrica kulihama bara lao nchi zao na corrupition tele kati ya nani tajiri nani maskini mpka wazungu wakapekea kutushangaa, na kuona tumeshafeli ikiwa tumeshindwa kutoka hata kwa misaada waliojitoa wao muhangaa kwa kodi zao. Kwa hiyo wameshatuona wajinga na IQ ndogo na hawawezi tena endelea toa misaada tu nao wanaitaji na wakitoa sasa ni masharti ili nao wasije umia. Kwani hawakioni kinachoendelea katka nchi zetu, sana sana ni matatizo tu, sasa wanataka tutumie akili zetu na maarifa yetu wenyewee labda tutatoka tuachane na ujinga wa kuwa omba omba, kwa kuwa bara limejaliwa raslimali nyingi duniani na ni moja ya mabara tajili duniani Afrika, na nchi tajili kabisa kwa rasilimali asilia ziko Afrika, congo inaongoza zaidi kwa utajili asilia duniani, na zikifwatiwa na zingine zote afrika, lakini tumelala fofofo ni shidaaa.
ReplyDeleteKosa la elimu, utashi na hekima.ni uswahili mtupu. Inabidi raisi kama huyu inabidi spewe msjibu hanazo juu. Kawekwa kibaraka kafika majuu hakitarajia, kapata kiwewe.limbukeni aibu kwa taifa. Tatizo hajielewi.ujinga unaua ni hatari kwa maendeleo. Ndo kinachorudisha maendeleo ya Africa nyuma. Viongozi kama hawa hata haya hawana.
ReplyDelete