Wachambuzi na wadau mbalimbali wametoa maoni yao kuhusu Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/17, huku watumiaji wa huduma za fedha kwa njia ya simu wakikumbwa na maumivu wa kodi.
Hiyo ni siku moja baada ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango kuwasilisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 20116/17.
Pamoja na mambo mengine, bajeti hiyo inapendekeza kuongeza ushuru wa vinywaji baridi, maji ya juisi, vinywaji vikali, bia na sigara.
Pia itawagusa watumiaji wa M-pesa, Tigopesa, Airtel Money, Ezypesa kwa kukatwa Sh 280 kwa kila Sh 1000 watakayotuma.
Jana Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo), alisema hatua hiyo ya Serikali kuendelea kutafuta kodi kwa kuzidi kuwaumiza wananchi inakwenda kinyume na matarajio ya Watanzania wengi.
Alisema katika bajeti hiyo ya Serikali na ukusanyaji wa mapato yake, katika kila Sh 1000 itakayokatwa kwa huduma kwenye ATM kuanzia Julai Mosi mwaka huu, Sh 280 zitachukuliwa na TRA.
Zitto alisema hali hiyo pia itawakumba watumiaji wa miamala ya M-pesa, Tigopesa, Airtel Money, Ezypesa ambalo ndilo kundi kubwa la Watanzania wanaotumia huduma hiyo nchini.
Aawali kodi ya bidhaa ilikuwa asilimia 10 lakini kwa hatua ya kuongezwa kwa kodi ya ongezeko la thamani kodi itapaa na kufikia asilimia 28.
Kwa mantiki hiyo, katika kila Sh 100 kodi ni Sh 28 na katika Sh 1000 kodi ni Sh 280.
Kutokana na hali hiyo kodi ya VAT hulipwa na mtumiaji wa mwisho ambaye anatuma au kupokea fedha, hali ambayo itawaumiza watumiaji wa mwisho.
“Hivyo hivyo katika miamala ya M-pesa, Tigo pesa na kadhalika, katika kila Sh 1000 itakayokatwa kwa huduma kwenye ATM kuanzia Julai 1, 2016, Sh 280 zitachukuliwa na TRA,” alisema Zitto.
Alisema ameshangazwa na hatua ya Serikali kuongeza kodi ya VAT kwenye utalii hali ambayo inaweza kusababisha Tanzania kupoteza watalii wengi kwa washindani wake kwa sababu itaongeza gharama kwa watalii.
“Kama tunataka kutumia utalii kama kichocheo cha ajira ni vema kufikiria upya suala hili,” alisema.
Akizungumzia mapendekezo ya Serikali katika Sheria ya Kodi ya VAT ili kutoza kodi bidhaa zinazotoka Zanzibar, alisema hatua hiyo inavunja misingi iliyowekwa na sheria ya zamani ambayo ilifanana na ile za Zanzibar.
“Ikumbukwe kuwa Sheria ya Kodi ya VAT ya 2014 ilivunja misingi iliyowekwa ya sheria ya zamani ambayo ilifanana na ile ya Zanzibar. Mapendekezo ya sasa yana madhara makubwa kwa Zanzibar kwa sababu hakuna atayewekeza Zanzibar ili kufaidika na soko la Bara.
“Biashara nyingi zinazozalisha Zanzibar zitahamia Tanzania Bara. Mapendekezo haya yanaweza kusababisha mgogoro kati ya pande mbili za Muungano,” alisema.
Kilio Kwa watumia M-pesa, Tigo Pesa , Airtel Money na Wale wa Kwenye ATM.......Kila ukituma 1000/- utakatwa kodi 280/-
7
June 10, 2016
Tags
Tunaomba hizo picha mnazo tumia, Muwe mnaandika Kumbukumbu / Archives au tarehe.. Ukiangalia hiyo ya hopo juu ina mislead na inaonesha kwamba TBC inamuhojia au inapeperusha habari zako... Nape na TCRA pia wanaiona hii picha... Huyu mwanasiasa uchwara maji yamemfika shingoni na Yupo chama kimpya cha......
ReplyDeleteBaadhi ya wanasiasa wanawatisha watu kwa kueleza mambo kijumlajumla badala ya kufafanua ili mtu aelewe mfano unaposema kuwa ktk kila 1000 inakatwa 280 hii maana yake mtu ukitoa 10,000 unakatwa 2800 wakati si kweli kwani kwa kitendo cha mtu kwenda kutoa sehemu ya akiba yako benki au kwenye simu hakuna biashara yoyote uliyofanya kiasi utozwe kodi kiasi hicho isipokuwa mtoa huduma ndiye aliyefanya biashara na ndio wanaotakiwa kulipa hiyo kodi yaani kama unaenda kutoa pesa kwenye atm au kwenye simu mtoa huduma anakakuta kiasi fulani kwa ile huduma aliyekupa hivyo hicho kiasi alichokukata ndio anatakiwa akilipie hiyo kodi kama amekulipisha 1,000 basi tra watachukua 280 lakini sio kama wanavyoeleza hawa wanasiasa uchwara ili kuwatisha watu kwamba mtu akienda kutoa pesa benki au kwenye simu basi atakatwa pesa chungu nzima,sio kweli acheni kuwadanganya watu.
ReplyDelete:-d
ReplyDeleteMheshimiwa kachemka, Ukitoa pesa benki ni kweli benki italipia ushuru 10% na VAT 18% lakini sio kwenye kiasi unachotoa bali kwenye makato unayolipa benki. Mfano kama ukitoa 100,000 utakatwa sh 2000, basi kodi iko kwenye 2000 na sio 100,000 uliyotoa.
ReplyDeletePili hakuna mapendekezo ya VAT kwenye huduma za mitaandao ya simu bali excise duty 10% kwenye gharama za kutuma au kupokea pesa. Atakumbuka kwamba sheria hii ilipitishwa july 2013 lakini ilikuwa kwenye money transfer tu hali iliyosababisha mitandao kuhamishia gharama za kutuma kwenye kutoa ili kukwepa kodi hii. na sasa kodi imewafuata hukohuko kwenye kutoa pia.
Hb ww unaejua kuelewesha watu tueleweshe.hy tuambie hy mtoa huduma yy atapata wapi pesa za kulipa pesa hizo km hajapata faida kwa mteja,kwa maana hiyo basi mteja ndie atakae umia sbb mtoa huduma hawezi kubali kupata hasara ni lazima pesa yk irudi
ReplyDeleteHapo kweli wanasiasaucchwara WA ajenda ya upotofu kwa wengi qasio uelewa.. Atabidi serikali iwaelinishe tafsiri sahihi Ili iweze kuleya uelewa kwa mwanancchi WA kawaida Na ikibidi Tv 📺 Na magazeti Na mabango katika mabasi ya mikoani. Na mwendo Kasi yahusishwe manake upotoshwaji umeshaanza...Hapa Ni kazi Tu NA hamuoni ndani tunawajueni hila zenu Na njama zenu!!!
ReplyDeleteIssue ya Zenji utaitumia Sana je umeshahamia Cuf au bado uko Chama cha watu watatu..au cdm
ReplyDelete