Kinachomtesa Raisi Magufuli ni Woga

NCHI inatikisika. Kilicho nyuma ya mtikisiko huo ni woga wa mkuu wa nchi, Rais John Magufuli, tena woga usio na mchungaji, anaandika Faki Sosi.
Mambo mengi yanayoonekana kumpoteza Rais Magufuli kwenye nyoyo za Watanzania ni yale anayoweza kuyatibu.

Bila shaka, kama angekaa na wasaidizi wake na wasaidizi hao wakaondoa woga, Rais Magufuli angeendelea kutawala nyoyo za wananchi.
Rais Magufuli hapendi kukosolewa, anapotokea mtu na kumkosoa, huumia na kuhemuka, hili ndio tatizo kuu.

Katika hili, amepishana kwa asilimia kubwa na mtangulizi wake, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete. Mkwere huyu (Kikwete) kwake maneno hayakuwa tija.

Na kama yalikuwa yakimuumiza basi aliwezi kuhimili mihemuko yake ingawa kwenye utawala wake waandishi waliathirika kwa kuvamiwa na wengine kuuawa.
Kwenye utawala wa Rais Kikwete, watu walikuwa huru kusema, kujadili na hata kugongana mawazo hadharani na kisha mjadala kuhitimishwa bila kutoana ngeu.

Hulka hii haipo kwa Rais Magufuli, anapoguswa hutaka kujitutumua kwa haraka na pale anapojitutumua mara nyingi hukosea. Hana subira.
Lakini pia wapinzani wanaposema jambo hata kama lina ukweli kiasi gani, yeye huliingia kwa pupa hatimaye hujikuta akizama ‘chaka.’

Kinachomtesa zaidi Rais Magufuli ni kutaka kupendwa, kuaminiwa na hata kushangiliwa na kila Mtanzania. Bila shaka atofanikiwa.

Jambo hili ndio linamtia doa kwa kuwa, anaamini kwamba ametawala nyoyo za Watanzania. Anaamini kuwa afanyalo ni lulu kwa Watanzania hivyo anayetokea kumkosoa, anakuwa adui yake.
Haamini kwamba, wapo walio na mawazo mbadala dhidi ya uamuzi wake, mawazo hayo kwake hataki kuyasikia. Anayempigia makofi na kumsifu, huyo ndiye rafiki yake, anayemkosoa anajenga uadui naye.

Naamini maisha kama haya ndiyo yanayomliwaza Rais Magufuli, lakini bila shaka hakuna taifa linaweza kuongozwa na kiongozi mwenye fikra za namna hii, asiyependa kukosolewa.
Rais Magufuli hatofurahia kuwa rais kama ataendelea kuwa na tabia hii. Taifa hili limeondoka kwenye mtazamo wa ‘zidumu fikra za mwenyekiti’ anapaswa kunong’onezwa hivyo.
Walio karibu naye wanapaswa kumweleza kuwa, dunia imehama na Tanzania imehama. Anapaswa kuishi kulingana na wakati na kwamba, sasa si zama za giza.

Anapaswa kuelezwa kuwa siku zinasonga mbele, waliomuona shujaa wanaanza kujutia, uamuzi wa kulipuka umewagusa na kuwaumiza.

Mashabiki wake wanaanza kupukutika. Waliomuona jasiri wanamuondoa kwenye fikra hizo, anaonesha kushindwa mapema.
Makundi yanayoonekana kutoridhika na utawala wake licha ya kumpamba wakati na baada ya uchaguzi yanadhihiri.

Wapo waliodhani Rais Magufuli ni shujaa katika utumbuaji majipu, lakini kumbe sivyo. Sakata la Kampuni ya Lugumu limemshusha, halizungumzi na wala hajihusishi. Watanzania wanajiuliza kulikoni? Kaishiwa nyembe ama sindano za kutumbulia?

Wapo wanaojadili ukanda kwamba, uteuzi wake unazingatia hivyo, hawa wanaoneshwa kutoridhishwa na hatua hii. Kundi hili tayari linamtazama tofauti.

Wapo wanaojadili ubaguzi. Ni kwa kuwa Baraza la Mawaziri aliloliunda limetelekeza Wazanzibari. Kwake Wazanzibari huenda si lolote si chochote.

Hii maana yake hata ile idadi ndogo ya Wazanzibari waliompa kura kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015, watazidi kupungua. Hawa si wapumbavu, wanampa muda tu, hisabu yao ipo wazi.
Kundi lingine ni la Waislam, hawa wanaamini kwamba Rais Magufuli amewatelekeza. Wanaibua maswalia kwamba, wao hawajasoma? hawana nafasi kwenye utawala wake? ama hawakumpigia kura?

Wanajiuliza maswali hayo kutokana na uteuzi wake, ni kwa kuwa wanahesabu wanaotemwa na wanaosajiliwa kwenye serikali yake, ni katika ngazi zote.
Bila shaka kuongoza taifa lenye dini mbili na moja ikaonekana kulalamika kuelemewa, yapo madhara lakini tuombe yasitokee. Wapo waliomshangilia kwenye kundi hili na sasa wamemjengea chuki.

Kundi la waliopenda kuangalia matangazo ya moja kwa moja ya Bunge, nalo linamtazama kwa jicho la chuki. Kwa kuwa amezuia kupata huduma hiyo.

Mikutano ya hadhara amezuia, wapo wanaotaka kujua nini kianendela kutoka kwa viongozi wao na katika mkusanyiko ya hadhara. Hawa wamenyimwa uhuru huo, bila shaka amewachukiza.
Mteule wake ndani ya Bunge, Dk. Tulia Ackson, Naibu Spika naye anakwenda kwa filimbi ya bosi wake (Rais Magufuli), yote haya yanaonekana wazi na kuchukiza wengi.

Idadi ya watu wengi waliokuwa wakimshabikia Rais Magufuli inapungua kila kukicha. Rais Magufuli anajitengenezea uadui mwenyewe hivyo anapaswa kujipima.
Katika yote hayo, anapotokea mtu na kukosoa, Rais Magufuli anaingia woga kwamba, wananchi wataelewa na wanaweza kumwona hafai. Hili ndio tatizo kuu.

Fikra hizi ndizo zinazomlazimu kuhakikisha anaminya sauti za wengi. Anachopaswa kuelezwa ni kuwa, woga huu ndio unammaliza na njia rahisi ni kuacha watu waseme na yeye asikilize.
Rais Magufuli anapaswa kujua kwamba, asitegemee kukosolewa na wabunge wa CCM, njia ya kujua wapi anapoteleza ni kuruhusu sauti huru kuvuma.

Chanzo:Mwanahalisionline

Post a Comment

20 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nafikiri wewe mwandishi unaungaunga habari zako kwa sababu ni mwanachama wa chama nanihii hauna mantiki wala usibitisho uya semayo ili mradi unaropoka kwa kuchanganya mada mara muoga mara anapenda sifa halafu unavyochangia mada zako ni kamavile mhemuko unaokusukuma wacha fitina kwa raisi mkishughulikiwa mnasema mnaminyiwa

    ReplyDelete
  2. Faki Sosi, Mwanahalisi na Udaku, Umejitahidi kutoa Fikra zako na Hata Kufikia katika kudhania labda Mtukufu Raisi Kukosa Nyembe au Sindano za Kutumbulia? Kwa Taarifa yako na wenzako na wote wenye kuto kujiamini au kuto mwelewa mtukufu Raisi JPJM. Ni Hivi... Uwoga Hana na wala Usidhani kuna siku itatokea He is The Main MAN. Ni Jasiri na Shupavu na Mchapa kazi.. Ameweza kuingia katika Mioyo Yetu sisi Watanzania wa All Walks of LIFE na Ametuletea maisha Yenye Matumaini.. Ni kweli atapata MAADUI wengi Kama Wewe na wengineo wenye kufanana na wewe au wanaotumiwa watu kama wewe. Nadhani unajijua wewe mwenyewe na waliokutuma ajili ameweza Kuziba Mianya Mingi mliyo kuwa mkiitumia ya kujipatia maisha HEWA... Kwa hiyo ni jambo la kawaida mtajaribu kuleta kila chokochoko ili mradi kwamba muonekane nyinyi mko katika usawa na sisi na mtufuku Rais JPJM tuko upande wa pili,,,, Tunakwambieni Serikali yetu hii ya Awamu ya Tano Iko kwa ajili ya Kumtumikia Mtanzania Na Hatuto sita Kumshughulikia yeyote ambaye atakuwa na Dhamira kama zako.. Na tunawaahidi Watanzania wenzetu kwamba Nchi iko katika Amani na itaendelea kuwa katika Amani na Upendo ,,, Na hatutosita kumshughulikia yeyote anayetumiwa na maadui wa ndani au Nje walioguswa na Kasi yetu.. Hapa ni Kazi Tu...

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umemfahamisha juu juu tu na akiendelea na chokochoko basi tuta mshughulikia na hao waliomtuma

      Delete
  3. Hii makala yako ndiyo ya Wale Wale ... Tunauliza wewe umetumwa na nani? Tunavyojua na kuona kasi ya Utendaji wa Magu.. Imemgusa kila mtanzania katika aina mbili

    Kama ulikuwa una hewa - BASI KASI IMEKUPITIA VIBAYA
    Kama ulikuwa umedanwa na hewa - BASI KASI IMEKUPA FARAJA

    Imenisikitisha makala yako iliyojaa fikra Potofu na maneno yasiyo na mshiko au mwelekeo.. Mioyo ya Watanzania tunaijua sisi Watanzania ambao kila nyumba na Mtaa na kijiji na Mkoa na Mikoa ambo Mtukufu Raisi ameweza kufanya mambo mengi kwa muda mfupi na anaendelea kuyafanya.. Hivi leo ( kwa sasa) wafanyakazi unawakuta maofisini na wana kuhudumia bila kutaka Rushwa ambayo huko nyuma hufanyi lako bila kupenyeza. Hospitali sasa hivi huduma zimeboreshwa na watu wanajituma... Bandari zetu uwajibikaji na ukusanyaji kodi umekuwa bora na unaridhisha zaidi...Hayo mambo mengine yanayo wagusa saidi... umeshaona yanako elekea na kazi tunayafanyia ,, hakuna sababu ya wewe kuandika usicho kijua kwa ufinyu wa muono wako.... Hapa ni kazi tu... wazembe wapotoshaji wabadhirifu wachochezi matapeli Wana sasa Uchwara Dumilakuwili HATUNA MUDA NAO KATIKA UJENZI WETU WA TAIFA

    ReplyDelete
  4. Hii makala yako ndiyo ya Wale Wale ... Tunauliza wewe umetumwa na nani? Tunavyojua na kuona kasi ya Utendaji wa Magu.. Imemgusa kila mtanzania katika aina mbili

    Kama ulikuwa una hewa - BASI KASI IMEKUPITIA VIBAYA
    Kama ulikuwa umedanwa na hewa - BASI KASI IMEKUPA FARAJA

    Imenisikitisha makala yako iliyojaa fikra Potofu na maneno yasiyo na mshiko au mwelekeo.. Mioyo ya Watanzania tunaijua sisi Watanzania ambao kila nyumba na Mtaa na kijiji na Mkoa na Mikoa ambo Mtukufu Raisi ameweza kufanya mambo mengi kwa muda mfupi na anaendelea kuyafanya.. Hivi leo ( kwa sasa) wafanyakazi unawakuta maofisini na wana kuhudumia bila kutaka Rushwa ambayo huko nyuma hufanyi lako bila kupenyeza. Hospitali sasa hivi huduma zimeboreshwa na watu wanajituma... Bandari zetu uwajibikaji na ukusanyaji kodi umekuwa bora na unaridhisha zaidi...Hayo mambo mengine yanayo wagusa saidi... umeshaona yanako elekea na kazi tunayafanyia ,, hakuna sababu ya wewe kuandika usicho kijua kwa ufinyu wa muono wako.... Hapa ni kazi tu... wazembe wapotoshaji wabadhirifu wachochezi matapeli Wana siasa Uchwara Dumilakuwili HATUNA MUDA NAO KATIKA UJENZI WETU WA TAIFA LA MAENDELEO

    ReplyDelete
  5. Muongo we MKAWA mbona Waislamu wengi wana nyadhifa kubwa serikalini??? Makamu wa raisi , waziri Mkuu na mawaziri kibao tu,, Mara nyingi ni lazima tukubaliane na ukweli kuwa sisi wasilamu shule ilitupiga chenga kwa sababu nyingi tu hakuna haja ya kuzitaji hatutamaliza leo.
    Swala lako la msingi ulilotaka kuandika hapa ni juu ya BUNGE LIVE tu hayo mengine hapo juu ni viungo tu. Sisi huku MTIMBIRA hatuna muda huo wa kuangalia BUNGE LIVE saa 4 asubuhi,, tuache kwenda shamba kulima ili tukae kuwaangalieni mkitoka nje ya bunge huku mmelipwa??? Tena basi sisi wakulima wengi wetu hatuna hata TV na wala umeme haujafika au tutumie Generator??? Hivi nyie mnazo kweli mkulima na BUNGE LIVE??? Hata huko mjini kwenu si wote watakuwa na muda wa kuangalia BUNGE LIVE au kwa akili yenu Watanzania wengi wanaishi wapi na wanaishije hamjui!!!!Njooni uchaguzi ujao mtatutambua kwani hamfanyi tulichowachagulia mtufanyie ambacho ni kuwakilisha sisi,,Sasa hivi mnapotoka nje na mjadala unaendelea hivi mnatuwakilishaje au mnachangiaje??? Asilimia kubwa ya mliowatapeli kutuwakilisha ni sis wakulima kama unalijua hilo!!! Au mnataka tusiende shamba tuwaangalieni Bungeni mkiburuzana??? 2020 si parefu njooni tu.

    ReplyDelete
  6. Hivyo vyote ulivyoongea ni sifa za kiongozi dikteta.

    ReplyDelete
  7. Wewe Mzushi aliyekwambia JpJm anateseka ni Nani? Au ndiyo Uzushi mliozoea Kuzusha wazuhaji

    ReplyDelete
  8. Hii ni Typical Mbowe's Echo.. Wewe Sosi Faki kama unatumiwa au unafikiri utaweza kumuwalisha au Kukiwakilisha kikundi au Makundi ,... Yunakwambia Fupisha hilo.

    Uhuru wa kusema tunanyimwa.....
    Gemoklasia Inabakwa / Inabanwa
    linda demoklasia

    Na ya kwako leo mpya.. Laisi anateswa na Woga!

    Hayo yote hapo juu tuwesha wasikia waimbaji kwa muda... Na tunawaambia NGOMA MTAICHEZA WENYEWE,,, Hapa kazi Tu.

    ReplyDelete
  9. Wewe Mzushi aliyekwambia JpJm anateseka ni Nani? Au ndiyo Uzushi mliozoea Kuzusha wazushaji?????

    ReplyDelete
  10. Raisi Magufuli ndiyo ni muoga.alianza kwa kasi, wengi tulijua kuna mwisho.angerudisha katiba mpya ambayo ingezingatia sheria za nchi ambazo zingemsaidia na zingefuatwa na wanasheria nchini.
    Sikatai kutumbua wake, lakini Chama chake ambscho ndicho chanzo cha matatizo kimemzidi nguvu.viongozi wa ngazi zote za juu za chama chake waliopita ambao bado ni vinara na viongozi kichama si tu wamemzidi nguvu bali bado wanaendesha chama hicho na bado wanasauti kubwa na ni chanzo chote vha matatizo haya anawsogopa, wamemzidi nguvu, na anashindwa kuwatumbua.wanakinga, wansmwangalia hawezi kuwagusa n.a. hii inala kiwewe.watu walitegemea angewatumbua kapinga mwamba.anakula nao sahani moja akijua fika ni wahujumu.kwa namna hii lazima spate hasira anajua mspungufu yake lakini hsna nguvu.anajua watu wanafahamu bali insmrudisha nyuma na inambidi afanye udictstor kwa wapinzsni. Wengi wansochangia hii mada hawafikiri kwa kina madhara yanayosababishwa na shida hii.walioamka wameamka na wanajaribu kuelimisha Taifa.wengi bado giza imetanda kielimu na kifikra na hii ni hatari kwa maendeleo nchini.muda wa maendeleo unapotezwa na kutumika vibays.,

    ReplyDelete
    Replies
    1. Anony 7:24 PM Wakati wa mahaba umekwisha wacha ukereketwa Magu mziki mwingine hata Rome haikujengwa kwa siku moja msichambe kabla ya kupata choo

      Delete
  11. Type vtu vyenye ukweli wewe.....na alyekwambia magufuli anateseka n nan

    ReplyDelete
  12. Nadhani Kichwa cha Habari kilipaswa kuwa KINACHOWATESA WAPINZANI NA MAFISADI NI MAGUFULI. Wewe mwandishi ni mothafucker sijapata kuona. Kumanyoko zako wewe.

    ReplyDelete
    Replies
    1. SAWA SAWA MDAU HICHO NDICHO KILIPASWA KUANDIKWA KINACHO WATESA NI UPINZANI NA MAFISADI NI MAGUFURI. ILE MIANYA YA UFISADI WIZI IMEBANWA. NA WAO WALIZOEA KUOTAFUNA NCHI AU KUWATAFUNA WANACHI WALIO WA KHALI YA KAWAIDA. NA WAPONZANI WANATAKA MADARAKA. SASA WAMEKUWA HAWANA NYIMBO HAWAONI WAPI PA KUSHIKA.WATATOKAJE ILIYOBAKI WANATAFUTA KIKI ILI WATOKE NAO

      Delete
  13. kuna haja ya watanzania kupata elimu kwanza, mawazo na maoni yaliyotolewa na mwandishi wa mada hapo juu yana mashiko makubwa sana lakini watu wanajibu wengine kwa kutukana, hii ni hatari kubwa na inaonesha ni kwa jinsi gani elimu bado inahitajika sana kwa watanzania, ila ninachoamini mimi tusubiri muda kidogo na yakiwafika shingoni mtasema wenyewe ila kwa utawala huu kuna hatari ya kujenga kizazi chenye woga na kisichoweza kuthubutu. hii inamaana kuwa kusoma hujui lakini hata picha huoni?

    ReplyDelete
  14. Mnazunguuka si mmwambie tu huyu mwandishi wa makala ni kibaraka wa chama cha wachaga....
    Mlitupigia kelele sana dunia nzima kuwa Mzee Jk ni raisi dhaifu, yule kibaraka wenu alikuwa mbunge wa ubungo mmesahau alimtukana mzee Jk kuwa ni raisi dhaifu na hakumjibu wala kumshughulikia, Kuna siku pia alisimama yule babu yenu mfadhili wenu wakati bado yupo bungeni mwaka jana alijotutumua kusimama na kuanza kusema ooh nchi inahitaji maamuzi magumu nchi imekufa haina mwelekeo nchi inahitaji mtu jasiri na shupavu atakakuwa na ujasiri wa kufanya maamuzi magumu,

    Tatizo lenu ni kuwa mmezowea uongo mihemuko na sifa zisizo na tija, Sasa nyie ndio mnaotakiwa kuelewa kuwa watanzania tunazidi kuwaelewa na kuwafahamu kuwa hamna jipya.

    ReplyDelete
  15. Mnazunguuka si mmwambie tu huyu mwandishi wa makala ni kibaraka wa chama cha wachaga....
    Mlitupigia kelele sana dunia nzima kuwa Mzee Jk ni raisi dhaifu, yule kibaraka wenu alikuwa mbunge wa ubungo mmesahau alimtukana mzee Jk kuwa ni raisi dhaifu na hakumjibu wala kumshughulikia, Kuna siku pia alisimama yule babu yenu mfadhili wenu wakati bado yupo bungeni mwaka jana alijotutumua kusimama na kuanza kusema ooh nchi inahitaji maamuzi magumu nchi imekufa haina mwelekeo nchi inahitaji mtu jasiri na shupavu atakakuwa na ujasiri wa kufanya maamuzi magumu,

    Tatizo lenu ni kuwa mmezowea uongo mihemuko na sifa zisizo na tija, Sasa nyie ndio mnaotakiwa kuelewa kuwa watanzania tunazidi kuwaelewa na kuwafahamu kuwa hamna jipya.

    ReplyDelete
  16. Duuh,eti hawajasona unauhakika na unaloandika??

    ReplyDelete
  17. Duuh,eti hawajasona unauhakika na unaloandika??

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad