June 21 2016 Mbunge wa Nchemba Juma Nkamia alisimama bungeni kuomba mwongozo wa bunge kujadili tukio la mtuhumiwa wa kesi ya kumtukana Rais Magufuli kuchangiwa fedha na watu kwa ajili kulipa fidia, kitendo kinachoashiria dharau. Mwongozo wa Nkamia ukaungwa mkono pia na Mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde.
Nkamia alisema…
’Kuna mtu alimtukana Rais na akahukumiwa kwenda jela au kulipa faini ya milioni 7, alilipa nusu ya faini ile na akaruhusiwa aondoke akatafute fedha nyingine. Nilitaka wanasheri watusaidie, hivi kumtukana Rais wa nchi alafu yule aliyetukana anaruhusiwa akatafute fedha za kulipa‘ –Juma Nkamia
‘Siku ya kukabidhiwa fedha anaita na waandishi wa habari, na baadhi ya wabunge humu ndani wa chama fulani walionyesha wananchangia fedha yule mtu ili akalipe faini. Kwahiyo ni maana kuwa alitumwa na chama hicho akamtukane Rais.’ –Juma Nkamia
‘Sasa naomba kujua sio dharau kwa Rais? sheria inaruhusu jambo hili kufanyika? na kama mimi leo nikahukumiwa kwa kesi ya kuiba kuku siwezi kuruhusiwa kutafuta fedha, iweje mtu huyu akaruhusiwa kutoka nje kutafuta fedha na bado akaonekana watu wakimkabidhi fedha? hizi ni dharau kwa taifa kwa ujumla‘ –Juma Nkamia
Kwa tusi aliotukanwa huyo raisi?kwani yeye mungu?mbona jk alikuwa anatuknwa lakini hatujawahi ona aina hii udikteta?
ReplyDeleteSijui tunaenda wapi,mimi naamini kijana angeomba msamaha yasingefika kote huko japo hata hakuthubutu wala kushauriwa kuomba msamaha kwa kosa alilotenda,mbaya zaidi inaonyesha kuna watu na elimu zao wako nyuma yake.Tuombee nchi yetu.
ReplyDeleteInataka moyo kuwa kiongozi Tanzania
ReplyDeleteJaman kwani kuchangiwa ni kosa nalo??watu wamejitolea kumsadia mahakama inachotaka si faini ikamilike au kuna lingine...au mimi ndo sielewi..huku tuendako sijui...
ReplyDeleteHawa watu wanao lalamika sijui wanataka nini kwa watz hivi kweli mtu ni kosa la kwanza na hukumu imetoka wasamalia wema wameona ni bora kumchangia ili mambo yaishe kuna ubaya gani hapo jamani!!? mbona kuna watu wameiba mabilioni na wamepewa vifungo vya nje!! ebu acheni uchochezi wa kisiasa jamani da!!
ReplyDeleteHapo wewe ndio mchochezi wa siasa.Japo kuwa mimi ni CHADEMA lakini kwa hili hebu tuwe wakweli,unadhani angekuwa ni mwanafunzi kutoka CCM hao waliojitolea kuchanga wangemchangia eti kisa ni mwanafunzi?Nchi ni yetu,hatumkomoi mtu bali tunajikomoa sisi wenyewe,tunapandikiza maovu pasipotakiwa,ingekuwa vyema hao waliochanga wangemshawishi kwenda kuomba msamaha kwa kosa la kutukana.Au ungeshuhudia majibu aliyokuwa anajibu kijana nadhani kama wewe ni muungwana usingesema hivyo.MUNGU WETU NA ATUSIMAMIE.
Deleteacheni ujinga nyinyi mnaomtetea, kama angetukanwa baba yako au mama yako ungekubali? neno "samahani" ni dogo sana ameshindwa hata kusema samahani? unafiki mtupu kwendeni zenu
ReplyDeleteHapo haktukanwa Baba yako au mama yako pumbafu wewe , Umesoma wewe jaribu kulinganisha na kulinganuwa , mlimpa nafasi kusema samahani ,? hayo alikuwa anatakiwa kuyafanya hakimu
DeleteElimu chache udhia kweli , wanasema wanaume watanzania 100 basi ni watatu tu wamesoma hadi shahada ni kweli ?
Hapo haktukanwa Baba yako au mama yako pumbafu wewe , Umesoma wewe jaribu kulinganisha na kulinganuwa , mlimpa nafasi kusema samahani ,? hayo alikuwa anatakiwa kuyafanya hakimu
DeleteElimu chache udhia kweli , wanasema wanaume watanzania 100 basi ni watatu tu wamesoma hadi shahada ni kweli ?
dawa yake ipo
ReplyDeletejamani kwani sheria iliyotumika kumhukumu huyu kijana ni ya Tanzania au Ya Kenya? basi mnaolalamika kijana kachangiwa nadhani mngetoa maoni sheria irekebishe kwanza? pia msijisahau makali ya upanga kwa kuwa mmeshika mpini?
ReplyDeletekeshalipa faini nini tatizo? acheni shetani apite fanyeni kazi za kujenga taifa sasa.
ReplyDelete