Kumekucha CCM vs Ukawa

MAMBO yanazidi kwenda mrama kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), anaandika Dani Tibason.

Msimamo uliotolewa na Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha) unaakisi mwanzo mpya wa msuguano wa kisiasa nchini.

Tayari Bavicha wametangaza msimamo wa kutoshirikiana na vijana wa CCM katika tukio la aina yoyote.

Mbali na kutangaza msimamo huo pia wametangaza kuzuia mikutano yote ambayo itaandaliwa na CCM kama inavyozuiwa ya Chadema.

Msimamo huo umetolewa leo na Julius Mwita, Katibu Mkuu wa Bavicha wakati akizungumza na waandishi wa habari Dodoma.

Mwita amesema, kutokana na kitendo cha Serikali ya CCM kushirikiana na Jeshi la Polisi kuzuia mikutano ya Chadema kinaonesha wazi kuwa, serikali ina mpango wa kuhakikisha inaua upinzani jambo ambalo haliwezi kukubalika.

Amesema, kutokana na hali hiyo kwa sasa Bavicha wametangaza kutoshirikiana na vijana wa CCM katika mazingira yoyote ikiwa ni pamoja na katika masomo, nyumba walizopanga, misiba na katika majamga mengine mbalimbali.

“Kutokana na kuwepo kwa vitendo vya kikatili vinavyofanywa na Serikali ya CCM vya kuzuia mikutano ya upinzani, sasa tunatangaza sisi vijana wa Bavicha hatutashirikiana na wanachama wa CCM kwa njia yoyote ya kijamii wala kimaendeleo.

“Natangaza kwa vijana wote wa Chadema hatutashiriki katika mazizi, hatutashiriki kusoma nao wale waliopo katika vyuo, hatutashiriki sherehe mbalimbali zinazowahusu wao wala hatutashiriki katika jambo lolote la kimaendeleo, na hii ni msimamo wetu.

“Pia tunawapongeza wabunge wetu kwa kususia shughuli zote za ambazo zinafanywa na CCM kwani kwa kufanya hivyo inaonesha kuwa sasa tumechoka na uongozi wa kiimla,” amesema Mwita.
Hata hivyo amedai, Rais John Magufuli ni muoga kuliko marais wote kwa kuwa ni rais ambaye hapendi kukosolewa na kuambiwa ukweli pale ambao amekuwa akikosea jambo ambalo anatakiwa kujitafakari na kujikosoa.

“Sasa vijana vijana tumejipanga kuhakikisha Jeshi la Polisi linazuia mikutano au mikusanyiko ambayo inafanywa na CCM na ikumbukwe kuwa, 23 Julai mwaka huu CCM watakuwa na vikao vya kumkabidhi rais Magufuli kuwa mwenyekiti wa CCM.

“Sasa tunataka Jeshi la Polisi kuzuia mkusanyiko huo na kama haitawezekana vijana wa Chadema na Ukawa watazui mikutano hiyo.

“Haiwezekani mikutano ya Chadema ikawa ndiyo inayozuiliwa wakati mikutano na mikusanyiko ya CCM inaendelea kufanyika, jambo hili kamwe haiwezi kukubalika na tunasema sasa imefika mwisho wa uvumilivu,” amesema Mwita.

Edward Simbeye, Katibu Mwenezi Bavicha amesema, yeye ndiye mratibu wa mahafali za wanafunzi wa Chadema vyuo vikuu (Chaso) nchini hivyo polisi walipaswa kumkamate yeye na si kuzuia mahafali hayo.
Tags

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Bange zingine tabu sana hivi nyie Bavichwa na nyinyi mmekuwa serikali mtapasuka msamba

    ReplyDelete
  2. Mmmh,Jamani mimi ni BAVICHA lakini nashindwa ku-cop na nyie wenzangu,nyie mnatumia nini?Au kipi hasa mpaka tufikie huko?Tunabaguana hadi kwenye mazishi?kweli jamani,tumuogope Mungu.

    ReplyDelete
  3. Mimi hata nikute ccm kaanguka hapo sitoi msaada na yeye asinipe msaada period...

    ReplyDelete
  4. Julius Mwita, Nakuona kwenye picha! Umuri wako siujui zaidi ya kuweza kukisia..
    Uliyoandika uhakika sina kama mzungunzaji ni wewe au umeandikiwa au umeleta fikra za kutumwa na waliokutuma. Je wazazi wako wako hai? Je una ndugu ? je umesha ona nakubarikiwa kizazi na mungu? nadhani ukiweza kuyajibu haya.. Basi utaweza kuzinduka na kuweza kutafakari aliyekupotosha na kukujenga katika Chuki ya kupita kiasi ana lengo gani na wewe na kwani kaamua kukutumia wewe? Nakukumbusha tu kuwa Watanzania ni Wamoja Nchi yao imejengwa kwa misingi ya UZalendo / Upendo / Amani Na Usalama... Kingine chochote kinyume na hayo... Hatutakuelewa wala hatutopendezewa uwe mmoja wa Jamii yetu.. Rudi kwa Baba Na Mama wakupe muongozo Wa Maisha na Kuishi na Watu. Na kuomba na Ningependa utoe kauli nyingine ya kuwaomba Radhi wote tunaosoma haya maneno yanayodai kuwa yako yaliyojaa CHUKI isiyo na Kifani... Wewe ni Mtoto wetu na lazima tukuongoze kama ulikosa Wa kukuongoza... Na Imani wazazi wako watakuwa wa kwanza KUKUKEMEA KWA HILI.

    ReplyDelete
  5. Julius Mwita, Nakuona kwenye picha! Umuri wako siujui zaidi ya kuweza kukisia..
    Uliyoandika uhakika sina kama mzungunzaji ni wewe au umeandikiwa au umeleta fikra za kutumwa na waliokutuma. Je wazazi wako wako hai? Je una ndugu ? je umesha ona nakubarikiwa kizazi na mungu? nadhani ukiweza kuyajibu haya.. Basi utaweza kuzinduka na kuweza kutafakari aliyekupotosha na kukujenga katika Chuki ya kupita kiasi ana lengo gani na wewe na kwani kaamua kukutumia wewe? Nakukumbusha tu kuwa Watanzania ni Wamoja Nchi yao imejengwa kwa misingi ya UZalendo / Upendo / Amani Na Usalama... Kingine chochote kinyume na hayo... Hatutakuelewa wala hatutopendezewa uwe mmoja wa Jamii yetu.. Rudi kwa Baba Na Mama wakupe muongozo Wa Maisha na Kuishi na Watu. Na kuomba na Ningependa utoe kauli nyingine ya kuwaomba Radhi wote tunaosoma haya maneno yanayodai kuwa yako yaliyojaa CHUKI isiyo na Kifani... Wewe ni Mtoto wetu na lazima tukuongoze kama ulikosa Wa kukuongoza... Na Imani wazazi wako watakuwa wa kwanza KUKUKEMEA KWA HILI.

    ReplyDelete
  6. Hivyo weewe Umelipwa au Umetumwa kumwaga SUMU?

    ReplyDelete
  7. Mhhhhh Mimi ni Chadema damu damu Lakini hii siyo Yetu. Kulikoni.

    ReplyDelete
  8. Dani Tibason Bora Ulivyo leta Hii Mpya ya Julius Mwita... Kweli ELIMU ukikosa ni Matatizo sasa sindiyo mana Suala la Elimu linaangaliwa Upya.. Sasa utasema nini kuhusu huu utumbo na Chuki na mameno yasiyo eleweka Basi mradi yuko yuko anataka sifa na hajui anachozungumza.

    ReplyDelete
  9. Hii nguo aliyovaa nimeshamuona nayo mtu .. vile nani? sasa yeye kaipata vipi? isije kuwa amekunywa? au ndiyo sare sare.

    ReplyDelete
  10. Hawa watoto wamekosa mwelekeo. Wanadhani wana uwezo wa kupambana na Serikali/Dola. Wakumbuke kwamba wazazi wao ndo watakao umia pale watakapotendwa vilivyo. Waoneeni huruma wazazi wenu. Ikumbukwe kuwa they are one digit in a million, kuondoka kwao hakusababishi nyumba kuvuja.

    Mimi ni kijana na Siasa za nchi hii nazielewa fika, lakini katika hilo la Siasa za Ubaguzi siwaungi Mkono. WALAANIWE KAMWE KWA SIASA ZA CHUKI

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad