Kuna Unyanyasaji Mkubwa Tanzania – Maalim Seif

Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad ameiambia jumuiya ya kimataifa kuwa wapinzani hapa nchini wanakandamizwa na kunyanyaswa.

 Maalim Seif aliyasema hayo alipokuwa akihutubia mkutano uliondaliwa na Kituo cha Elimu cha Kimkakati cha Kimataifa cha Marekani (CSIS) juzi, uliofanyika Washington DC nchini Marekani.

 Alitoa mfano wa yeye kuhojiwa na polisi 11 kwa saa tatu na kijana aliyehukumiwa kifungo cha miaka mitatu au kulipa faini ya Sh7 milioni kwa kumkosoa Rais John Magufuli kwenye ukurasa wa facebook.

 “Tunashuhudia mmomonyoko wa hali ya juu wa demokrasia sasa hivi… na hali hii itazidi miezi michache ijayo,” alisema.

Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mmmh,sijui ni uandishi au ni kweli Maalim Seif alitamka hivyo,
    hivi kumuita mtu BWEGE ni kukosoa?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tatizo kubwa ninaloliona hata kama mtu kafanya kosa,lakini kama ni wa chama pinzani atatetewa tu.

      Delete
    2. na kuna mwingine naye alimwita mtu KILAZA ni kukosoa? amehukumiwa:?

      Delete
  2. hilo ni tatizo la watanzania wengi maana tuko kivyama zaidi kuliko uhalisia

    ReplyDelete
  3. kwa kweli hata mimi sio ukawa wala sio ccm ila kusema kweli unyanyasaji ni wa wazi kabisa!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad