Kwa Hili la Rais Kuendesha Bunge Kwa Remote Control Tutampinga Kwa Nguvu Zote-Zitto Kabwe

Mhe. Zitto Kabwe aliandika haya kupitia ukurasa wake wa Facebook na kusema hawatakubali kuona wanarudishwa nyuma au kuona misingi ya taasisi za uwajibikaji zikibomolewa.

"Rais Magufuli tunakuunga mkono kwa dhati kupambana dhidi ya ufisadi. Tunakupinga kwa nguvu zote kupambana dhidi ya demokrasia. Kuanzia mwanzo tumekuunga mkono dhidi ya ukwepaji kodi, ubadhirifu, uvivu na uzembe. Tangia mwanzo tulionya kuwa ni lazima udhibitiwe na Bunge ili ufanye kazi kwa mujibu wa Katiba. Hivi sasa wewe Rais ndio unaendesha Bunge kwa remote control. Tutakupinga kuturudisha nyuma. Hutafanikiwa kamwe kubomoa misingi ya taasisi za uwajibikaji tulizoanza kuzijenga". Alisema Zitto Kabwe.

Mbali na hilo Zitto Kabwe alisema Tanzania inataka uongozi madhubuti na siyo utawala wa imla na kudai watanzania hawatakubali kurudi nyuma katika utawala wa imla.

"Narudia nukuu muhimu sana " ukitaka kutawala tawala peke yako. Ukitaka kuongoza ongoza na wenzako". Rais Magufuli Tanzania inataka Uongozi madhubuti na sio utawala wa imla. Huko tumeshatoka na Watanzania hawatakubali kurudi huko". Aliongeza Zitto Kabwe

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. pole sana zitto nakushauri endelea na maandalizi ya ndoa yako kwa sasa ni muda mwafaka kwani umesimamishwa kihalali kilaza wewe

    ReplyDelete
  2. chupi zimewabana

    ReplyDelete
  3. Udaku... Hii ulishaletwa na tumesha Comment sana!!!! usirudie rusdie kwa udaku wako... Zitto hana mpya!! tumeshamwambia aje kijiweni tutadiskasi.. na kumuelewesha maana ya misamiati asivyo jua kuitumia na kumtafutia ustaarabu mwingine wa biashara ya Dagaa... Siasa uchwara imesha mshinda!! Elimu na umahiri hivi vigezo vyote hana...

    ReplyDelete
  4. Udaku... Hii ulishaletwa na tumesha Comment sana!!!! usirudie rusdie kwa udaku wako... Zitto hana mpya!! tumeshamwambia aje kijiweni tutadiskasi.. na kumuelewesha maana ya misamiati asivyo jua kuitumia na kumtafutia ustaarabu mwingine wa biashara ya Dagaa... Siasa uchwara imesha mshinda!! Elimu na umahiri hivi vigezo vyote hana... Kiasi anaonesha ametumwa au amechanganyikiwa anachanganya mada bila mpango uhuru pia hajui tumepata lini!!!

    ReplyDelete
  5. this guy ZITO talks too much and all in nonsense grow up man

    ReplyDelete
  6. Huna lolote wewe mmezoea yale mabunge hewa yaliyopita kwa hili hamuoni ndani. Hiyo ya kujitutumua kwako kisiasa utahangaika sana lakini ukweli utabakia Magufuli ndio Rais wa Nchi hii na sio wewe kibaka mwizi na tapeli mkubwa wa kisiasa. Kwani ni nani asiyekujua hila zako tumeishazijua hila zako hapa hupati kitu. Utaishia kufilisika kwa uroho wako wa madaraka.Usituletee siasa zako za kutafuta uongozi na utawala. Utawala hautafutwi hivyo utashangaaaa hapa kazi tu.

    ReplyDelete
  7. Na hata kama ni uongozi tunawataka watu wengine na sio wewe. Wewe hatukutaki tumekuchoka hata ubunge wenyewe ni washidashida utaisoma namba mwaka huuuu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad