Kwanini makampuni makubwa ya mafuta SHELL na BP yalijiondoa kufanya biashara Tanzania ?

Kampuni ya SHELL japo ilikuwa ama bado mpaka sasa iko kama NEMBO HALISI ya biashara ya mafuta nchini , lakini miaka mingi iliyopita ilijiondoa kufanya biashara nchini mwetu .

Juzi juzi miaka michache iliyopita tumeshuhudia kampuni lingine kubwa la BP , kampuni pekee lililoaminika kutochakachua mafuta nalo likifunga virago vyake.

Nilikuwa nawaomba wadau waliozifahamu sababu za makampuni haya kutukimbia watuwekee hapa tuzijadili na kujifunza , na ikibidi tujirekebishe ili tusije kukimbiwa na makampuni mengine .

By Erythrocyte/JF
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Inasemekana BP imejiondoa Afrika na sio Tanzania tu, lakini sin uhakika

    ReplyDelete
  2. Kwetu hapa bi mdogo awamu ya nne ndo mmiliki mkubwa wa uagizaji mafuta
    Hata mita hazikufungwa bandarini kisa yeye yeye bibi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hmmm huyo wa awamu ya nne alikuwa ni shidaaa!!! Yaani unajiuliza alikuwa kikazi kajiriwa na Taifa hili wanachi wamemchagua Kwa kumuamini kwa yote au alikuwa yupo zaidi kutafuta maslai mfukoni mwake kwa njia yeyote ile ili awe bwana tajiri

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad