List ya Nchi 11 zinazoongoza Kwa Amani na Usalama Duniani

List ya nchi zenye usalama zaidi duniani kwa mwaka 2016 imetoka hivi karibuni ambapo nchi 11 zimetajwa kuongoza kwa kuwa na usalama na amani zaidi. List hiyo ilihusisha mataifa 163 ambapo ilijulikana yale yanayoongoza kwa amani na usalama pamoja na yale ambayo ni hatari zaidi kuishi kutokana na hali ya usalama.

Toleo la 10 la kila mwaka lililotolewa June 8 2016 limetaja viwango vya amani na usalama kupitia system ya ramani  shirikishi ya mtindo wa rangi za kujificha, kila nchi ilitolewa alama kati ya 5, nchi zenye alama chini ya 5 ndio zenye hali kubwa ya usalama na amani na zilizoizidi namba 5 ndizo hatari zaidi.

Ulifanyika uchambuzi wa mambo 23 chini ya makundi matatu, Usalama na amani ya taifa, Migogogro ya ndani na nje ya nchi pamoja na huduma za kijeshi. Nchi ya Iceland inatajwa kuongoza kwa kuwa na amani zaidi kutokana na utulivu wa jamii yake.

Nchi za ulaya zinaongoza kutokana na kutokuwa na migogoro ya ndani na nje pamoja ya hali ya utulivu kwa ujumla, japokuwa Afrika inasifika kuwa na nchi zenye  amani hakuna hata nchi moja ya Afrika iliyopo katika list. Hata hivyo imetoka pia list ya nchi ambazo usalama wake ni wa chini sana ambapo nchi za Syria, Iraq, Sudan Kusini, na Afghanistan .

CHANZO: independent.co.uk

ORODHA YA NCHI 11 ZINAZOONGOZA KWA KUWA NA USALAMA NA AMANI ZAIDI DUNIANI

11.Finland – 1.429

10. Slovenia – 1.408

9. Japan – 1.395

8. Canada – 1.388

7. Switzerland – 1.37

6. Czech Republic – 1.36

5. Portugal – 1.356

4. New Zealand – 1.287

3. Austria – 1.278

2. Denmark – 1.246

1. Iceland – 1.192
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Pamoja na vishindo vyote vya polisi ,ccm
    Tanzania hatumo
    Kweli dunia inajuwa

    ReplyDelete
  2. yah dunia inajua kuwa tunachinjana kama kuku na albino wanaisha kwa kuuwawa, wazee na vikongwe kunyongwa kila uchao kwa kuhusishwa na imani za ushirikina, na bado migogoro ya kisiasa isiyoisha, na ishu ya uchaguzi zanzbar ndio kabisa... eti kisiwa cha amani???!!!!

    ReplyDelete
  3. Nyie mnacho-comment akijui na mnarukia mambo. Unajua mchakato wake? mbona nchi kama Finland na Sweden kunatokea matatizo ya millipuko ya mabo kila kukicha lakini zimo? hapa kinachoangaliwa ni setup ya suala la kiusalama na namna ya kuweza kupambana na uhalifu. Mfano nchi hizo zilizotajwa ikitokea wewe umepata tatizo lolote la kiusalama itawachukuwa polisi dakika 5 kukufikia na kutoa msaada husika. Pili yakitokea majanga ya asili kama tetemeko la ardhi basi uwezekano wa kunusuru maisha ya watu ni zaidi ya asilimia 80%. Kila eneo la makazi ya watu linamilikiwa na vyombo vya ulinzi na usalama na muda wote matukio ya nchi husika yanaonekana kwa kutumia teknolojia hasa camera na satellites. Sasa linganisha na nchi yetu halafu ndiyo utoe comments zako usikose uzalendo. Mmeisha sahau juzi tu kuwa nchi inayovutia kuishi uniani Tanzania ni ya pili? Acha uana -harakati muwe na uzalendo nanchi yenu au nyie siyo Watanzania? basi rudini kwenu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad