Lulu Michael Arudi Chuo, Anachukua Telecommunication Engineering

Msanii mahiri wa filamu Elizabeth Micheal ‘Lulu’ amerudi chuoni na kuamua kuchukua kozi ya Telecommunication engineering.

Muigizaji huyo ameweka wazi anachosomea baada ya mashabiki katika mtandao wa Periscope, kutaka kujua anasomea nini baada ya kupost video mbalimbali katika mtandao huyo huku akizungumzia maswala ya chuo.

“Jamani nimechoka kuulizwa nasomea nini, nasomea nini, nachukua Telecommunication engineering,” alisema Lulu.

Muigizaji huyo hakupenda kuweka wazi ni chuo gani anasoma, lakini aliweka wazi wiki hii naingia katika mitihani.

Lulu ni miongoni mwa wasanii wachache wa filamu walioamua kurudi darasani na kuongeza maarifa.

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Basi tu utoto ulimsumbua mapema,Lulu ana akili na sasa angekuwa mbali sana.HONGERA SANA LULU.

    ReplyDelete


  2. Telecommunication Engineering

    ReplyDelete
  3. ni heri apate elimu itayomsaidia maisha ya baadaye kuliko kutegemea bongo movie wakati soko la bongo movie limeshakufa tangu zamani

    ReplyDelete
  4. Kesi yake iliishiaga wapi ?

    ReplyDelete
  5. Sijaelewa hiyo telecom.... Maana siyo cozi ya kirembo.... Teeeh

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad