Madereva Taksi Wagomea Huduma ya Usafiri wa Uber, Waeleza Wanachokiona

Baada ya kampuni ya huduma ya usafiri ya Uber kuzindua huduma yake jijini Dar es Salaam wiki kadhaa zilizopita, madereva taksi wa jiji la Dar es salaam wanaonyesha kutoielewa huduma hiyo na kudai umekuja kuwaaribia biashara yao ya taksi.

Jiji la Dar es salaam limekuwa jiji la 475 duniani kujiunga na mtandao huyo ambao unatoa huduma ya usafiri katika majiji mbambali duniani.

Huduma ya mtandao wa Uber, huwaunganisha madereva na wasafiri kwa muda muafaka, kwa kubonyeza tu kitufe. Au ukiwa unatoka na marafiki kwenda mjini kibiashara, au kuangalia vivutio vya kitalii, Uber hutoa njia rahisi yenye unafuu kufika kila mahali.

Mmoja kati ya madereva taksi wa Namanga jijini Dar es Salaam, Mitawa Ramadhani amesema usafiri huo umekuja kuwakandaniza kutokana na huduma hiyo kuandaa bei ambazo haziendani na umbali ambao wanatembea.

“Uber nimeshazungumza nao, nimeshaona mwenyendo wao na kufanya nao kazi, nikapata nafasi kubwa ya hasara, sikuweza kufurahia kufanya biashara yenye hasara kubwa na kuwa na faida kidogo, sikuwaambia na nikaweka ndani ya nafsi, na sasa hivi sipo ridhaa na wao kufanya nao kazi,” alisema Mitawa.

Pia dereva mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Ramadhani Libui, alisema alikuwa ana mpango wa kwenda kujiunga lakini baada ya kuona kilicho wakuta wenzake, ameghaili kujiunga.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad