Jana Mtukufu wa nchi mkuu sana Rais Magufuli wakati akiwaapisha wakuu wa Mikoa wapya na wakuu wa wilaya kula kiapo cha uadilifu alitamka ''Tulikuwa tunafuatilia kwenye revenue, yuko mtu mmoja alikuwa anafanya transaction ya fedha kila dk 1 kati ya milioni 7 na 8. Serikali ilikuwa inapoteza pesa, bahati nzuri huyo mtu yuko mikono salama, tunatafuta jinsi ya kuzirudisha''
Kauli hii imeniacha njia panda, kwamba huyu mtu
- Alipata wapi ujasiri wa kuhamisha kiashi hicho cha fedha kila baada ya dakika moja?
- Hizo fedha zilikuwa kwa wema au ubaya?
- Huyo mtu ni nani mpaka asitajwe wananchi wakamjua?
- Yuko mikono salama, Hiyo mikono salama ni ipi kwa mtu wa namna hii?
- Watazirudisha vipi pesa zote alizohamisha?
- Amekuwa akihamisha pesa kwa muda gani na mpaka anawekwa mikono salama alikuwa kashachukua kiasi gani?
- Atapelekwa mahakama ya uhujumu/mafisadi?
By Chachu Ombara/JF
Mmmh sie yetu macho na masikio...
ReplyDeleteWewe mwenye huna uhakika na hili ndio maana umeweka kimafumbo,kama unajua A-Z weka wazi kila kitu,mpelekee JPJM halafu tuone kama hatatumbuliwa.MJENGA NCHI NI MWANANCHI MWENYEWE.
ReplyDeleteDaaa hii nayo Kali. Kweli umasikini utawaishia Watanzania walio wengi kwa mtindo juu? Wa watu wachache kulibia Taifa na kujilimbikizia. Ni ndoto ya alinacha kwa mtanzania wa kawaida kutoka katika wimbi la umasikini, na kukosa huduma muhimu zote katika Taifa lake. Ataendelea kunyonywa kuibiwa na kukandamizwa. Si ajabu ndio maana wengi wachache waliozoea kufanya uzandiki wao kutaka kujifanya wanauchukia utawala Mtukufu wa sasa ni kwa sababu tu ya mabaya yao ya uzandiki wanao lifanyia Taifa hili. Au watu wengine wote wa Taifa hili. Na kuwaweka katika wakati mgumu. Katika dunia hii nao ili wakiishi maisha ya juu na kifahari zaidi. Na wengine kutabika kwa wanayoyafanya
ReplyDeleteAfrica kuna maneno
ReplyDeleteSometimes we European we don't understand
Ndo Tanzania yenu hiyo. Mkiambiwa Ukweli mnaupotosha Ukweli.Rais amewambia mumuombee sana. Anakutana na mabo makubwa sana na ya Ajabu.
ReplyDeleteILA MBONA KAMA NA WEWE MWANDISHI UNAMJUA,SI UMTAJE.
ReplyDelete1.Ujasiri kaupata kwa mafisadi wenzie walio ngazi za juu.
ReplyDelete2.Ni kwa ubaya,maana hakuna pesa za wema zikatoka bila kibali na kwa haraka haraka hivyo.
3.Iko siku tutamjua maadam mkuu kamtaja.
4.Mikono salama ni TAKUKURU,POLICE,JESHI.
5.Hata wakitaifisha mali zake ni namna moja wapo ya kurudisha.
6.Ni kwa muda gani wamehamisha na kiasi gani tuwaachie vyombo
wakati ukifika tutajulishwa.
7.Ndio maana kuna mahakama ya mafisadi kwa hiyo atapelekwa.
Wee anonymous, hapo juu, una akili sana. Ningejua upendeleo wako ningekupa ofa ya kinywaji baridi! Majibu yako yamejaa ukomavu na uzalendo.
DeleteTuendelea kuiombea nchi yetu. Tanzania bila ufisadi, inawezekana.